Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Ooh! My Dear Zanzibar.



OoH! My dear Zanzibar Island,Mungu akupe nini tena,licha ya udogo wako ila una ardhi nzuri yenye rutba,una mali asili zenye kuvutia,una wasoma mengi wa maana wa kujivunia,una vipaji vingi ,za kuringia sehemu yeyote,una sauti nzuri nyororo iso kifani ,but look at you now my dear ni nani anaekufisidi na anaevifisidi vitu vyako? qasida hizi zinanifanya nikumiss sana na nidondeshe chozi juu yako zanzibar....















































































[ Read More ]

ZIARA YA DK SHEIN KISIWANI PEMBA


ZIARA YA DK SHEIN KISIWANI PEMBA

>
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein Akiangalia karafuu zilizokatwa wakati zikisafirishwa kwa njia ya magendo.Karafuu hizo zikiwa zimehifadhiwa katika kituo cha ZSTC, huko katika Bandari ya Wete jana.(Katikati)  ni mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein, (kushoto) Naibu Meneja wa ZSTC Pemba, Hamad Khamis Hamad
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein Akisikiliza raisala ya wachumaji wa karafuu katika kambi ya daya Mtambe  jana alipofanya ziara kutembelea kambi za wachumaji wa karafuu Mtambwe wilaya ya Wete

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK A,li Mohamed Shein Akizungumza na wananchi na wakulima wa karafuu katika banda la ZSTC Daya Mtambe ambapo ni kituo kikuu cha ununuzi wa zao hilo, linalopelekea kukuza uchumi wa Nchi.
[ Read More ]

MEENA BAZAR JIONI YA LEO


Hii ndio Dada njoo ya Mysore inavyokuwa  kipindi cha  mwanzo wa Ramdhan.


































[ Read More ]

HAPPY-BIRTHDAY MY BABY BROTHER ABDUL-KADIR.

        You are the star of our family, you are the smile of my life. I wish you a very happy birthday and bless you with all my love and care. May God always take your care.I love you Brother.



















ENJOY YOUR DAY SISTER LOVE YOU SOO MUCH.



[ Read More ]

NICE VIEW IN ZANZIBAR












[ Read More ]

BIDHAA ZA FUTARI ZAPANDA ZANZIBAR




  baadhi ya wananchi wa manispaa ya mji wa Zanzibar wamelalamikia kupanda kwa bei ya mazao ya kilimo siku moja baada ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya wateja katika soko la Mwanakwerekwa wamesema bidhaa nyingi zinazotumika kwa ajili futari zimepanda bei ikilinganishwa na siku za kawaida.
Wamesema mazao yaliopanda bei ni pamoja na ndizi ya mkono mmoja inayouzwa kati ya shilingi elfu tatu na 1,500, kwa dole moja, viazi vikuu na majimbi yanauzwa kati ya shilingi elfu mbili na 5,000 kwa fungu.
Maboga yanayouzwa shilingi 1,500 hadi 4,000 kwa boga moja, na ndizi mbichi aina ya mtike inauzwa kati ya shilingi 2,000 hadi elfu nne kwa chana moja, huku nazi ikiuzwa kati ya shilingi 800 hadi elfu moja.
Miongoni mwa wateja hao Ali Kassim kutoka Fuoni, wilaya ya Magharibi ameiomba serikali kuwapunguzia ushuru wafanyabiashara wanaoingiza mazao nchini ili kupunguza bei ya mazao hayo masokoni.

Nao wafanyabishara wa mazao hayo wakizungumza na Zenji fm redio juu ya kupanda bei kwa mazao hayo wamesema mazao hayo wananua kwa bei ya juu kutokana na uzalishaji wake mashambani kuwa mdogo.
Mbali na serikali kuwataka wafanyabiashara kupunguza bei za bidhaa katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani, lakini bado kumekuwa na ongezeko kubwa la bei ya mazao hayo.
Wakati huo huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kuweka udhibiti wa bei za mazao yanayoonekana kupanda kiholela hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mfanyabishara wa soko la Chakeche Hamis Juma Hamis amesema serikali haijaweka kitengo kinachosimamia bei na kusababisha wafanyabiashara kuuza mazao hayo kwa bei ya juu.
Amesema mazao yanayonekana kupanda bei ni pamoja na ndizi za mkono mmoja, mtwike, viazi vikuu na majimbi yanauzwa kwa bei ya juu.
Nae mnunuzi wa soko hilo Fatma Ali amesema wafanyabishara wanaufanya mwezi mtukufu wa ramadhani kujinufaisha kibiashara na kuwataka kupunguza bei ili watu wenye uwezo mdogo kumudu kununua futari
Nae katibu wa afisi ya mufti Zanzibar Sheikh Fadhili Sorofa amewausia wafanyabiashara kumuogopa mwenyezi mungu kwa kutopandisha bei za bidhaa. Amesema wafanyabiashara wanadhima kubwa iwapo watanunua bidhaa kwa bei nafuu na kuziuza kwa bei ya juu
[ Read More ]

DK SHEIN AZUNGUMZA NA WATENDAJI WA WIZARA ZA AFYA, ARDHI, MAKAAZI MAJI NA NISHATI



Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzibar Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya hiyo kuhusu azma ya serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake,kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao,  kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012
  Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya hiyo kuhusu azma ya Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake,kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao,  kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya Ikulu mjini Zanzibar jana,na kujadili namna ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha mmoja ujao,hasa kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012,(kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzibar Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,maji na Nishati, Ikulu mjini Zanzibar jana,na kujadili namna ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha mmoja ujaohasa kupitia bajeti ya mwaka 2011-2012,(kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad
[ Read More ]

Mashirika ya misaada yaonya juu ya baa la njaa Pembe ya Afrika




Takriban watu milioni mbili katika maeneo ya pembe ya Afrika yaliyokumbwa na ukame wameathiriwa vibaya na baa la njaa lililokumba baadhi ya maeneo ya nchi zaKenya, Ethiopia, Djibouti na Somalia.
Wasiwasi huo wa kuongezeka kwa baa hilo unakuwa wakati ambapo kamati ya bunge la Marekani inayohusika na masuala ya kuratibu fedha za misaada ikipendekezwa kupunguziwa bajeti kwa Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani -USAID-  kwa mwaka wa fedha wa 2012 kwa kiasi cha dola za nchi hiyo milioni 488 kutika kiwango cha mwaka uliopita na dola milioni 705 pungufu ya ilivyopendekeza serikali ya Rais Barack Obama.
Mpaka sasa Marekani imetoa kiasi cha dola milioni 570 kupambana na baa la njaa katika eneo la pembe ya Afrika. Mkuu wa Utawala msaidizi wa shirika hilo la misaada la Marekani Donald Steinberg amesema iwapo bajeti yao itapunguzwa katika kutoa msaada wa chakula kutatokea madhara.
Wakati hali hiyo ya wasiwasi ikijitokeza, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani -WFP- limesema mashirika ya misaada yanashindwa kuwafikia zaidi ya Wasomali milioni mbili katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na baa la njaa kutokana na kundi la wapiganaji la Al Shabaab kuyazuia mashirika mengi ya misaada yasifike katika maeneo hayo.
Hata hivyo hali katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu imekuwa na afueni, ambapo Msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia misaada ya dharura Valerie Amos kusema kwamba idadi ya wakimbizi wa Kisomali  wanaokimbili nchini Somalia imepingua tangu wapiganaji wa Al Shabaab kujiondoa katika mji mkuu huo, mwishoni mwa wiki na kufungua njia kwa misaada zaidi kuwafikia walengwa.

Amesema watuwapatao laki moja wameyakimbia maeneo ya kati na kusini mwa nchi hiyo na kukimbilia Mogadishu. Hata hivyo ameonya kwamba hali ya usalama bado siyo nzuri.

Waziri mkuu wa Uturuki amesema ziara hiyo itakuwa ni ya kujionea wenyewe jinsi hali ilivyo katika taifa hilo lisilo na usalama duniani.Katika hatua nyingine Waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan amearifu kwamba atayatembelea maeneo yaliyokumbwa na baa la njaa nchini Somalia akiwa pamoja na familia yake katika siku zijazo. Katika ziara hiyo pia atakuwemo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki. Imekuwa nadra sana kwa viongozo duniani kuitembelea nchi hiyo kutokana na kukosa usalama.
Baa la njaa nchini Somalia limesababisha asilimia 10 ya watoto nchini humo walio na umri chini ya miaka 10 kufariki dunia kila baada ya wiki 11.
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia misaada Catherine Bragg ameelezea juu ya kina mama wanavyolazimika kuwaacha watoto wao wachanga wakifa njiani, wakati wanapotembea kwa wiki nyingi wakitafuta usalama.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na  Somalia Augustine Mahiga amesema karibu  watu milioni 3.7,nusu ya idadi ya jumla Wasomali,  wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.

habari na dw.
[ Read More ]

Life Still Has A Meaning



If there is a future there is time for mending-
Time to see your troubles coming to an ending.

Life is never hopeless however great your sorrow-
If you're looking forward to a new tomorrow.

If there is time for wishing then there is time for hoping-
When through doubt and darkness you are blindly groping.

Though the heart be heavy and hurt you may be feeling-
If there is time for praying there is time for healing.

So if through your window there is a new day breaking-
Thank God for the promise, though mind and soul be aching,

If with harvest over there is grain enough for gleaning-
There is a new tomorrow and life still has meaning.
[ Read More ]

RAMADHAN KAREEM




[ Read More ]