Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Kidongochekundu Dispensary Yafungiwa

BODI ya Ushauri wa hospitali Binafsi imeifungia hospitali moja na kutoa onyo kwa hospitali nne kutokana matatizo ya mbali mbali ikiwemo ukosefu wa wafanyakazi wa kutosha pamoja na mazingira yasiyo salama ya utoji huduma za afya.

Msaidizi Mrajis wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi, Dk. Shaaban Seif Mohammed aliitaja hospitali iliyofungiwa ni Kidongoochekundu Dispensary na zilizopewa onyo kali ni Hassan Clinic, SDA Dispensary, Jang’ombe Dispensary pamoja na Kwamchina Dispensary.


Alitaja miongoni mwa makosa yaliyobainika ni pamoja na kutowasilisha vielelezo vya wafanyakazi wao pamoja na uchafu wa takataka za mabomba ya sindano ambayo yametumika kwa muda mrefu bila kutupwa sehemu husika.

Akizungumzia kwa hospitali iliyofungwa na pamoja na kukuta mfanyakzi mmoja anaefanya kazi zote za kiuguzi pamoja na kidaktari jambo ambalo linaweza kuhatarisha zaidi utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

Alifahamisha pia kuwa hospitali ya kwa Mchina na DSA Dispensary Jang’ombe ndio zilizobainika kuwa na kasoro nyingi ikiwemo uchakavu wa majengo hasa kuta za ndani pamoja na sehemu ya kufungia vidonda kuwa sakafu yake imechimbika jambo ambalo linaweza kupelekea maambukizi ya maradhi zaidi kwa wagonjwa.

Alisema Bodi hiyo imetoa muda wa mwezi mmoja kwa wamiliki wa hospitali hizo kurekebisha kasoro hizo kwa lengo la kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Alisema vitendo vinavyofanywa na baadhi ya hospitali Binafsi si vizuri na vinaenda kinyume na maadili ya utoji wa huduma za Afya hali inayoweza kurudisha nyuma maendeleo ya serikali katika kuimarisha huduma za afya kwa jamii.

Ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa waangalifu wanapokwenda hospitali hizo kuwa na kuacha mara moja kutumia hospitali ambazo zina kasoro za utoaji huduma za afya.

Alifahamisha bodi inazifanyia ukaguzi wa mara kwa mara hospitali hizo ili kuhakikisha zinafanya marekebisho ya kasoro walizonazo na iwapo watakaidi bodi haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuzifungia moja kwa moja.

Alisema serikali imekuwa ikichukua juhudi kadhaa katika kuhakikisha hospitali binafsi zinatoa huduma zenye ubora kwa wananchi kwani zinasaidia sana katika kupunguza misongamano kwenye hospitali za serikali.
[ Read More ]

Mawakili Wataka Kesi ya Mv Spice Kupelekwa Mahakama Kuu Malumbano ya sheria yatawala mahakamani

UPANDE wa utetezi unaoisimamia kesi ya washitakiwa wa kuzama kwa meli ya Mv. Spice Islanders, imemshauri Kaimu Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar, Essaya Kayange, kuihamishia kesi hiyo Mahakama Kuu ili maamuzi ya kisheria yaweze kupatikana.

Upande huo wa utetezi ulidai kuwa, katika kesi hiyo kuna baadhi ya mambo ya msingi ambayo mahakama hiyo haina uwezo wa kuyatoa kwa mujibu wa sheria, badala yake lazima yatolewe na Mahakama Kuu.

Hayo yameelezwa na wakili wa kujitegemea Masumbuko Lamwai, mbele ya Kaimu Mrajis huyo wakati kesi hiyo inayowakabili watuhumiwa 11 akiwemo Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub, kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.


Watuhumiwa hao ni Said Abdallah Kinyanyite, Abdallah Mohammed Ali, Yussuf Suleiman Issa (Kassu), Simai Nyange Simai, Haji Vuai Ussi, Abdallah Mohammed Abdallah, Juma Seif Juma, Hassan Mussa Mwinyi, Salim Said Mohammed Battashy, Mohammed Hasnuu Makame pamoja na Jaku Hashim Ayoub.

Lamwai alisema kuwa, kuna mambo mengi yanahitajika kuzungumzwa katika kesi hiyo, lakini inashindikana kutokana na uwezo ulionao mahakama hiyo ambayo haitaweza kuyatolea maamuzi.

Alisema kuwa, kwa mujibu wa sheria kesi hiyo ilikuwa ifikishwe Mahakama Kuu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza na sio Mrajis wa mahakama, na kama suala ni mahakama tu basi ilikuwa isikilizwe na mahakama ya mkoa.

Kwa upande mwengine akiungana na hoja za wakili Hamid Mbwezelani juu ya suala zima la kutokamilika kwa upelelezi wa kesi hiyo wakili Lamwai alisema kuwa hoja hizo hazina msingi mahakamani hapo.

Alidai kuwa Tume ya Uchunguzi iliyofanya uchunguzi wake ilikuwa na Jaji wa Mahakama Kuu pamoja na Mwendesha Mashitaka wa serikali, ambao wao ndio wanaowashuku watuhumiwa wa kesi hiyo, lakini Mwendesha Mashitaka huyo huyo anadai kuwa upelelezi wake bado haujamilika.

“Mheshimiwa kesi hii haikuletwa mahakamani kwa misingi ya kisiasa ya kuwapoza wananchi waliofikwa na maafa, bali imekuja kwa misingi ya kisheria, na kama ipo kwa misingi ya kisiasa basi haipaswi kuwepo hapa”, alisema Lamwai.

Alisema kuwa, kimsingi upelelezi wake tayari umeshafanywa na Tume hiyo, na pendekezo lake linaheshimika kwa ushahidi wao na hakuna wa chini yake akatoa hoja zake za kupingana na hizo.

Alisema kuwa, suala hilo la kutokamilika kwa upelelezi ni sawa na kuwatia hatiani watuhumiwa hao kabla ya kutiwa hatiani na mahakama.

Mapema wakili Hamid Mbwezeleni aliiambia mahakama hiyo kwa kudai kuwa wanashindwa kuelewa ni uchunguzi gani unaofanywa juu ya kesi hiyo wakati ripoti yake tayari imeshatolewa.

“Sizushi kama uchunguzi umefanywa na ripoti yake kutolewa na miongoni mwa wachunguzi ni Jaji Mkuu na kuamua watuhumiwa wafikishwe mahakamani, kwani hawakuwa na shaka kwa tuhuma walizokuwa nazo ndiyo maana wakaamua kuwaleta mahakamani”, alisema wakili Mbwezeleni.

Hivyo alisema kuwa suala la kutokamilika kwa upelelezi halina mashiko, na kuiomba mahakama hiyo ilikatae ombi lao hilo na kama kuna ulazima wa kukubaliwa, basi watuhumiwa hao waondolewe udhia wa kwenda na kurudi mahakamani, hadi watakapokamilisha upelelezi wao.

Akijibu hoja hizo, Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo Mohammed Khamis, Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya DPP, alisema kuwa suala la uchunguzi uliofanywa na Tume hauhusiani kabisa na upelelezi wa upande wa mashitaka.

Alifahamisha kuwa, Tume iliyoundwa kutafuta chanzo cha ajali imetoa mapendekezo mengi ya kisheria na ya kiutendaji na si lazima yafuatwe, na kwa msingi huo mapendekezo yote hayo jukumu la kuamua nani ashitakiwe na nani asishitakiwe lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.

Aidha alisema kuwa, ijapokuwa Mwendesha Mashitaka wa serikali alikuwemo katika Tume hiyo, lakini uwepo wake huo hauhusiani kabisa na utendaji wake huo bali alikuwa ni Katibu wa Tume hiyo.

“Tume imetoa maoni yake na Ofisi imetimiza wajibu wake, sisi tunajenga upelelezi ambao utaishawishi mahakama na si kufuata maoni ya Tume ni vitu viwili tofauti visivyoingiliana kiutendaji, na mahakama inafahamu hilo”, alisema Mwanasheria huyo wa serikali.

Baada ya hoja za pande mbili hizo, hakimu Essaya Kayange ambaye pia ni hakimu wa mahakama ya mkoa Vuga aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 7 mwaka huu kwa maamuzi.
Mbali ya mawakili hao upande wa utetezi pia ulikuwa ukisimamiwa na wakili Abdallah Juma pamoja na Kepteni Bendera.

Katika kesi hiyo, watuhumiwa wote hao wanakabiliwa na mashitaka ya uzembe na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hali iliyosababisha kuzama kwa meli ya Mv. Spice Islanders na kuua watu 203, Septemba 10 mwaka jana.
[ Read More ]

Baridi kali yaua zaidi ya watu 160 Ulaya



 

Baridi iliyoleta kizaazaa barani Ulaya imekwishaua watu 164, huku watu wanaoishi katika nchi za Ukraine na Italia wakiwa katika shida kubwa ya kukabiliana na viwango vya baridi ambavyo vimevunja rekodi barani Ulaya.

 
Vijiji vyote vilivyopo katika eneo la mashariki ya Ulaya vilipoteza mawasiliano hapo jana kutokana na baridi kali na theluji, huku maelfu ya wakaazi wake wakishindwa kutoka nje ya nyumba zao.

Hali ya hewa hiyo ambayo haijashuhudiwa kwa miongo kadhaa sasa barani Ulaya, ilisababisha pia barabara kutopitika, usafiri wa ndege na reli kushindwa kufanya kazi na matumizi ya gesi kupanda ghafla katika eneo hilo.
Na wakati watabiri wa hali ya hewa wakionya kutokea kwa baridi kali zaidi siku za usoni, maelfu ya watu nchini Ukraine wanatafuta hifadhi ili kuepukana na theluji hiyo iliyokwishaua jumla ya watu 101, mpaka kufikia leo asubuhi.
Mmoja wa watu wasio na makazi nchini Ukraine katika baridi kali.Mmoja wa watu wasio na makazi nchini Ukraine katika baridi kali.Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya kutoka mjini Kiev, takriban watu 1,600 wameomba uangalizi wa kitabibu baada ya kupatwa na homa kali inayoathiri mfumo wa upumuaji na wengine kupata ganzi miguuni kutokana na baridi hiyo kali iliyofikia kiwango cha nyuzi za celisiasi 35 chini ya sifuri.
Na huko mjini Warsaw, Poland watu tisa wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya kemikali aina ya zebaki kushuka mpaka kufikia nyuzi za selisiasi 32 chini ya sifuri ambayo ni sawa na nyuzi joto za Fahrenheit 25.6 chini ya sifuri.
Idadi hiyo mpya inaongeza vifo vilivyosababishwa na baridi nchini Poland kufikia watu 29, tangu juma lililopita.
Na mjini London, Uingereza Ofisi inayoshughulikia utabiri wa hali ya hewa imetangaza hali hiyo kuendelea katika maeneo mengi zaidi na theluji itaendelea kuanguka kwa kiwango kikubwa zaidi mjini Kiev, hii leo.
Aidha, Utabiri wa hali ya hewa unaonesha mji wa Berlin hapa Ujerumani utapatwa na theluji kali na baridi itafikia nyuzi joto za selisiasi kumi chini ya sifuri.
Na hofu zaidi inapanda kwa watu wasiokuwa na makazi hasa wale wanaoishi mitaani na kulala barabarani. Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na jumuiya zake ziko katika harakati za kuwatafutia ufumbuzi watu hao.
Mwakilishi wa shirikisho hilo Zlatko Kovac, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa kuwa watu hao wasio na makazi wamejikuta taabani na bila tahadhari yoyote na wako katika hali mbaya kwa sasa.
Nchi zilizoathirika na baridi hilo ni pamoja na Italia, Poland, Ukraine, Bulgaria, Romania, Ujerumani, Uingereza na Urusi.

[ Read More ]

TUMUOMBEENI VENGU JAMANI





   Watanzania  tumuombeeni Vengu  apone haraka he is still in coma.so sad jamani.tumuombee sana.
[ Read More ]

A TITANIC LIKE SCENE AS A COSTA CONCORDIA CRUISE SHIP SINKS OFF THE ITALIAN COAST...!!!



  •  The luxury cruiser was carrying 4200 people when it capsized off the cost of Italy
  • Three confirmed dead,  at least 50 still missing
  • Passengers Evacuated To Nearby Island
  • Power Failure Could Be Responsible, Says Sea Industry Expert
Tragedy: A terrified passenger said it was 'like a scene from the Titanic' as the ship began to sink and people were ordered into lifeboats and airlifted to safety
---
A ship has run aground off the Italian coast. Three people have been confirmed dead. The AFP news agency is reporting that 70 passengers are still missing as divers search the stricken vessel.
 

An evacuation operation involving five helicopters, from the coast guard, navy and air force, as well as boats and divers was launched after the luxury liner began to take on water. More than 4,000 people were rescued, though the search continues. Those pulled from the water are being sheltered in hotels, schools and churches on the island.
 
A passenger took this photo of a group of passengers in life-jackets on board the liner as they waited to be rescued
----
"An incident occurred near the island Isola del Giglio of the coast of Italy. The evacuation started promptly, but the position of the ship has worsened, making it more complicated to complete the last part of the evacuation. At this moment, the cause of the incident cannot yet be confirmed."
Reports suggest there were around 1,000 Italians on board, as well as 500 Germans, 160 French and more than 1,000 crew members. The Mediterranean cruise was en route to Savona, with further stops scheduled for Marseille, Barcelona, Palma de Mallorca, Cagliari and Palermo.
"Our first thoughts go to the victims and we would like to express our condolences and our closeness to their families and friends," said Costa.


 The Costa Concordia lies partly submerged this morning after hitting rocks. So passengers were rescued by helicopter




[ Read More ]

Breaking news:

   Kamati kuu ya CCM iliyofanya mkutano wake leo jioni mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imempitisha Mohamed Raza kuwa mgombea wa kiti cha uwakilishi jimbo la Uzini, Unguja kwa tiketi ya chama hicho. Kamati hiyo imempitisha baada ya mchuwano mkali na kuwepo kwa njama za kumtema Raza huku wapinzani wake wakidai kuwa Raza hana elimu ya kidato cha nne, ana uraia wa nchi mbili, na kwamba, haiwezekani kuongozwa na mhindi. bila shaka Raza hivi sasa atapokea habari hizo kwa shangwe kubwa baada ya kupitishwa. uchaguzi mdogo unafanyika Feb 12 mwaka huu.
[ Read More ]

MZEE KIPARA WA KAOLE AFARIKI

Baadhi ya wasanii waliofika kumjulia hali jana ni pamoja na  Fatuma Makongoro 'Bi Mwenda' (mbele).

MSANII mkongwe wa maigizo na filamu, Mzee Fundi Said, aliyevuma katika fani…
Mzee upara akipata matibabu jana.
Muuguzi akimhudumia Mzee Kipara.
Baadhi ya wasanii waliofika kumjulia hali jana ni pamoja na  Fatuma Makongoro 'Bi Mwenda' (mbele).
MSANII mkongwe wa maigizo na filamu, Mzee Fundi Said, aliyevuma katika fani hiyo tangu akishiriki uigizaji vipindi vya Radio Tanzania hadi kundi la Kaole, amefariki leo asubuhi majira ya saa 3:30 huko Kigogo.  Hali ya msanii huyo ilianza kuwa ya utata miaka ya karibuni akisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kimwili ambapo jana hali yake ilikuwa mbaya wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika makazi yake katika nyumba inayomilikiwa na kundi la Kaole.
Mtandao huu utawaletea habari zaidi za tukio hilo pindi zitakapopatikana.

na globalpublishers 

[ Read More ]

Ajali Yaua Sita

WATU sita wamekufa papo hapo wakati gari walilokuwa wakisafiria lilipopata ajali likikwepa mbwa katika eneo la katikati ya Kijiji cha Paje na Jambiani katika Mkoa wa Kusini Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Augustino Olomy alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa dereva wa gari hilo, Said Hemed Salim pia alikufa.

Wengine waliokufa ni Abdalla Maliki Jaffari (20), Haji Hassan Pandu (20), Ayoub Andrea (20),
Abdalla Haji Hemed (20) na Ramadhan Hanaa (19).


Kwa mujibu wa Kamanda Olomy, ajali hiyo ilitokea wakati wakienda Kijiji cha Paje usiku saa
sita ambapo walikutana na mbwa na wakati wakijaribu kumkwepa, gari hilo iliserereka na kugonga ukingo wa barabara.

Pia watu wengine sita walijeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini
hapa ambapo ni Hassan Kichupa aliyekuwa amepata afueni na kuweza kuzungumza.

Olomy alisema gari hilo aina ya Toyota Noah liliharibika vibaya huku injini yake ikitoka nje pamoja na bodi ya gari hiyo kuvurugika.

“Ni ajali mbaya katika mwanzo wa mwaka wa 2012 katika Mkoa wa Kusini Unguja ambayo imesababisha vijana sita; nguvu kazi ya taifa kupoteza maisha,”alisema Olomy.
[ Read More ]

Prof LIPUMBA ACHAGULIWA MWENYEKITI WA UCHUMI DUNIA



Prof. Ibrahim Lipumba
Prof. Ibrahim Lipumba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Uchumi wa Dunia. Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF ameteuliwa nafasi hiyo kutokana na uwezo wake na elimu aliyonayo ya mambo ya Uchumi.

[ Read More ]

BEYONCE AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

Beyonce has given birth to a baby girl! is reporting that the baby girl's name is Blue Ivy Carter (or at least that is what Jay is telling his friends). Earlier in the night, it was reported that the baby's names was Ivy Blue Carter...seems like a late night switcharoo from E! News cleared up the confusion.
Beyonce gave birth on Saturday, January 7th during a scheduled C-Section at Lennox Hill Hospital.
Earlier tonight, The New York Daily News reported that Beyonce and Jay-Z had rented out an entire floor at New York's Lennox Hill Hospital on the Upper East Side.
According to Beyonce's hometown paper, The Houston Chronicle, "Beyoncé has given birth to a girl early this evening in New York, says a close source. Baby and mom are doing fine."


[ Read More ]