Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mwili wa kichanga waokotwa jalalani

Mwili wa mtoto mchanga wa umri wa miezi miwili umeokotwa ukiwa kwenye dampo la taka pale Mwananyamala Jijini.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limejiri majira ya saa 4:00 asubuhi pale Mwananyamala Kwa Msisiri Jijini.

Akasema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, polisi walifika eneo hilo na kuukuta mwili huo ukiwa umefungwa kwenye taulo na kisha kuviringishwa na khanga juu yake.

Akasema baada ya kuhakikisha hakuna mtu aliyemuona, mwanamke aliyefanya unyama huo aliutupa mwili huo kwenye dampo hilo kabla ya kuingia mitini.

Kamanda Kalunguyeye akasema Polisi wapo katika msako mkali wa kumtafuta mwanamke huyo ili afikishwe katika vyombo vya sheria.

Katika tukio jingine, watu wawili wamekamatwa na polisi baada ya kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya.

Akasema, watu hao walikamatwa majira ya saa 1:00 asubuhi eneo la Stendi ya Mbezi wakiwa na kete nane za madawa ya kulevya.

Akawataja watu hao kuwa ni Evance Jackson. 20, na Rajabu Jumanne, 21.

Akasema, watu hao watafikishwa Mahakamani haraka baada ya kukamilika kazi ya kuwahoji kuhusiana na tukio hilo.
[ Read More ]

Mwamuziki maarufu wa taarab Nasma Hamis 'Kidogo' afariki.


FANI ya muziki wa taarabu nchini imepata pigo kubwa baada ya kumpoteza mtunzi na mwimbaji mahiri, Nasma Khamis, maarufu 'Kidogo'.

Nasma, 57, ambaye anakumbukwa kwa baadhi ya nyimbo zikiwamo, Mtu Mzima Ovyo alifariki usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam.

"Hebu tueleze una kitu gani ee cha kututambiaa, ebu tuambie una kitu gani ee cha kuturingiaa, tema mate chini nyuma hujioni ee wanakukimbia, kaona mambo yako huku taarabu imo taarabu imo kaona mambo yapo huku wee! utaumiza roho yako....wadudu wadogo wadogo wananyevua nyevua," hayo ni baadhi ya maneno katika wimbo wa 'Mtu Mzima Ovyo' ulioimbwa naye Nasma.

Kulingana na ndugu zake, Nasma alifariki saa sita usiku kwenye Hospitali ya Temeke alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na malaria.

Baba mdogo wa marehemu, Hamis Mohamed 'Kaniki' aliiambia Mwananchi nyumbani kwake, Kinondoni Hananasif, Dar es Salaam ambako kumewekwa msiba huo kuwa Nasma alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu mara kwa mara, lakini wiki iliyopita alilazimika kulazwa Temeke kutokana na hali yake kuwa mbaya na uchunguzi ulionyesha alikuwa na malaria.

" Siku nne zilizopita alilazwa Temeke lakini jana hali yake ilibadilika na saa sita usiku akafariki, Mungu ndiye anayetoa na yeye ndie anayechukua"alisema mzazi huyo.

Alisema Nasma ambaye ameacha watoto sita, wanne wa kike na wawili wa kiume atazikwa leo kwenye makaburi ya Kisutu.

Akizungumzia msiba huo, msanii mwingine mahiri ambaye alitajwa kuwa mpinzani wa Nasma, Hadija Kopa alisema, "Nimepata taarifa leo (jana), nasikia uchungu sana ni mwenzetu tulikuwa naye, Mungu amlaze mahali pema peponi." Alisema upinzani wake na Nasma ulikuwa ni wa kazi na si wa ubaya kama watu walivyodhani.

"Upinzani wetu ulikuwa ni wa kazi na si wa ubaya na kama ni ubaya kinapotokea kitu kama hiki lazima uweke tofauti pembeni ni kitu kikubwa cha kuhuzunisha, katangulia mbele za haki hatuna budi kumuombea Mungu amlaze mahali pema peponi.

Msanii huyo ambaye alikuwa akiishi Tabata Kinyerezi, Dar es Salaam atakumbukwa kutokana na nyimbo zake zenye vijembe walivyokuwa wakitupiana na mwenzake, Hadija Kopa na kuifanya fani ya taarabu kutamba miaka ya '90 kiasi cha kuitwa rusha roho.

Baadhi ya nyimbo ambaye zilimzolea sifa msanii huyo na hazitasahaulika masikioni mwa watu ni pamoja na ule wa 'Mwanamke Mazingira ', Subira Heri Mpenzi na Sanamu la Micheline.

Wakati wa uhai wake, Nasma aliimbia vikundi mbalimbali kama vile, Egyptian, Babloom, Tanzania One Theatre na Muungano Culrural Troupe. Mpaka mauti yanamkuta msanii huyo alikuwa akifanya shuguli zake binafsi.

[ Read More ]