| FUNDI ujenzi aliyefahamika kwa jina moja la Ally, amekufa baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tisa wakasti akiwa katika shughuli za ujenzi katika ghorofa hiyo. | ||
Fundi huyo alikuwa katika ya nyumba ya Shubas Patel iliyokuwa na ghorofa 12 na alianguka wakati akiwa kazini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema ajali hiyo ilitokea jana, saa 10 jioni, Mtaa wa Sewa na Zanaki Ilala jijini Dar es Salaam. Alisema fundi huyo, akiwa na wenzake wakiendelea na kazi kwenye ghorofa ya tisa, ghafla alidondoka hadi ghorofa ya tatu ambapo alinasa kwenye kizuizi cha mabati. Alisema alipata majeraha kwenye paji la uso pamoja na kuvunjika mkono wake wa kushoto. Hata hivyo wenzake walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na alikufa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo. SOURCE;NIFAHAMISHE.COM | ||
ASKARI mstaafu wa Jeshi la la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Matiko Ng'eng'e (55) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kisu.
Ng'eng'e ambaye alikuwa sanjenti wa jeshi hilo anadaiwa kufanya hivyo saa 11:00 alfajiri ya jana nyumbani kwake Ukonga Mazizini, jijini Dar es Salaam.
Habari ambazo Mwananchi imezipata na kuthibitishwa na Polisi zilisema mauaji hayo yalifuatia mgogoro wa shamba ambalo mtuhumiwa alikuwa ashinikiza liuzwe huku mkewe akipinga vikali mpango huo.
Akisimulia mkasa huo nyumbani kwao, mtoto wa mtuhumiwa huyo, Joyce Matiko (22) alidai kuwa baba yake ana wake wawili wa ndoa na kwamba marehemu alikuwa ni mke mdogo.
Kwa mujibu wa Joyce, mke mkubwa wa baba yake anaishi Banana.
Alisema hata hivyo familia hizo zimekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kuhusu eneo ambalo mke mdogo na watoto wake wamekuwa wakiishi na kwamba mgogoro huo ulitokana na baba yao kutaka eneo liuzwe ili apate fedha za kusafirisha familia kwenda kijijini.
"Muda mfupi kabla ya mauaji ya mama yetu, baba alituita watoto wote watano pamoja na mama na kutukanya tusithubutu kuuza eneo tunaloishi hata kama itatokea yeye amekufa.
Tulishangazwa sana baba kutuita na kutukanya eti tusithubutu kuuza eneo hilo, wakati yeye ndiye kinara wa kutafuta madalali kwa siri ili afanikishe zoezi hilo,"alisisitiza mtoto huyo.
Alisema mara baada ya kikao hicho, baba yao aliwataka warudi ndani wakalale na kwamba walifanya hivyo.
Mtoto huyo alisema ilipofika saa 9:30 usiku alisikia kelele za mama yao akiomba msaada kwamba anakufa na kuomba asaidiwe jambo lilowashtua mno.
Alisema baada ya kusikia kelele hizo waliamua kutoka na kumkuta mama yao akiwa amelala chini huku damu zikiwa zinamtoka kwa wingi mwilini.
"Tulimkuta mama akiwa amelala chini katika dimbwi la damu, lakini baba hakuwepo alikuwa amejifungia chumbani, tulipiga kelele za kuomba msaada na muda mfupi tu majirani walifika na kutusaidia kumtoa kabla polisi kufika," alisema.
Alisema baada ya polisi kufika walimchukua mtuhumiwa (baba yao) na mama yao ambaye kwa wakati huo alikuwa ameshapoteza maisha.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema polisi wanamshikilia mtuhumiwa huyo katika Kituo cha Polisi cha Staki Shari, wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.
Kamanda Shilogile alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana, kwa uchunguzi na kwamba upelelezi ukikamilka mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara moja.
Waziri Kiongozi alikuwa akitokea mkoani Dodoma kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM akiwa amefuatana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar, Shawana Buheit Hassan ambaye pia ni mjumbe wa NEC.
Taarifa zilizopatikana zimeeleza kwamba ndege hiyo iliondoka juzi saa 12:00 jioni mjini Dodoma na ilitarajia kutua saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege Zanzibar.
Hata hivyo, kutokana na uwanja huo kuwa gizani, ndege hiyo ilizunguka mara kadhaa katika anga ya Zanzibar na baadaye kwenda kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mamlaka ya Usalama wa Usafiri wa Anga Zanzibar, Said Sumri, alithibitisha kuwa ndege hiyo ilishindwa kutua Zanzibar ikiwa na wajumbe wa NEC.
Hata hivyo, Sumari hakutaka kuingia kwa undani zaidi juu ya suala hilo kwa madai kwamba si msemaji.
Lakini vyanzo vya habari katika tukio hilo vilieleza kwamba ndege hiyo ililazimika kuzunguka katika anga ya Zanzibar na baadaye kurejea Dar es Salaam na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
“Tulilazimika kulala Dar es Salaam baada ya ndege yetu kushindwa kutua kutokana na tatizo la giza kufuatia jenereta ya uwanja kuharibika,” chanzo kimoja cha habari kilikaririwa kikisema.
Hata hivyo, abiria wote waliokuwemo katika ndege hiyo baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, walilazimika kujihudumia gharama za hoteli na kulazimika kusafiri Zanzibar siku iliyofuata na kuwasili Zanzibar saa 4:00 asubuhi jana.
Baadhi ya viongozi waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ni wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin (Magomeni), Ali Suleiman Ali (Kwahani), Thuwaiba Kisasi (Viti Maalum), Zainab Shomari (NEC), Issa Ahmed Othman (NEC) na wasaidizi kadhaa wa Waziri Kiongozi.
Lakini Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar, Malik Mohammed Hanif, alisema ndege hiyo ilishindwa kutua Zanzibar kwa vile uwanja wa ndege upo katika matengenezo.
Alisema tangu kuanza matengenezo katika uwanja huo, umekuwa ukifungwa kuanzia saa 1:00 usiku ili kuweka mazingira ya utulivu wakati mafundi wakitekeleza majukumu yao.
“Ndege ilishindwa kutua kutokana na matengenezo yanayoendelea katika uwanja huo na sio kweli kama jenereta liliharibika ghafla," alisema Mkurugenzi huyo.
Zanzibar haina huduma za umeme tangu Desemba 10, mwaka jana na kuathiri sekta za kiuchumi na kijamii, baada ya waya unaopokea umeme kutoka Tanzania Bara kulipuka katika kituo cha Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Kutokana na tatizo hilo, taasisi mbalimbali zimekuwa zikitumia umeme wa dharura wa majenereta, ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar ambao hivi sasa upo katika matengenezo makubwa yanayofanywa na Kampuni ya Sogea Satom ya nchini Ufaransa.
Uwanja huo wa ndege unatarajiwa kuongezwa urefu kutoka mita 2,662 hadi 3,022 na mradi huo unatarajiwa kukamilika Agosti, mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk Joyce Ndalichako (pichani) amepasha, mwaka 2009 ufauli kwa watahiniwa wa shule ni asilimia 72.51 ya watahiniwa 248,336 ikiwa imeshuka kwa tofauti ya asilimia 11.18 ukilinganisha na mwaka 2008 ambayo ilikuwa asilimia 83.69 na wale wa kujitengemea ni asilimia 54.12 ya watahiniwa 91,589 ikiwa imeshuka kwa asilimia 4.89 ya asilimia 59.01 ya mwaka 2008.
Kati ya watahiniwa 173, 323 waliofaulu, wasichana ni 74,696 (asilimia 67.59) na wavulana ni 98,627 kwa upande wa shule wakati kwa watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni wasichana 25,044 na wavulana 24,433.
Dk. Ndalichako ametaja orodha ya wanafunzi wanafunzi bora 2009, ikiongozwa na msichana Imaculate Mosha wa Marian Girls akifuatwa na Gwamaka Njobelo wa Mzumbe.
Namba 3- Wolfgang Seiya wa Majengo ya Kilimanjaro 4- ni Vanessa Chilunda, 5 ni Faith Assenga na 6 ni Doreen Philbert wote wa Marian Girls 7 ni Zahra Meghji wa Usagara na 8 ni John Kimbari wa St. James Seminali, 9 ni Said Abdallh na10 ni Evans Lwanga wote wa Feza Boys.
Dk. Ndalichako alizitaja shule kumi bora zenye watahiniwa zaidi ya 35 ikiongozwa na Marian Girls ya Pwani ambayo mwaka 2008 ilikuwa ya pili na inafuatiwa na St. James Seminary ya Kilimanjaro, Don Bosco seminary ya Iringa ambayo mwaka 2008 ilikuwa nafasi ya nane imepanda hadi nafasi ya tatu.
Alisema sekondari ya wasichana ya St. Francis ya Mbeya ambayo mwaka 2008 ilishika nafasi ya kwanza imeshika nafasi ya nne na kufuatiwa na St. Mar’y Junior Seminary ya Pwani iliyonafasi ya tano huku Uru Seminary ya Kilimanjalo imeshuka nafasi tatu na kushika nafasi ya sita wakati sekondari ya wanaume ya Feza imepanda nafasi moja hadi nafasi ya saba.
Dk. Ndalichako alisema shule zilizoshika nafasi ya nane tisa na 10 ni Anwarite Girls, Maua Seminary na St Mary Goreti zote za Kilimanjalo.
Kwa upande wa shule zenye watahiniwa chini ya 35, Dk Ndaliachoka alisema kundi hilo linaongozwa na shule ya wasichana wa Feza ya Dar es Salaam na kufuatiwa na Mafinga Seminary ya Iringa, St. Joseph-kilocha Seminari ya Kilimanjaro iliyo nafasi ya tatu na nafasi ya nne ikishikwa na Queen of Apostle-Ushirombo ya Shinyanga.
Zingine kuwa ni Dungunyi Seminari ya Singida iliyonafasi ya tano na kufuatiwa na Rubya Seminary ya Kagera, Sengerema Seminary ya Mwanza iko nafasi ya saba na kufuatiwa na sekondari ya wasichana ya Bethelsabs ya Iringa huku Thomas More Machrina ya Dar es Salaam ikishika nafasi ya tinsa na Hellen’s pia ya Dar ikiwa nafasi ya 10.
Dk Ndaliachoka alizitaja shule kumi za mwisho kwa watahiniwa 35 au zaidi kuanzia iliyoshika mkia kuwa ni Busi ya Dodoma, Milola ya Lindi, Misima ya Tanga, Kiwere ya Tabora, Potwe da ya Tanga, Masanze ya Morogoro, Mandawa ya Lindi, Msata ya Pwani, Chekelei ya Tanga na Jangalo ya Dodoma.
Alizitaja shule kumi za mwisho zenye watahiniwa chini ya 35 kuwa ni Kizara ya Tanga, Mungumbi ya Lindi, Songolo ya Dodoma, Nakuhukahuka na Marambo za Lindi, Dole ya Zanzibar, Ruponda na Mpunyule za Lindi, Ruvuma ya Singida na Viziwi Njombe ya Iringa.
“ Hapa sina mchanganuo wa ufaulu wa somo moja moja, ila somo la Civis watahaniwa wamefaulu sana wakati hisabati imeendelea kuwapiga chenga.”
Hata hivyo, Dk. Ndalichako alisema baraza hilo limesitisha matokeo ya watahiniwa 7, 242 ambao hawajalipa ada ya mtihani na wamepewa muda wa miaka mwili kulipa na kinyume cha hapo matokeo hayo yatafutwa.
“ Pia tumesitisha matokeo ya watahiniwa wawili wa kujitegemea kutokana na kuwa na sifa zao kufanana, nah ii tumeigundua dakika za mwisho, majibu yao yatatole hadi hapo watakapoleta uthibitisho. Haiwezekani kufanana majina, wamezaliwa mwaka mmoja na sifa zo za kidato cha pili zinafanana na tumeshawaandikia matokeo.”
Dk. Ndalichako alisema kuwa na hata wanafunzi wawili wakafanana kila kitu, ikiwa ni majina, tarehe na umri wa kuzaliwa,” alisema.
Baraza hilo pia limefuta matokeo ya watahiniwa 405 na watano wa mtihani maarifa(QT).
“ Baraza limegundua udanganyifu wa watahiniwa kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripiti ya somo moja na hili tumeshirikiana na taasisi ya kubaini miandiko.
“ Pia kunawale ambao wamekamatwa na ‘notes, na wale waliokutwa chooni wakisoma, waliokutwa na simu kwenye chumba cha mtihani. Lakini wapo ambao walibainika na mfano usio wa kawaida wa majawabu, kwa mfano kuna wengi wamefanana kila kitu labda badala ya kuandika ‘themselves’ wanaandika ‘them selves’.”
Dk. Ndalichako aliongeza kuwa: “ Pia kunawengi ambao swali la kemia ambao lilitakiwa kueleza jinsi ya kutenganisha kerosene na water wao wajibu jinsi ya kutenganisha alcohol na water, lakini kulikuwa na udanganyifu hatari sana wa watahiniwa kubadilisha namba za wenzao.”
Alisema kuwa watahiniwa 53 pia wamefutiwa kutokana na kutokuwa na sifa kutoka shule za Mkwese sekondari(25), Ruruma (15), Thaqalaini(6), Bishop Kisanji(5), St Vicent na Edmund Rice Sinon kila moja mmoja.
Dk Ndalichako alisema mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari ya Kadoto amefutiwa matokeo kwa kuandika matusi kwenye skripti ya somo la baiolojia ikiwa ni kinyme na kifungu cha 5(13) cha kanuni za mitihani.
Pia alisema kuwa Baraza liemevifutia usajili wa watahiniwa wa kujitegemea kwa Sinza Iteba na Dar es salaam Prime vya Dar es salaam kutokana na kuzidiwa uwezo wa kuwachukua watahiniwa wengi.
Chanzo cha habari hii www.habarileo.co.tz
Na Charles Ndagulla na
VILIO, simanzi na majonzi jana vilitawala mazishi ya Mtanzania Imran Mtui (31) aliyeuawa kikatili nchini India hivi karibuni, katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Njoro Manispaa ya Moshi.
Mwili wa marehemu huo ulizikwa bila kichwa huku pia ukidaiwa kuwa na majeraha mengi mwilini kuanzia miguuni na kwenye paja lake karibu na kiuno huku kiwiko cha mkono wa kulia nacho kikidaiwa kunyofolewa.
Mwili huo uliwasili mjini moshi usiku wa kuamkia jana baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam, ukitokea nchini India huku gharama zote za kuusafirisha zikibebwa na serikali ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kabla ya mazishi, kaka wa marehemu, Maliki Mtui, alisema kuwa wameshtushwa na kifo cha ndugu yao hasa kutokana na marehemu kutokuwa na historia ya ugomvi.
Kwa mujibu wa kaka huyo, mwili huo pia umeonekana kuwa na alama za kamba kwenye mikono yake hali ambayo inaonyesha marehemu kabla ya kuuawa alifungwa kamba ili asiweze kujitetea.
Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kutokea katika mji wa Bangalore nchini India ambako marehemu alikuwa tayari amehitimu masomo yake ya biashara na utawala (Business Administration) na tayari alikuwa akijiandaa kurejea nyumbani.
Kaka huyo wa marehemu aliwaambia waandishi wa habari kuwa mdogo wake huyo alipatwa na mkasa huo akiwa njiani kuelekea mjini ambako rafiki yake wa kike ambaye pia ni Mtanzania aishie visiwani Zanzibar alikuwa akisoma.
“Niliwasiliana naye siku ya tukio kabla hajapatwa na mauti haya nikamuuliza anatarajia kurudi lini nyumbani akanijibu angerudi mapema na rafiki yake alikuwa akimsubiri lakini hakuweza kutokea” alisema.
Pamoja na kuishukuru serikali ya Tanzania kugharamia kuusafirisha mwili wa marehemu mdogo wake, Mtui ameitaka pia serikali kuwathamini raia wake walioko nje ya nchi kwa kufuatilia taarifa zao pindi wanapokumbwa na matukio kama hayo ya kuuawa kwa mdogo wake.
Naye msemaji wa familia ya marehemu Mtui ambaye pia ni shekhe wa msikiti wa Majengo, Shekhe Said Khatibu, alisema kuwa serikali haiwathamini raia wake walioko nje na ndiyo maana serikali haijatoa tamko rasmi kulaani mauaji hayo.
Shekhe huyo pia alisema katika kile kinachoonyesha kuwa idara za serikali zimelala, serikali imeshindwa kutuma hata mwakilishi kwenye mazishi hayo ambayo tukio lake lina utata.
Aidha, alipinga taarifa zote zilizotolewa na madaktari nchini India kwamba marehemu alifariki dunia kwa ajali ya treni na kusisitiza kuwa taarifa hizo sio za kweli.
In a heart-rending incident, three members of a family committed suicide by consuming poison in Bogadi near here last night.
The deceased have been identified as Mangalamma (48), wife of Shivanna, her son Bhyrava (28) and daughter Lakshmi (22), wife of Swamy.
They allegedly ended their lives in their house behind Government School on Bogadi. Lakshmi is survived by two sons Preetham, 7, and Varun, 3. Her husband Swamy is said to be the main reason behind the trio taking the extreme step. The incident came to light when a neighbour Anitha reportedly went to the house of Mangalamma at about 6 am today.
Preetham opened the door for Anitha who found the three persons lying dead. She then informed neighbours who in turn alerted the Police.
Lakshmi, who was married to Swamy 7 years ago, was being constantly ill-treated by her husband who had turned into an alcoholic two years ago. Swamy, who owns a chicken stall in Bharathi Nagar, is said to have been assaulting Lakshmi and two children almost everyday. Attempts to reconcile the couple went in vain, according to neighbours.
Lakshmi, apparently fed up with her husband's ill-treatment, is said to have left for her parents' house along with her two children on Jan. 29.
Her father Shivanna, also said to be an alcoholic and totally non-chalant about his family affairs, was reportedly sleeping outside the house when the family members consumed poison last night.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamka leo, huko maeneo ya Kibwenzini Zanzibar wakati watu hao wakiwa wamelala ndani humo.
Ilidaiwa kuwa jenereta hilo liliripuka majira ya saa 11 za alfajiri na kuzua moto uliosababisha vifo hivyo.
Ilidaiwa kuwa familia hiyo ilinunua jenereta hilo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kutokana na kukosekana kwa umeme visiwani Zanzibar.
Katika ajali hiyo waliopoteza maisha walitajwa kuwa ni Safia Shabani, Ahmed Shaban na mtoto ambaye hakuweza kupatikana jina lake, akiwemo na msichana wa kazi Sikudhani Nasorro.
Hadi habari hii inarushwa hewani, kamanda wa Polisi wa wilaya husika hakuweza kupatikana kuongelea juu ya tukio hilo juhudi zaidi zinafanyika ili kuweza kupata maelezo yake.






.jpg)

