Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Zuma promises half a million jobs


New South African President Jacob Zuma has promised to create half a million jobs this year in his first state of the nation address.

He said fighting poverty was his priority, a week after South Africa officially announced it was facing its worst recession in 17 years.

"We must act now to minimise the impact of this downturn on those most vulnerable," he said in Cape Town.

But he also told parliament the government had to spend wisely.

Mandela cheers

The BBC's Karen Allen in Cape Town says Mr Zuma, in power for less than a month, has had to perform a delicate balancing act to appease his unions allies, currently staging strike action, and avoid scaring off investors.


"Between now and December 2009, we plan to create about 500,000 job opportunities," he told MPs.

He promised his government would create a further four million jobs by 2014, but did not explain how.

Mr Zuma also:

• announced an annual national holiday, Mandela Day, on 18 July, prompting cheers from the audience and a wave from the watching anti-apartheid icon himself

• promised to deliver "the best World Cup ever" when South Africa hosts the football tournament in June 2010

• promised to provide anti-retroviral HIV drugs for 80% of those in need by 2011, as part of efforts to halve the rate of new HIV infections within that period

• stuck by pledges to cut violent crime by between 7%-10% a year (in a country where 50 people are killed every day)

Mr Zuma, whose African National Congress Party (ANC) swept into power in April elections on the back of strong support from unions and the poor, cautioned against expectations of a quick fix to the financial slump.

"The economic downturn will affect the pace at which our country is able to address the social and economic challenges it faces. But it will not alter the direction of our development," he said.

Ex-South African President Nelson Mandela listens to the state of the nation address by President Jacob Zuma in parliament, Cape Town, on 3 June 2009
Ninety-year-old Nobel laureate Nelson Mandela was in the audience

Fifteen years after the end of apartheid, about 40% of South Africans live in poverty - more than half of that number surviving on less than one dollar a day, according to government data.

Its economy shrunk by 6.4% during the first quarter of this year and almost one in four South Africans is unemployed.

Mr Zuma said a three-year 787bn rand ($98bn; £60bn) spending programme announced in this year's budget - and including funds for schools, transport, housing and sanitation - must be properly planned.

"In the face of the economic downturn, we will have to act prudently - no wastage, no rollovers of funds - every cent must be spent wisely and fruitfully," he said.

[ Read More ]

Kinakili safari huenda kisipatikane


Maafisa wa safari za ndege wa Ufaransa wamesema vifaa vya kunakili safari ya ndege iliyotoweka katika bahari ya Atlantic huenda visipatikane.

Maafisa hao walisema watafanya uchunguzi kwa makini mno, lakini walisema kazi yao wanaitekeleza katika mazingira ya hali ngumu mno.

Ndege hiyo, nambari AF 447, ilitoweka siku ya Jumatatu ilipokuwa safarini kutoka Rio nchini Brazil, ikielekea Paris, nchini Ufaransa, na ikiwa na abiria 228.

Mabaki ya ndege hiyo yameonekana kilomita 650 (maili 400) kutoka pwani ya Brazil, na wanamaji wa nchi hiyo wamekuwa wakifanya uchunguzi zaidi katika eneo hilo.

Maafisa wa Brazil na Ufaransa wamesema hakuna shaka mabaki yaliyopatikana ni ya ndege iliyotoweka.

Baadhi ya vitu vya kwanza kabisa kuonekana ni mafuta yaliyomwagika, kiti cha abiria na vinginevyo.

[ Read More ]

Obama aanza ziara mashariki ya kati


Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Saudi Arabia katika mwanzo wa ziara yake mashariki ya kati, inayolenga kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na nchi za Kiislamu.

Bwana Obama alitarajiwa kuwa mjini Riyadh kwa muda wa saa nne kabla ya kuelekea nchini Misri, ambako atatoa hotuba muhimu mjini Cairo.

Anasema anataka kuanzisha mdahalo na waislamu , kuondosha hali ya kutoelewana na kufufua mashauriano ya amani ya mashariki ya kati.

Hii ni ziara ya kwanza ya rais Obama katika eneo hilo, mbali na kupitia Iraq muda mfupi mwezi Aprili.

Saudi Arabia ndiyo inayodhamini mpango wa kipekee wa amani kwa uhusiano kati ya nchi za kiarabu na Israel, ingawa kwa sasa hivi mazungumzo yamekwama.

Misri inahusika sana katika matatizo ya WaPalestina , kwa kuwa msuluhishi kati ya Israel na kundi la Hamas kwenye ukanda wa Gaza.

Bwana Obama alipata mapokezi ya taadhima mjini Riyadh kabla ya kufanya mazungumzo na mfalme Abdulla.

Bwana Obama hakutarajiwa kutoa taarifa yoyote mjini Riyadh, lakini lakini siku ya Alhamisi anatarajiwa kutoa hotuba katika chuo kikuu cha Cairo nchini Misri, ambayo mwandishi wa BBC anasema ni mojawapo ya hotuba muhimu sna za rais Obama kama rais wa Marekani.

Safari ya rais Obama mashariki ya kati haijumuishi Israel, lakini muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea Saudi Arabia alikutana na waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak mjini Washington.

Akizungumza na BBC kabla ya ziara hiyo, rais Obama alisema anaamini Marekani '' itaweza kufufua tena mashauriano ya kufana'' kati ya Israel na Palestina.

Alisema ziara hiyo inakusudiwa kutoa fursa kwa Marekani na nchi za kiislamu kusikilizana zaidi.

Ziara hiyo ya mashariki ya kati imekuja huku kukiwa na taarifa zilizodaiwa kutoka kwa viongozi wa Al Qaeda, ukiwemo ujumbe ulionakiliwa kutoka kiongozi mkuu wa kundi hilo Osama Bin Laden.

Kwenye kanda hiyo iliyoonyeshwa na Televisheni ya Ki-Arabu ya al-Jazeera , Bin Laden anamlamu rais Obama na mtangulizi wake George W Bush kwa kukuza chuki dhidi ya Marekani.

[ Read More ]

Mwanajeshi Dar afa ajalini


Askari mmoja wa Jeshi la Wananchi Tanzania, JWTZ, mwenye cheo cha Kapteni, aliyetambuliwa kwa jina la Robert Makongoro, 31, amefariki dunia papo hapo baada ya gari alilokuwa anaendesha kugongwa na gari lingine katika barabara ya Sam Nujoma Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amesema ajali hiyo ilitokea jana mishale ya saa 10:30 jioni eneo la Super Star kwenye makutano ya barabara inayotokea Sinza Makaburini.

Amesema mwanajeshi huyo aligongwa na gari lenye namba za usajili T 792 ARX aina ya Suzuki, iliyokuwa ikiendeshwa na Joanes Kacheche, 41, akitokea Mwenge kuelekea maeneo ya Ubungo.

Kamanda Kalunguyeye amesema gari la Joanes lilipofika maeneo hayo, lilivaana na la mwanajeshi lenye namba za usajili T 715 AZX aina ya Toyota Carina lililokuwa likitokea Sinza Makaburini.

Amesema gari la mwanajeshi liligongwa upande wa dereva.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Lugalo.

Kamanda amesema Polisi wanamshikilia dereva Joanes kwa uchunguzi zaidi na endapo atabainika ana makosa hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa.

[ Read More ]

SMZ yaunda tume kuchunguza meli iliyozama


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuunda Tume kuchunguza chanzo cha kuzama kwa meli ya MV Fatih ikiwa na abiria na mizigo katika Bandari ya Malindi ya Zanzibar.

Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuja Zanzibar ilizama Ijumaa iliyopita baada ya kukumbwa na tatizo la kuingiza maji ikiwa katika mkondo wa bahari, hatua iliyosababisha mabaharia kutumia mashine kumwaga maji.

Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, aliiambia Nipashe kwamba tume hiyo itaangalia sura nzima ya tukio, hasa ubora wa chombo hicho pamoja na kupitia ripoti mbali mbali za ukaguzi wa meli hiyo.

Alisema iwapo kutabainika kwamba kuna uzembe ulikuwepo, hatua zitachukuliwa kwa wahusika kulingana na sheria.

Alisema kumejitokeza matapeli wanaodai wao ni waathirika wa ajali hiyo tangu serikali ilipotangaza itawasaidia watu walioaathirika.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Vuai Iddi Lila, alisema idadi ya abiria bado inaleta utata kwa vile watu waliosalimika idadi yao sasa imefikia 33 na waliokufa ni sita. Orodha ya awali ilidai kuwa abiria walikuwa 25 na mabaharia 13.

Wakati huo huo Kazi ya kuiopoa meli hiyo katika bandari ya Malindi iliendelea jana lakini hadi alasiri chombo hicho kilikuwa bado hakijaopolewa.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Bandari, Abdi Omar, alisema chombo cha kunyanyua vitu vizito maarufu kama ndovu, kiliharibika ghafla katika sehemu ya jenereta na kukwamisha zoezi hilo. Alisema mafundi walikuwa wanaendelea kutengeneza.

Awali Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Generali Davis Mwamnaynge na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema walitembelea eneo la tukio na kuwataka askari wa uokozi kuzidisha ushirikiano ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.

[ Read More ]

Kiti cha ndege chakutwa kikielea

Kiti, koti okozi, vipande vya chuma na dalili za mafuta vimeonwa katikati ya Bahari ya Atlantic na rubani wa Jeshi la Brazil ambaye ni mmoja wa wataalamu wanaoitafuta ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, Air France, iliyopotea tangu juzi. Mabaki hayo yalionekana jana kutoka angani umbali wa kilometa 650 Kaskazini mwa kisiwa cha Brazil cha Fernando de Noronha, karibu na njia ambayo ndege hiyo ilipitia kabla ya kupotea ikiwa na watu 228, msemaji wa Jeshi la Anga, Jorge Amaral alisema jana. Licha ya kuonekana mabaki hayo, bado hakukuwa na dalili zozote za uhai katika maeneo mawili tofauti yaliyokutwa na mabaki hayo yaliyoachana umbali wa kilometa 60.

"Maeneo yalikopatikana mabaki hayo ni kuelekea pale ambapo ishara ya mwisho kutoka ndege hiyo ilipoonekana kwa waongoza ndege na kisha ikashindwa kuonekana tena," Amaral alisema. "Hiyo inamaanisha kuwa ilijaribu kukata kona, pengine ikitaka irudi Fernando de Noronha, lakini hizo ni hisia tu." Amaral alisema Serikali isingeweza kuthibitisha kuwa mabaki hayo yanatokana na ndege hiyo hadi hapo itakapokuwa imeopolewa kutoka ndani ya maji na kuitambua. Meli za kivita za Brazil zinatarajiwa kufika eneo la tukio leo.

Ugunduzi huu umekuja muda wa zaidi ya saa 24 baada ya ndege hiyo kuripotiwa kutoweka na kusababisha hofu ya watu wote waliokuwamo kupoteza maisha. Waokoaji bado wanaendelea na msako katika eneo pana la bahari hiyo kuanzia Kaskazini Mashariki mwa Brazil hadi pwani ya Afrika Magharibi. Ndege hiyo aina ya Airbus A330 yenye umri wa miaka minne, ilipoteza mawasiliano Jumapili saa 4.14 usiku. Ujumbe uliotoka katika ndege hiyo muda mfupi kabla ya kutoweka, ulisema ilikuwa imepoteza msukumo wa hewa na kukabiliwa na matatizo ya umeme.
[ Read More ]

Tanzania yakubali kupokea wafungwa wa kimataifa

Tanzania iko tayari kuwachukua watu watakaopatikana na hatia ya makosa ya jinai kutumikia vifungo vyao nchini. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Jakaya Kikwete alisema hayo jana alipokutana na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Jaji Sang-Hyun Song. “Tunaweza kuchukua watakaopatikana na makosa kutumikia vifungo hapa Tanzania, tuko tayari kwa hilo,” Rais alimweleza Jaji Sang-Hyun Song.

Mahakama ya Kimataifa ingependa watuhumiwa wa mahakama hiyo kutumikia vifungo vyao katika nchi zilizo karibu na wanakotoka ili waishi katika mazingira yaliyo sawa ama kufanana na nchi wanazotoka. Jaji Sang-Hyun Song alifika nchini kujitambulisha na kuishukuru Tanzania kwa kuiunga mkono mahakama hiyo na shughuli zake katika juhudi za kutafuta haki na kulinda haki za binadamu duniani. Jaji Song ameshika wadhifa huo kwa muda wa miezi miwili na nusu sasa.

“Nimekuja Tanzania kujitambulisha kwako na uongozi wako na pia kukushukuru kwa kuiunga mkono Mahakama ya Kimataifa,” Jaji Song alimweleza Rais Kikwete. Katika kikao hicho, Rais Kikwete pia alimwambia Jaji Song kuwa ICC inaweza kutumia majengo ya Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR) iliyoko Arusha.

Rais Kikwete alisema ICTR ina uwezo wa kukidhi mahitaji yote ya ICC kwa kuwa ina vyumba vya mahakama vinne, ofisi na vyumba vyote muhimu kwa mahitaji ya mahakama ikiwamo jela ya kimataifa ambayo inawashikilia watuhumiwa wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

ICTR inatarajiwa kukamilisha kazi zake mwakani. “ICTR ina majengo na vifaa vya kimataifa, Afrika inataka pia kuwa na utambulisho wake katika hili, mnaweza kuendesha baadhi ya kesi mjini Arusha na pia itakapofika kipindi kuwa mnataka kuwa na ofisi za kanda katika Afrika, mnaweza kutumia majengo haya mara Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda itakapokamilisha kazi zake,” alieleza Rais.

Jaji Song alimshukuru Rais Kikwete kwa wazo hilo alilosema ameshukuru kulipata na atalitilia maanani kwani ICC ina nia na lengo la kushirikiana vilivyo na Afrika na kwamba pamoja na kuwa na watuhumiwa wengi kutoka Afrika, pia wafanyakazi wengi wa mahakama hiyo wanatoka Afrika na wametoa mchango mkubwa katika kazi hiyo

[ Read More ]

Wanafunzi 70 Mbagala kutibiwa Muhimbili kutokana na mabomu

KARIBU wanafunzi 70 kati ya 1,000 waliobainika kuwa na matatizo mbalimbali yaliyotokana na milipuko ya mabomu iliyotokea Aprili 29 kwenye kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mbagala Kuu, watatibiwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mwananchi imeelezwa.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa watu walioathirika na milipuko hiyo, karibu wanafunzi 900 walibainika kuwa na matatizo na kutibiwa na timu ya madaktari iliyopelekwa eneo hilo baada ya kuripotiwa kuwa watoto wengi walipata matatizo ya kutoona, kutosikia vizuri na maumivu ya kichwa.

Milipuko hiyo ilisababisha vifo vya watu zaidi ya 26 na kujeruhi watu kadhaa huku ikiharibu nyumba za wakazi wengi wa maeneo yanayozunguka kambi hiyo.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi waliopewa rufaa hiyo ni wale waliobainika kuwa na matatizo ya kutosikia na kutoona vizuri.

“Wanafunzi sita wamepelekwa Muhimbili kutokana na kugundulika kuwa hawasikii vizuri kutoka na kuathirika na milipuko ya mabomu hayo na madaktari wamesema watoto wengine 20 hawataweza kuona vizuri hadi wapate matibabu zaidi na kupewa miwani,” alisema mwalimu mmoja wa Mbagala Kuu ambaye alikataa kutajwa gazetini.

Katika Shule ya Msingi Maendeleo habari zinasema kuwa wanafunzi 30 wamebainika kuwa na matatizo ya macho huku 14 wakiwa na matatizo ya kutosikia vizuri.

Kwa mujibu wa walimu hao, baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisumbuliwa na tatizo la masikio kuvuma wakati wote, kuwa na nta nzito na macho kuwasha walitibiwa shuleni hapo na kuendelea vizuri.

Baadhi ya walimu wa shule hizo waliliambia gazeti hili jana kwa nyakati tofauti kuwa tangu kutokea milipuko hiyo Aprili 29 mwaka huu, baadhi ya wanafunzi bado hawajafika shule.

Wamesema kuwa miongoni mwa wanafunzi hao ni pamoja na Majaliwa Petro (10) Mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Maendeleo ambaye tangu kutokea milipuko hiyo hajafika shule.

Hata hivyo, dada wa Petro, Siwema Petro (13) anayesoma Maendeleo alisema mdogo wake ameathirika kisaikolojia na kuwa wakati wote anataka kukimbia na mara kadhaa anaongea mwenyewe.

“Wakati milipuko inatokea Majaliwa alikuwa shuleni, lakini tunasikia katika harakati za kujiokoa aliona mtu aliyekatwa shingo na bomu, sisi tunadhani ndicho kilichomuathiri zaidi,” alisema Siwema.

Milipuko hiyo pia imefanya miguu ya mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Mbagala Kuu, Quntinea Livingston, 7, kupooza na hivyo kusaidiwa kwa kubebwa.

Margareth Gilbert, 28, mama mzazi wa Livingston alisema mwanaye aliangukiwa na ukuta akiwa katika harakati za kukimbia baada ya kusikia milipuko ya mabomu.

Katika hatua nyingine, meya wa manispaa ya Temeke, Jerome Bwanausi amesema Mbagala sasa iko shwari na anasikitishwa na baadhi ya watu kutoa kauli za uongo na kuwatisha wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya hiyo, Bwanausi alisema taarifa zinazosambaa Mbagala kwamba mabomu yatalipuka wakati wowote ni za uongo.

“Msemaji mkuu wa suala zima la mabomu ni mkuu wa mkoa na mpaka sasa hajatoa taarifa yoyote ya ulipuaji mwingine wa mabomu kwa hiyo eneo hilo ni shwari,” alisema.

Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi jana alilazimika kuiongezea muda kamati inayofanya tathimini ya mali na majengo yaliyoteketezwa kwa mabomu hadi Juni 3 mwaka huu.

Lukuvi aliliambia gazeti hili jana kuwa amelazimika kuiongezea kamati hiyo muda baada ya mwenyekiti wake kuomba muda zaidi kwa ajili ya kukamilisha kazi.

“Nilitegemea kupokea taarifa ya kamati hiyo kesho (leo), lakini mwenyekiti wa kamati Cleophace Rweye alifika ofisini kwangu na kuomba muda zaidi wa kufanya kazi hiyo,” alisema Lukuvi.

“Moja ya mambo aliyodai hajayakamilishwa ni uandaaji wa taarifa na kufikisha taarifa yao kwa mtathimini mkuu wa serikali.”

Alisema ili waathirika hao waondokane na shida ya kuishi kwenye mahema hayo, serikali inahitaji kuwalipa fidia zao mapema, hivyo taarifa ya kamati hiyo ndiyo itakayokuwa mwongozo wa malipo.

Baadhi ya wakazi wa Mbagala Kuu jana waliendelea kuilalamikia kamati hiyo kuwa haikufanya tathimini kwenye nyumba zote zilizokumbwa na maafa hayo.

Wakizungumza na Mwananchi katika ofisi za kata hiyo wakazi hao walisema nyumba zao hazijafanyiwa tathimini tangu zoezi hilo lilipoanza.

Swaum Husein, 32, mkazi wa kitongoji cha Mwanamtoti alisema: “Sijafanyiwa tathimini yoyote katika nyumba yangu mpaka leo hii tunatangaziwa kuwa kazi hiyo imefikia ukomo wake.”

Lusian Matius mkazi wa mwanamtoti alisema: “Unavyotuona hapa tumelazimika kumchukuwa mjumbe wetu aje atueleze kwa nini mpaka leo hii nyumba zetu hazijafanyiwa tathimini.”

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, mjumbe wa shina namba moja, Mohamed Likata, 48, alikiri kuwa wakazi hao hawajafanyiwa tathimini na kwamba lina nyumba 34 zinazohitaji.

[ Read More ]

CWT, HakiElimu wasaka chimbuko la kuvuja mitihani

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na asasi ya HakiElimu, wamezindua shindano la kufahamu chimbuko la kuvuja kwa mitihani ili kukusanya maoni yatakayosaidia kupata ufumbuzi wa tatizo hilo nchini. Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Idara ya Upatikanaji wa Habari wa HakiElimu, Robert Mihayo alisema lengo la shindano hilo ni kupata mawazo na maoni ya wananchi kujua sababu za kuvuja kwa mitihani nchini na kupata ufumbuzi na kuhimiza wananchi kuboresha elimu.

Alisema taifa linahitaji elimu iliyo bora ambayo siyo tu kufaulu mitihani, bali pamoja na kumjengea uwezo mwanafunzi wa kutumia elimu aliyoipata kutatua changamoto anazokumbana nazo katika maisha ya kila siku ambapo mfumo wa elimu nchini sasa umejikita zaidi katika kufaulu.

“Katika shindano hilo litakalowashirikisha Watanzania wote bila kujali umri wala uwezo wa kitaaluma yaani kuanzia wanafunzi hadi maprofesa, linawataka washiriki kutumia kurasa mbili au michoro kuelezea chanzo cha uvujaji wa mitihani, athari zake na nini kifanyike kutatua tatizo hilo,” alisema. Alisema mwisho wa shindano hilo ni Agosti 15, mwaka huu na washindi wawili wa kwanza watapata Sh 500,000 kila mmoja, washindi 10 wanaofuata watapata Sh 200,000 kila mmoja na washindi hao na wengine 50 watakaofuata watapatiwa redio moja kila mmoja zinazotumia umeme wa jua.

Alisema mawazo ya washiriki yatachambuliwa na kutengeneza kitabu kitakachosambazwa nchini ili maoni hayo yawafikie wananchi wengi na kupelekwa serikalini ili watendaji wayafanyie kazi kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. Akizindua shindano hilo, Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema ingawa serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwamo za kuwafukuza kazi wakuu wa shule zilizohusika, kuwafutia matokeo ya mitihani wanafunzi waliobainika kuiba, lakini uvujaji na wizi umeendelea kutokea mwaka hadi mwaka.


[ Read More ]

Barcelona mabingwa wa ulaya 2009, yaichapa Man United 2-0


MABAO ya Samuel Eto'o,dakika ya 10 ya kipindi cha kwanza na Lionel Messi, dakika ya 70 yameipa ubingwa wa tatu wa Ulaya Barcelona na kuivua ubingwa huo Manchester United.

Mpira wa kwanza wa Barca, uliomaliza utawala wa dakika 10 za kwanza za mchezo huo lilifungua mlango kwa mabingwa hao wa Hispania kuonyesha dhamira ya ushindi.

Eto'o, alibashiriwa mapema na mkongwe Rui Costa wa Ureno kuwa ndiye angeweza kuipatia timu yake bao la dakika za nyongeza na kuwaduwaza Man United.

Mshambuliaji huyo wa Cameroon aliweza kutimiza ubashiri huo, kwa kuipa Barca bao muhimu ambalo hatimaye lilireejeshea jeuri timu yake na kuanza kutawala sehemu kubwa ya mchezo kipindi cha kwanza.

Mchezo ulianza kwa timu hizo kuonyesha makali, ingawa ilikuwa Man United ambayo ilikuwa na uchu kwa kulishambulia lango la Barca na kupata mikwaju kadhaa ya adhabu ndogo ambayo 'mtaalam' wake, Cristiano Ronaldo alishindwa kuitumia.

Katika mchezo huo, mwamuzi Massimo Busacca, ambaye kabla ya mchezo alikwenda Vatican, makao ya Kanisa Katoliki, kuomba baraka kwa Papa Benedict XVI akimwonyesha kadi ya njano Gerrard Pique kwa kumchezea vibaya Ronaldo.

Nao Ronaldo na Paul Scholes walionyeshwa kadi za njano kwa mchezo mbaya dhidi ya wapinzani wao.

Mabadiliko ya kipindi cha pili ya kocha Alex Ferguson kuwatoa Ji- Sung Park na Anderson na kuwaingiza Carlos Tevez na Scholes hayakusaidia.

Vikosi:

Barcelona - Victor Valdes, Carles Puyol, Gerrard Pique, YayaToure, Sylvinho, Xavi Hernandez , Sergio Busquets, Andres Iniesta, Lionel Messi, Samuel Eto'o, Thierry Henry.

Manchester United: Edwin Van der Sar, John O'Shea, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Patrice Evra; Anderson, Michael Carrick, Ryan Giggs, Ji- Sung Park, Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney.

[ Read More ]