Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Rais wa Zanzibar akamilisha zuiara ya Mkoa wa Kaskazini Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, katika mkutano wa majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,(kushoto) katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee na Waziri wa Bishara,Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui.
Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na Viongozi hao katika mkutano wa  majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
[ Read More ]

Wabunge wa EALA Shy-Rose akipongezana na Nyerere

Wabunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na Shy-Rose Bhanji wakipongezana muda mfupi baada ya kuchaguliwa bungeni mjini Dodoma. 


*****


Kitendawili cha nani ataiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kimetenguliwa jana baada ya Wabunge wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwateua wagombea hao.

Bunge lilipiga kura jana kuwachagua wabunge tisa kutoka Chama tawala CCM na kambi ya Vyama vya Upinzani.

Katika uchaguzi huo CCM iliyokuwa na wagombea 24 walioshinda ni pamoja na Charles Makongoro Nyerere, , Shy-Rose Bhanji, Adam Kimbisa,  Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Bernard Murunya,Janet Mmari na Angela Kizigha
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema Bhanji alishika nafasi ya pili katika kundi la kwanza (wanawake) akipata kura 120 akitanguliwa na Angela Kizigha aliyepata kura 166. Wote ni kutoka CCM.

Wengine waliogombea katika kundi hilo ni Rose Mwalusamba wa CUF ambaye licha ya kujitoa alipata kura saba, Fancy Haji Nkuhi (57), Dk Goodbertha Kinyondo (32), Janet Mmari (119) na Janet Mbene (87).

Katika kundi la pili kutoka Zanzibar, Abdullah Ali Hassan Mwinyi alirejea tena katika bunge hilo baada ya kuongoza kwa kupata kura 227 akifuatiwa na Mariam Ussi Yahya (91).

Katika kundi hilo, Septuu Nassor Mohammed na Dk Said Gharib Billal  walishindwa kurejea katika bunge hilo baada ya kuambulia kura 74 na 88 mtawalia. Wengine walioshindwa ni Dk Ahmada Hamid Khatibu (36), Dk Haji Mwita Haji (11), Khamisi Jabir Makame (6) na Zubeir Ali Maulid (39).

Katika kundi la vyama vya upinzani, mbali ya Dk Masha wengine walioshindwa ni Anthony Komu wa Chadema (93), Juju Danda wa NCCR-Mageuzi (23), Micah Mrindoko wa TLP (66) na Mwaiseje Polisya wa NCCR-Mageuzi (42).

Katika kundi la nne la Tanzania Bara, Kimbisa ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam aliongoza kwa kupata kura 210 akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bernard Murunya aliyepata kura 135 na Makongoro kura 123.

Walioshindwa katika kundi hilo ni Dk Edmund Mndolwa (42), Elibariki Kingu (31), Dk Evans Rwaikiza (78), Mrisho Gambo (75) na Siraju Kaboyonga (38) wote kutoka CCM na John Lifa Chipaka wa Tadea (8).

 Twaha Taslima wa Cuf na Nderakindo Kessy wa NCCR-Mageuzi walichaguliwa kwa upande wa vyama vya upinzani. Taslima alipata kura 175 na Kessy kura 113.

Kabla ya uchaguzi wa jana, upinzani ulikuwa na nafasi moja katika bunge hilo ambayo ilikuwa inashikiliwa na Dk Fortunatus Masha wa UDP ambaye alianguka baada ya kupata kura 58.
[ Read More ]

Msiweke Fedha Majumbani - Dk Shein


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar hasa wakulima wa zao la karafuu kutoweka fedha zao majumbani na badala yake waweke kwenye mabenki yaliopo nchini kwa ajili ya usalama wa fedha zao.
Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kutoa zawadi ya vyeti maalum kwa wanunuzi bora wazalendo wa zao la karafuu msimu huu wa mwaka 2011-2012, hafla iliyofanyika huko katika uwanja wa Jamuhuri, Wete Pemba.

Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa ni vyema wakulima baada ya kuuza karafuu zao waweke fedha zao benki badala ya majumbani kwani inasemekana fedha nyingi walizozipata wananchi katika kuuza karafuu wameiweka majumbani.
Alisema kuwa ni jambo la busara kuweka fedha zao katika benki yoyote wanayoitaka wenyewe ikiwemo benki yao ya PBZ na hata benki nyenginezo kwa ajili ya usalama wa fedha zao na hata wao wenyewe.
Amesema kuwa bilioni 71 zimetumika katika kununua karafuu Unguja na Pemba, hali ambayo imewapelekea wananchi walio wengi kufaidika na fedha hizo kutokana na kuuza karafuu zao katika vituo vya ZSTC. Alisema kuwa sheria ya karafuu itatengenezwa upya ili iweze kukidhi haja pamoja na mazingira yaliopo hivi sasa.
Rais Dk. Shein aliwapongeza wananchi kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha zao hilo wanawauzia Shirika la ZSTC na kueleza kuwa lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ni kuwa na bajeti itakayokuwa haina tegemezi kutoka upande wowote.
Aidha, Dk. Shein alilitaka Shirika la ZSTC kuhakikisha linatafuta mbinu za kuviimarisha vituo vya kununulia karafuu kwa kuhakikisha vinatoa huduma muhimu zikiwemo vyoo, samani, maji, umeme na huduma nyenginezo.


Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwaeleza wananchi na wakulima wa zao la karafuu kuwa Serikali itafanya juhudi ya kuhakikisha kuwa barabara kadhaa hasa zile zinazoelekea katika maeneo yanayozalisha karafuu kwa wingi zinatengezwa japo kwa kiwango cha kifusi ili iwe rahisi kusafirisha zao hilo wakati wa mvua na hata wa jua.
Dk. Shein alisema kuwa serikali itaanzisha mfuko wa kuendeleza zao la karafuu na kuupitia upya utaratibu wa kuwapa fidia wananchi pamoja na kuhakikisha kwwamba mapungufu yote yaliokuwepo kabla ya kusita utaratibu huo yanafayiwa kazi.
Pia, Dk. Shein aliupongeza Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kuongeza idadi kubwa ya zao la karafuu ambalo zimenunuliwa na ZSTC mwaka huu na kufikia tani 2285 ambapo mwaka jana karafuu zilizonunuliwa katika Mkoa huo zilikuwa tani 25 tu.
Dk. Shein alimpongeza Waziri ya Biashara pamoja na watendaji wake kwa hatua iliyofikiwa ya mafanikio pamoja na kupongeza Kikosi kazi maalum, vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wenyewe ambao pia walichangia kupambana na magendo.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa mbali ya zao la karafuu pia, sekta ya utalii nayo imefanikiwa kutokana na wageni wegi kuja kutembelea Zanzibar na kusisitiza kuwa mikopo iliyokopeshwa Zanzibar uwezo wa kuilipa yote upo na Zanzibar hivi sasa inakopesheka na hakuna aliyepata hasara huku serikali ikiwa imepata fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha maendeleo nchini.
Wauzaji waliopewa vyeti hivyo maalum ni kutokana na kuuza zao hilo kwa ZSTC ni Bwana Hamad Said Hamad,Said Ali Juma, Hussein Khamis Jabu na Mohammed Issa Salim ambapo Mkoa Bora ni Mkoa wa Kusini Pemba na Wilaya Bora ni Wilaya ya Wete.
Na kwa upande wa Shehia, Shehia bora ya kwanza ni Shehia ya Selem, ikifuatiwa na Shehia ya Finya, Mtambile na Ziwani.
Wakati huo huo, Dk. Shein ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa aliweka jiwe la msingi Tawi la CCM Kinyasini na kuwataka wana CCM kujitolea kuimarisha kazi za chama ikiwa ni pamoja na kuchangia ujenzi wa Matawi.
Aidha, Dk.Shein aliwasihi wana CCM kujua kwamba Wazanzibari wote ni wamoja hivyo itikadi za vyama zisiwagombanishe jambo la muhimu ni kuelewa kuwa Serikali ni moja lakini kila mmoja anachama chake na kusisitiza kuwa katika serikali hamna upinzani na kuwataka Wana CCM kutobweteka na badala yake waendelee kukimarisha chama hicho.
Pia, aliweka jiwe la msingi katika Afisi ya la CCM Jimbo la Tumbe na kupata maelezo juu ya ujenzi wa tawi hilo ambalo aliahidi kuunga mkono kumalizia ujenzi wake ambapo katika ujenzi wa Tawi la Kinyasini, Dk. Shein aliahidi kutoa msaada wake kwa kuliezeka tawi hilo pamoja na kutia madirisha na mlango wa nyuma wa mbele na kutia rangi
[ Read More ]

Rehema Mwinyi on Newspaper.



nilijiskia furaha na bado najiskia vizuri to be one in million of students ambao nao wangependa
watokee kwenye gazeti hii.wapo watakao ona its just a simple thing but for me its Big, na anyone atakae hisi ivyo basi ujue huyo ni hater ambao hana nafasi kwenye maisha yetu.kutokana na ndoto zangu za wapi nataka niwe.so yes i did it baby. kwasababu "hata mbuyu nao ulianza kama mchicha,so who knows?may be this is the beginning? nnachoweza kusema ni kuwa usikae chini kutegema mungu akutendee miujiza kumbuka kuwa ilikua zamani enzi za mitume tu.so you have to go out there and do something remarkable.

think big,dream big.

in Allah i trust.

[ Read More ]

FC Neno la leo.



Kuna wanaokupenda na kukubali na kudhihirisha upendo wao wa dhati kwako ukiwa bado hai.Pia kuna wanaokupe na kukubali.ila wanashindwa kuzihirisha upendo wao kwako.hadi pale utakapo kufa..lakini pia kuna wanaokuchukia ila wanajifanya wanakupenda ukiwepo bado hai ila ndio maadui zako wakubwa! Binadamu tumeekewa mipaka na ni ngumu kuweza kuwajua watu wa makundi haya matatu..ila Mungu ni muona yote na yeye anajua zaidi.
[ Read More ]

FC neno la leo.

Fc neno la leo ni kipengelea kipya ambacho kitawashirikisha wadau mbali mbali wa blog hii.ukiwa na ujumbe au neno lolote nimekukaa na unataka ku share nasi pamoja na kufikisha ujumbe kwa jamii yetu. tafadhali tutumie ujumbe wako kupitia.

email:fromcoast1@hotmail.com
twitter:@fromcoast

nasi tutalieka hapa itapendeza zaidi kama utatumia jina au picha yako (lakini ni hiari sio lazima.)

ahsante adm.
[ Read More ]

mama Lulu afunguka rasmi

[ Read More ]

TAHADHARI YATOLEWA.


Tahadhari yatolewa juu Tishio La Tsunami Bahari Ya Hindi Baada Ya Tetemeko La Ardhi Lenye Ukubwa Wa Magnitude 8.7 Chini Ya Bahari Kuitikisa Indonesia.
 Sea levels indicate a Tsunami was been generated. It is estimated to reach the Kenyan Coastline of Mombasa at 17:06 hrs, and the Tanzanian Coastlines of Lindi at 17:07hrs, & Dar es Salaam at 17:10hrs
[ Read More ]

LULU APANDISHWA KIZIMBANI, APELEKWA SEGEREA



Msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la mauaji. 
Lulu alipandishwa kizimbani kwa usiri mkubwa akitokea Kituo cha Polisi cha Oysterbay alikokuwa akishikiliwa na kupandishwa kizimbani moja kwa moja bila kuwekwa mahabusu ya mahakama hiyo kama iwavyo kwa washitakiwa wengine wanaosubiri kusomewa kesi zao.
Baada ya kupandishwa kizambani alisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambapo alisema Mnamo Aprili 7 mwaka huu majira ya saa saba za usiku maeneo ya Sinza Vatican jijini Dar es Salaam Elizabeth Michael (18) alimuua Steven Kanumba. Katika kesi hiyo mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote isipokuwa alinyoosha kidole na kupinga umri uliotajwa kuwa ana miaka 18 na kusema umri wake ni miaka 17. Baada ya kusomewa shitaka hilo, Lulu alipelekwa gerezani Segerea na kesi yake itasikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.

source.GPL
[ Read More ]

Massive 8.9 earthquake hits Indonesia, tsunami warning issued



The US Geological Survey said Wednesday the quake was centered 20 miles beneath the ocean floor around 308 miles from the provincial capital of Banda Aceh.
Said, an official at Indonesia's Meteorology and Geophysics Agency who goes by only one name, said a tsunami warning has been issued.
Indonesia straddles a series of fault lines that makes the vast island nation prone to volcanic and seismic activity.
A giant 9.1-magnitude quake off the country on December 26, 2004, triggered a tsunami in the Indian Ocean that killed 230,000 people, nearly three quarter of them in Aceh.
Source: AP
[ Read More ]