Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Profesa Mbwete awataka vijana wachangamkie vyuo vikuu.

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Prof. Tolly Mbwete amewataka wanafunzi nchini kuendelea na elimu ya vyuo vikuu hadi mwisho ili kupunguza pengo kubwa la wasomi nchini.

Profesa Mbwete alisema Tanzania ya sasa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa wasomi kuliko wajinga na kwamba kinachotakiwa ni kwa vijana kujifunga vibwebwe katika elimu ya vyuo vikuu.

Alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika mikoa mbalimbali hapa nchini vijiji vingi havina wataalamu wasomi wa elimu mbalimbali hususan ya ufundi.

Profesa Mbwete alisema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Zoom Poltechinic College kwa niaba ya Waziri wa Mali Asili na Utalii ambapo aliwataka wanachuo hao kusoma kwa malengo ya elimu ya juu zaidi na si kutaka kuishia katika ngazi ya stashahada.

"Katika suala la elimu taifa hili bado tuko nyuma kwa sababu nchi zilizoendelea, kiwango chao cha elimu ni asilimia 40 wakati hapa ni asilimia 10,"alisema Prof. Mbwete.

Alisema utafiti umebaini shida zilizoko vijijini jinsi watu wanavyopata shida ya kupata wataalamu wa kufanya kazi, hali inayowalazimu kutumia gharama kuwatoa mijini kwenda kufanya kazi au kutengeneza kitu fulani.

Alisema jitihada za kupata wasomi wengi zitafanikiwa ikiwa watu wengi wataendelea kuwekeza katika elimu na kwamba lengo liwe kupata wasomi wa taaluma mbalimbali.

Akizungumzia chuo hicho, Profesa huyo alimpongeza Mkurugenzi wa chuo hicho, Gaudios Shija kwa mafanikio aliyoyapata kwa kipindi kifupi tangu aanzishe chuo hicho mwaka 2000.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi kutumia nafasi walizopata kusoma kwa bidii ili waweze kuendelea na vyuo vikuu vingine.


source: mwananchi.

[ Read More ]