Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mwanafunzi Mtanzania, Imran Mtui auawa India



Habari zilizopo katika blogu ya Watanzania waishio Bangalore (TASABA), pia katika mtandao wa Twitter zinathibitisha kuwa, mwanafunzi wa Kitanzania, Imran Mtui (31) aliyekuwa anasoma katika Chuo kishiriki Cha Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India, amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa hauna kichwa.
Taarifa zinasema kuwa mwili huo ulikutwa kando kando ya reli katika eneo la Shivajinagar katika mji wa Bangalore ukiwa hauna kichwa huku mguu mmoja ukiwa umejeruhiwa vibaya.Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Mimi nilipata taarifa hizo juzi jioni ambapo jana tulifanya kikao na wenzangu na kumtuma Ofisa wetu Mzee Amon Mwamanenge na mwanasheria wetu wamekwenda huko kupata undani wa tukio hilo," alisema Balozi Kijazi.

Alisema kuwa kwa sasa hawezi kutoa picha kamili lakini mwili wa kijana huyo umekutwa ukiwa hauna kichwa na mguu umebondeka. Kijana huyo aliyefariki alikuwa amemaliza Shahada ya Usimamizi wa Biashara (BBM) na alitambulika kwa jina la Imran Mtui. Aliwahi kuwa Mtunza Fedha wa Chama Cha Wanafunzi wa Kitanzania Waishio Bangalore (TASABA).

Habari hizi zimedhibitishwa na mdogo wa marehemu, Issa Mtui, kwa njia ya simu akiwa safarini kuelekea Marangu, Moshi. Alieleza kuwa mwili wa marehemu unategemewa kuwasili nchini Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya taratibu za mazishi ambayo yatafanyikia Marangu.
Imrani ni wa pili kuzaliwa kati ya watoto wanne kwenye familia hiyo. Inadaiwa kuwa kabla mauti haijamkuta alitarajiwa jana angekuwa amerejea nchini baada ya kuwa amechukua vyeti vyake vya masomo ambavyo alikuwa akivisubiri baada ya kuhitimu masomo yake.

Polisi nchini India wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.
[ Read More ]

TANGAZO..

TAARIFA KAMILI YA KAMATI YA KUFUATILIA MSIBA WA KAKA YETU IMRAN MTUI CHINI RAIS WA TASABA NA MUWAKILISHI WA UBALOZI MR.AMON MWAMANENGE ITATOLEWA BAADAE USIKU HUU.TAARIFA ITAHUSISHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA POLISI,HOSPITALI NA KAMPUNI YA RELI KUHUSU KIFO CHA KAKA YETU IMRAN MTUI.TUNAOMBA RADHI KWA KUCHELEWESHWA KWA TAARIFA KWANI TULIKUA HATUWEZI KUZUNGUMZA LOLOTE MPAKA TUPATE RIPOTI RASMI YA KAMATI HII AMBAYO IMECHELEWA KUTOKANA NA SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WAO.TUNAKUMBUSHA YA KWAMBA TUSINGEWEZA KUANDIKA TETESI TULIZO SIKIA KUHUSIANA NA MSIBA HUU KWANI ZILIKUA NI TAARIFA ZISIZO RASMI.

TASABA SPOKESMAN
JUMANNE MTAMBALIKE
[ Read More ]