Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Urembo wamtumbukia nyongo.


Jitihada za kutafuta urembo wa ziada za mwanamke mmoja wa nchini Marekani zilimtokea puani baada ya sura yake kuharibika vibaya kiasi cha kuwa vigumu kutambulika alipoamua kujidunga sindano za urembo za silikoni.Mary Johnson mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa California nchini Marekani katika jitihada zake za kutafuta urembo wa ziada aliamua kufanya upasuaji wa kurekebisha sura yake aonekane kijana na mrembo. Lakini Mary ambaye ni mama wa watoto watatu alipoambiwa kuwa upasuaji wa kurekebisha sura yake utamgharimu maelfu ya dola za Marekani, aliamua kughairi kufanya upasuaji huo hospitalini na kuamua kutumia njia za kujidunga sindano za silikoni. Baada ya kufanya utafiti kwenye Internet Mary alinunua sindano za kimiminika cha silikoni kwa dola 10 tu na kujidunga mwenyewe kwenye mdomo wake na kwenye mashavu yake. Badala ya sindano hizo kumfanya aonekane mrembo kama alivyotarajia, ziliiharibu kabisa sura yake na kuifanya iwe vigumu kwa mtu kumtambua. Baada ya muda mfupi sura yake ilianza kubadilika rangi na kuvimba na kwenye kona za mdomo wake kulitokea vidonda vikubwa visivyoeleweka. Hali ilikuwa mbaya kiasi cha kusababisha Mary awahishwe hospitali na kufanyiwa upasuaji wa kuifanya sura yake irudie hali yake ya zamani. Hivi sasa ingawa sura ya Mary imerudia hali yake ya zamani, Mary anakiri kujutia uamuzi wake wa kutafuta urembo wa ziada.

source:nifahamishe.com
[ Read More ]

Mama Awauwa Watoto Wake Wanne Akidai Wana Mashetani Wabaya


Mama mmoja nchini Marekani amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne akidai walikuwa wame wameingilwa namashetani wabaya.
Banita Jacks, 33, wa Washington nchini Marekani amefunguliwa mashtaka manne ya mauaji ya watoto wake wanne wa kike wenye umri kati ya miaka mitano na 17.

Banita alikamatwa nyumbani kwake akiishi na mabaki ya miili ya watoto wake ambao maiti zao zilikuwa zikiozea ndani ya nyumba hiyo.

Banita alidai kuwa watoto hao walikuwa na mashetani wabaya na walikufa mmoja mmoja wakiwa usingizini.

Ndugu wapatao 30 wa familia ya Banita waliohudhuria kesi hiyo mahakamani waliondoka mahakamani kimya kimya bila kutaka kusema chochote.

Miili ya watoto hao iligundulika wakati polisi walipoingia nyumbani kwa mama huyo kusini mashariki mwa Washington mwezi januari mwaka jana.

Banita aliwaambia wapelelezi kuwa watoto wake walikuwa wakimilikiwa na mashetani wabaya na walianza kufariki mmoja mmoja wakiwa usingizini katika muda wa siku saba.

Banita aliwaambia pia wapelelezi hao kuwa aliwanyima chakula watoto wake hao kwa muda mrefu kabla ya vifo vyao.

Mchunguzi wa mambo ya kidaktari, Dr. Marie-Lydie Pierre-Louis alisema kuwa kwa kuangalia vielelezo vya idadi kubwa ya wadudu waliokutwa kwenye maiti hizo, miili ya watoto hao ilikuwa ndani ya nyumba aliyokuwa akikaa mama huyo kwa zaidi ya siku 15 kabla ya kugundulika.

Polisi walisema kuwa Banita alizuga amehama kwenye nyumba aliyokuwa akikaa kwa kufunga mapazia yote ya nyumba yake na kuacha kulipa bili za umeme na kuacha barua zake zirundikane mbele ya nyumba yake huku yeye akitumia mlango wa nyuma kutokea.

Banita huenda akafungwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.


SOURCE:nifahamishe.com


[ Read More ]