Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Wachomana Sindano Zenye Damu Yenye Ukimwi China

-
Rehema Mwinyi.

Mashambulizi ya watu kuchomwa sindano zinazohofiwa kuwa na damu yenye virusi vya ukimwi, yamezidi kuongezeka katika jimbo lililokumbwa na vurugu za kikabila la Xinjiang lililopo magharibi mwa China. Kumekuwa na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoshambuliwa kwa kuchomwa sindano zinazohofiwa kuwa zina damu yenye virusi vya ukimwi au kemikali zenye sumu katika mji wa Urumqi uliopo kwenye jimbo la Xinjiang magharibi mwa China pamoja na kwamba serikali ya China imeweka ulinzi mkali kwenye jimbo hilo kuzuia mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo yanatokana na vurugu za kikabila kati ya kabila dogo la Uygur ambalo wengi wao ni waislamu na kabila kubwa la Han.

Wakazi wa mji huo wa kabila la Han wamekuwa wakiwalaumu watu wa kabila la Uygur kufanya mashambulizi hayo ya kuwachoma watu sindano.

Jumla ya watu 45 kutoka makabila yote mawili wameishakamatwa katika mji huo wakituhumiwa kuhusika na mashambulizi hayo ya kutumia sindano.

Polisi katika jimbo la Xinjiang walitangaza kupokea ripoti ya watu 77 kushambuliwa na kuchomwa sindano hizo katika kipindi cha kuanzia jumapili mchana mpaka jumatatu mchana.

Taarifa za awali zilisema kwamba kulikuwa na jumla ya watu 531 waliokumbwa na mashambulizi hayo ya kuchomwa sindano katika wiki chache zilizopita.

Baada ya wiki iliyopita maelfu ya watu kuandamana kwenye mji huo kutaka serikali iongeze ulinzi kukomesha mashambulizi hayo, serikali ya China iliamua kupeleka majeshi yake na polisi wengi sana katika mji huo kulinda amani.

Mashambulizi hayo yamesababisha hali tata kwenye mji huo na kutishia kutokea tena kwa vurugu kubwa za kikabila kama zilizotokea julai 5 mwaka huu ambazo zilisababisha vifo vya takribani watu 200 wengi wao wakiwa ni watu wa kabila la Han.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya China ilisema kuwa watu watakaopatikana na hatia ya kuwadhuru watu kwa kutumia sindano, watahukumiwa adhabu ya kifo.

Hofu ya sindano hizo kuwa na damu yenye virusi vya ukimwi imetokana na kwamba jimbo la Xinjiang ndilo jimbo linaloongoza kwa waathirika wa ukimwi nchini China kukiwa na jumla ya waathirika 25,000 katika jimbo hilo kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana. Idadi hiyo kubwa inasababishwa na watumiaji wengi wa madawa ya kulevya katika jimbo hilo kutumia sindano zilizotumiwa na wenzao.

source:nifahamishe

Leave a Reply