Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Maafa ya Mvua Comoro Katika Picha









[ Read More ]

Mungu ibariki Tanzania.

    Uongozi mtamu lakini mgumu .So sad!! i am so sure kuwa Rais kikwete yupo katika wakati mgumu sana,pale watu uliowaamini wanaposhindwa kuwa waadilifu, Mungu muongoze aweze kuivusha vyema Tanzania, sometime we need to think positive and its negative . Uadilifu ni kitu kigumu sana tofauti na watu wanavyofikiria.kazi nzuri kwa waliofanikisha kujiuzulu kwa mawaziri..ila siku zote lazima tuelewe kwamba kwenye mwema hakosekani mbaya kuna wanaotaka changes kwa seek of the country and its people, ila ndani yake pia kuna wale wanaomendea kitu flani..so kazi imekamilika tunachotegemea ni mabadiliko ya kweli,tuache uchochezi utakaopelekea kuvunjika kwa amani.watanzania waungane kuleta mabadiliko lakini ni lazima kufanya maamuzi sahihi.tusieneze or kuandika upupu tu ambao mwisho wa siku utatuwasha wenyewe..Kweli kuna freedom of speech kuna wanaosema #mawaziri wameachia ngazi @ next Raisi!..unae chochea hivi jee umejiamini??lazima tukumbuke kuwa wapiganapo fahari wawili ziumiazo ni nyasi..so kabla ya kukurupuka lazima tufikirie wananchi wa kawaida ambao kila cku ndio waathirika wakubwa..Tuungane pamoja kuleta mabadiliko katika nchii yetu.lakini lazima tuelewe mabadiliko hayo hayaji kama ndoto ukilala utaota na kushtuka lazima tujipange.same na waliowezesha kujiuzulu kwa mawaziri naamini hawakuota tu na kukurupuka tu lazima wamejipanga wamejiamini na kushirikiana.Tuendelee kuwa na sauti mojà,kudumisha Amani na utulivu iliopo katika nchi yetu.Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki watanzani.
[ Read More ]

BREAKING NEWS:

 Mawaziri nane wajiuzulu.Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda
[ Read More ]

Brigedia Adam Mwakanjuki Afariki dunia



Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki wakati wa uhai wake akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Mwakanjuki amefariki duani jana Alaasiri baada ya kuugua kwa mfupi. Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na kitu gani lakini alifikishwa hospitalini mapema wiki hii.
Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wan chi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ na mumbe wa baraza la wawakilishi kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu wamesema kwamba taarifa ya mazishi itatolewa leo baada ya kukutana wanafamilia hiyo visiwani Zanzibar.
“Ni kweli Mjomba amefariki hivi punde dare s salaam na mipango ya mazishi itapangwa baada ya kikao cha familia yetu” alisema Vicky Mwakanjuki mtoto wa Dada wa Marehemu.
Wakati wa uhai wake Marehemu Mwakanjuki alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Zanzibar katika wizara mbali mbali pamoja na kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Tangu mwaka 2007 Marehemu Mwakanjuki hakuonekana katika harakati za siasa baada ya kupata ajali mbaya akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam katika eneo la Morogoro ambayo ilisababisha kuvunjika sehemu zake za viungo.
Licha ya juhudi za kupatiwa matibabu ndani na nje ya nchi lakini hakuweza kurudi katika hali yake ya kawaida ambapo wakati wa tukio inatokezea alikuwa akiendesha gari lake mwenyewe pamoja na mwanawe.
Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo pia kuwa miongoni mwa waanzilishi wa jeshi la kujenga taifa JKT.
Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.
[ Read More ]

Rais wa Zanzibar akamilisha zuiara ya Mkoa wa Kaskazini Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, katika mkutano wa majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,(kushoto) katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee na Waziri wa Bishara,Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui.
Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na Viongozi hao katika mkutano wa  majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
[ Read More ]

Wabunge wa EALA Shy-Rose akipongezana na Nyerere

Wabunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na Shy-Rose Bhanji wakipongezana muda mfupi baada ya kuchaguliwa bungeni mjini Dodoma. 


*****


Kitendawili cha nani ataiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kimetenguliwa jana baada ya Wabunge wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwateua wagombea hao.

Bunge lilipiga kura jana kuwachagua wabunge tisa kutoka Chama tawala CCM na kambi ya Vyama vya Upinzani.

Katika uchaguzi huo CCM iliyokuwa na wagombea 24 walioshinda ni pamoja na Charles Makongoro Nyerere, , Shy-Rose Bhanji, Adam Kimbisa,  Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Bernard Murunya,Janet Mmari na Angela Kizigha
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema Bhanji alishika nafasi ya pili katika kundi la kwanza (wanawake) akipata kura 120 akitanguliwa na Angela Kizigha aliyepata kura 166. Wote ni kutoka CCM.

Wengine waliogombea katika kundi hilo ni Rose Mwalusamba wa CUF ambaye licha ya kujitoa alipata kura saba, Fancy Haji Nkuhi (57), Dk Goodbertha Kinyondo (32), Janet Mmari (119) na Janet Mbene (87).

Katika kundi la pili kutoka Zanzibar, Abdullah Ali Hassan Mwinyi alirejea tena katika bunge hilo baada ya kuongoza kwa kupata kura 227 akifuatiwa na Mariam Ussi Yahya (91).

Katika kundi hilo, Septuu Nassor Mohammed na Dk Said Gharib Billal  walishindwa kurejea katika bunge hilo baada ya kuambulia kura 74 na 88 mtawalia. Wengine walioshindwa ni Dk Ahmada Hamid Khatibu (36), Dk Haji Mwita Haji (11), Khamisi Jabir Makame (6) na Zubeir Ali Maulid (39).

Katika kundi la vyama vya upinzani, mbali ya Dk Masha wengine walioshindwa ni Anthony Komu wa Chadema (93), Juju Danda wa NCCR-Mageuzi (23), Micah Mrindoko wa TLP (66) na Mwaiseje Polisya wa NCCR-Mageuzi (42).

Katika kundi la nne la Tanzania Bara, Kimbisa ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam aliongoza kwa kupata kura 210 akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bernard Murunya aliyepata kura 135 na Makongoro kura 123.

Walioshindwa katika kundi hilo ni Dk Edmund Mndolwa (42), Elibariki Kingu (31), Dk Evans Rwaikiza (78), Mrisho Gambo (75) na Siraju Kaboyonga (38) wote kutoka CCM na John Lifa Chipaka wa Tadea (8).

 Twaha Taslima wa Cuf na Nderakindo Kessy wa NCCR-Mageuzi walichaguliwa kwa upande wa vyama vya upinzani. Taslima alipata kura 175 na Kessy kura 113.

Kabla ya uchaguzi wa jana, upinzani ulikuwa na nafasi moja katika bunge hilo ambayo ilikuwa inashikiliwa na Dk Fortunatus Masha wa UDP ambaye alianguka baada ya kupata kura 58.
[ Read More ]

Msiweke Fedha Majumbani - Dk Shein


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar hasa wakulima wa zao la karafuu kutoweka fedha zao majumbani na badala yake waweke kwenye mabenki yaliopo nchini kwa ajili ya usalama wa fedha zao.
Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kutoa zawadi ya vyeti maalum kwa wanunuzi bora wazalendo wa zao la karafuu msimu huu wa mwaka 2011-2012, hafla iliyofanyika huko katika uwanja wa Jamuhuri, Wete Pemba.

Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa ni vyema wakulima baada ya kuuza karafuu zao waweke fedha zao benki badala ya majumbani kwani inasemekana fedha nyingi walizozipata wananchi katika kuuza karafuu wameiweka majumbani.
Alisema kuwa ni jambo la busara kuweka fedha zao katika benki yoyote wanayoitaka wenyewe ikiwemo benki yao ya PBZ na hata benki nyenginezo kwa ajili ya usalama wa fedha zao na hata wao wenyewe.
Amesema kuwa bilioni 71 zimetumika katika kununua karafuu Unguja na Pemba, hali ambayo imewapelekea wananchi walio wengi kufaidika na fedha hizo kutokana na kuuza karafuu zao katika vituo vya ZSTC. Alisema kuwa sheria ya karafuu itatengenezwa upya ili iweze kukidhi haja pamoja na mazingira yaliopo hivi sasa.
Rais Dk. Shein aliwapongeza wananchi kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha zao hilo wanawauzia Shirika la ZSTC na kueleza kuwa lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ni kuwa na bajeti itakayokuwa haina tegemezi kutoka upande wowote.
Aidha, Dk. Shein alilitaka Shirika la ZSTC kuhakikisha linatafuta mbinu za kuviimarisha vituo vya kununulia karafuu kwa kuhakikisha vinatoa huduma muhimu zikiwemo vyoo, samani, maji, umeme na huduma nyenginezo.


Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwaeleza wananchi na wakulima wa zao la karafuu kuwa Serikali itafanya juhudi ya kuhakikisha kuwa barabara kadhaa hasa zile zinazoelekea katika maeneo yanayozalisha karafuu kwa wingi zinatengezwa japo kwa kiwango cha kifusi ili iwe rahisi kusafirisha zao hilo wakati wa mvua na hata wa jua.
Dk. Shein alisema kuwa serikali itaanzisha mfuko wa kuendeleza zao la karafuu na kuupitia upya utaratibu wa kuwapa fidia wananchi pamoja na kuhakikisha kwwamba mapungufu yote yaliokuwepo kabla ya kusita utaratibu huo yanafayiwa kazi.
Pia, Dk. Shein aliupongeza Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kuongeza idadi kubwa ya zao la karafuu ambalo zimenunuliwa na ZSTC mwaka huu na kufikia tani 2285 ambapo mwaka jana karafuu zilizonunuliwa katika Mkoa huo zilikuwa tani 25 tu.
Dk. Shein alimpongeza Waziri ya Biashara pamoja na watendaji wake kwa hatua iliyofikiwa ya mafanikio pamoja na kupongeza Kikosi kazi maalum, vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wenyewe ambao pia walichangia kupambana na magendo.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa mbali ya zao la karafuu pia, sekta ya utalii nayo imefanikiwa kutokana na wageni wegi kuja kutembelea Zanzibar na kusisitiza kuwa mikopo iliyokopeshwa Zanzibar uwezo wa kuilipa yote upo na Zanzibar hivi sasa inakopesheka na hakuna aliyepata hasara huku serikali ikiwa imepata fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha maendeleo nchini.
Wauzaji waliopewa vyeti hivyo maalum ni kutokana na kuuza zao hilo kwa ZSTC ni Bwana Hamad Said Hamad,Said Ali Juma, Hussein Khamis Jabu na Mohammed Issa Salim ambapo Mkoa Bora ni Mkoa wa Kusini Pemba na Wilaya Bora ni Wilaya ya Wete.
Na kwa upande wa Shehia, Shehia bora ya kwanza ni Shehia ya Selem, ikifuatiwa na Shehia ya Finya, Mtambile na Ziwani.
Wakati huo huo, Dk. Shein ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa aliweka jiwe la msingi Tawi la CCM Kinyasini na kuwataka wana CCM kujitolea kuimarisha kazi za chama ikiwa ni pamoja na kuchangia ujenzi wa Matawi.
Aidha, Dk.Shein aliwasihi wana CCM kujua kwamba Wazanzibari wote ni wamoja hivyo itikadi za vyama zisiwagombanishe jambo la muhimu ni kuelewa kuwa Serikali ni moja lakini kila mmoja anachama chake na kusisitiza kuwa katika serikali hamna upinzani na kuwataka Wana CCM kutobweteka na badala yake waendelee kukimarisha chama hicho.
Pia, aliweka jiwe la msingi katika Afisi ya la CCM Jimbo la Tumbe na kupata maelezo juu ya ujenzi wa tawi hilo ambalo aliahidi kuunga mkono kumalizia ujenzi wake ambapo katika ujenzi wa Tawi la Kinyasini, Dk. Shein aliahidi kutoa msaada wake kwa kuliezeka tawi hilo pamoja na kutia madirisha na mlango wa nyuma wa mbele na kutia rangi
[ Read More ]

Rehema Mwinyi on Newspaper.



nilijiskia furaha na bado najiskia vizuri to be one in million of students ambao nao wangependa
watokee kwenye gazeti hii.wapo watakao ona its just a simple thing but for me its Big, na anyone atakae hisi ivyo basi ujue huyo ni hater ambao hana nafasi kwenye maisha yetu.kutokana na ndoto zangu za wapi nataka niwe.so yes i did it baby. kwasababu "hata mbuyu nao ulianza kama mchicha,so who knows?may be this is the beginning? nnachoweza kusema ni kuwa usikae chini kutegema mungu akutendee miujiza kumbuka kuwa ilikua zamani enzi za mitume tu.so you have to go out there and do something remarkable.

think big,dream big.

in Allah i trust.

[ Read More ]

FC Neno la leo.



Kuna wanaokupenda na kukubali na kudhihirisha upendo wao wa dhati kwako ukiwa bado hai.Pia kuna wanaokupe na kukubali.ila wanashindwa kuzihirisha upendo wao kwako.hadi pale utakapo kufa..lakini pia kuna wanaokuchukia ila wanajifanya wanakupenda ukiwepo bado hai ila ndio maadui zako wakubwa! Binadamu tumeekewa mipaka na ni ngumu kuweza kuwajua watu wa makundi haya matatu..ila Mungu ni muona yote na yeye anajua zaidi.
[ Read More ]

FC neno la leo.

Fc neno la leo ni kipengelea kipya ambacho kitawashirikisha wadau mbali mbali wa blog hii.ukiwa na ujumbe au neno lolote nimekukaa na unataka ku share nasi pamoja na kufikisha ujumbe kwa jamii yetu. tafadhali tutumie ujumbe wako kupitia.

email:fromcoast1@hotmail.com
twitter:@fromcoast

nasi tutalieka hapa itapendeza zaidi kama utatumia jina au picha yako (lakini ni hiari sio lazima.)

ahsante adm.
[ Read More ]