Kuna uwezekano mkubwa ya baadhi ya watu kupoteza maisha katika msiba huu kutokana na watu kukanyagana! Japo hakuna taarifa kamili!!na huku baadhi ya watu wakiimba nyimbo uku wakikimbia haya ni baadhi ya maneno... "polisi tunamtaka lulu huyo aliyeua
Imeshindikana kabisa kwa jeneza kuingizwa makaburini Kinondoni.Kamati iko busy kuangalia nini cha kufanya
na jeff msangi.twitter.
[ Read More ]
na jeff msangi.twitter.
Mkuu wa majeshi 1988 hadi 1994 General Ernest mwita kyaro afariki dunia.akiwa njiani kuelekea bugando.
[ Read More ]
Msalaba Mwekundu wakiwa stand by na pia msaada unahitajika
Watu wameisha anza kuzima na msalaba mwekundu umeanza kazi yao
Watu wengi wanazidiwa na kuzimia.Jamaa wa Red Cross wanajitahidi kadiri wanavyoweza.They are doing an amazing job
Ni majonzi
Mgeni Rasmi Mama Salma alipowasili msibani na waombolezaji wengine
Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbiliyini alipowasili viwanjani hapo
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiongea na wanahabari
Nnape Nnauye akiongea na wanahabari juu ya msiba huu
Umati wa watu
Millard Ayo & Ephraim Kibonde ndo wanedesha shughuli
Huyu ni kibaka akiwa amenaswa hapo msibani
Jukwaa likfanyiwa maandilizi
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiongea na wanahabari Nnape Nnauye akiongea na wanahabari juu ya msiba huu Umati wa watu Millard Ayo & Ephraim Kibonde ndo wanedesha shughuli Huyu ni kibaka akiwa amenaswa hapo msibani
Kwa habari zilizo tufikia na aliyepo eneo la tukio (Viwanja vya Leaders) ambako mwili wa marehemu Steven Kanumba uliwasili majira ya saa tatu kwa ajili ya misa na kuagwa.
Zoezi la kuaga limeshindikana kwa upande wa umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria hapo baada ya viongozi pekee kupata fursa ya kuaga na kufuatiwa fujo na polisi kushindwa kudhibiti kulingana na idadi kubwa ya waombolezaji.
Hivyo mwili wa msanii huyo maarufu wa filamu unaelekea kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku gari iliyobeba mwili wake ikisukumwa na wananchi waliojipanga barabarani kuelekea makaburini.
Huu ni umati wa watu unao elekea makaburini
Gari lililo beba mwili wa marehemu Steven Kanumba likielekea makaburini
picha na jeff masangi.
mama wa marehemu akiwasili uwanjani hapo
eneza lililobeba mwili wa Marehemu limewasili.Watu wanalia kwa uchungu sana.Wengi wanagombania kuligusa
Kwa mbele
red cross wakiwa uwanjani hapo kutoa huduma.
Msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.
"tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"
"Mtu aliepata mtikisko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.
Daktari mwingine alieshiriki katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo