Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

HUU NI KATILI.....

-
Rehema Mwinyi.

MWANAUME mmoja Aron Tilian (40) mkazi wa Kijiji cha Itimu, Kata ya Iwindi mkoani Mbeya amekamatwa na polisi kwa madai ya kufanya unyama kwa kumnyonga mpaka kufa mwanaye mwenye umri wa miaka mitatu na kumzika kwenye shamba la nyanya kisha juu yake kupanda miche ya mmea huo.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika kijiji hicho ambapo baada ya ukatili huo inadaiwa muuaji huyo alipeleka taarifa za uongo katika Kituo cha Polisi cha Mbalizi akidai kuwa mtoto huyo alikuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

 Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya mashuhuda na askari polisi walisema kuwa, Aprili 21 mwaka huu Tilian alifika kituo cha polisi na kutoa taarifa huku akiutangazia umma kuwa mwanaye huyo alikuwa amepotea.

 Baada ya taarifa hizo wananchi wanaoishi katika kijiji hicho walitafakari na kuangalia vizuri mazingira ya upotevu wa mtoto huyo ambapo walibaini kuwa Tilian hakuwa na uhusiano mwema marehemu ambaye hakuwa mwanaye wa kumzaa.

“Huyu ndugu wakati anamuoa mkewe alimkuta akiwa na mtoto huyo, baada ya kuanza kuishi naye  akaanza kumfanyia visa mtoto  sasa limetokea hili,’’ alisema shuhuda mmoja kwa sharti la kutoandika jina gazetini.

Siku ya Ijumaa Kuu Aprili 22, mwaka huu wananchi walimkamata mtuhumiwa na kuanza kumpiga ndipo alibainisha  kuwa alikuwa amemuua mtoto huyo na kumfukia katika shamba lake la nyanya, wakaamua kupiga simu kituo cha polisi,” aliongeza.

Baadhi ya askari waliofika katika eneo la tukio waliozungumza kwa sharti la kutoandikwa gazetini kwa kuwa siyo wasemaji walisema kuwa walikuta maiti ya mtoto huyo asiye na hatia ikiwa imefukiwa kwenye shimo dogo, huku kichwa chake kikiwa chini na miguu ikiwa juu.

Kwa mujibu wa polisi mmoja mwenye cheo cha juu, mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi, hata hivyo jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi ili kulizungumzia tukio hili hazikuzaa matunda.



na global publishers

One Response so far.

  1. Anonymous says:

    jamani!jamani!wanadamu tumuogopeni mungu..dah inauma sana wengine tunahangaika mchana na usiku nitapata wapi mtoto kama wenzangu wengine mtu unanyanyasika katika ndoa unadharauliwa,kutukanwa hata kuachwa jamani!wengine kila ukiconcive mimba inatoka matatizo katika uterus wewe mwingine waua mtoto,unamuua kifo cha kinyama na mateso namna hiyo?jamani malaika wa mungu?mwanamke wa watu amezaa kwa uchungu amehangaika kwa kila jinsi kulea ujauzito tena maskini ya mungu inaonekana ni wa kipato cha chini mno!leo shetani wa miguu miwili anakuja kumuua kinyama namna gani malaika wa mungu??dah!si afadhali ungempeleka katika kituo cha watoto yatima ukamtelekeza huko..mtoto alikuwa na afya nzuri, hilo zee lilaanike na askari wamshughulikie kisawasawa final auwawe ili iwe fundisho kwa wengine nao yaani hilo zee lilaanike kabisa lol!jamani wanawake wenzangu tuangalie sana wanaume tunaoolewa nao au kuishi nao especially kama tuna watoto wa pembeni binadamu wengine wamegeuka wanyama wakali wa porini tuwe makini sana.pole sana sana mama wa marehemu mtoto..mungu akutie nguvu ingawa ni ngumu sana ki ubinadamu,lakini yote muachie mungu yeye ndiye muamuzi na mtetezi wako..mtoto apumzike kwa amani.pole sana mama!

Leave a Reply