Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Angelina Jolie akatwa matiti kuzuia Saratani


Angelina Jolie
Mcheza filamu mashuhuri sana duniani,Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.
Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.
Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.
''Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,'' alisema Jolie.
Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.

Uwezekano wapunguzwa.

Katika taarifa iliyoandikwa na Bi Jolie na yenye kichwa, 'Uamuzi wangu wa kimatibabu', Bi Jolie alieleza kuwa mamake alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka 56.
Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku moja atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.
Angelina Jolie na Brad Pitt
Uwezekano wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.
Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu kufanyiwa upasuaji.
"ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya, na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata baada ya kuondoa viungo hivyo,'' alisema Bi Jolie.
"kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi.''
Muigizaji huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.
Wakati alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.
Jolie pia alihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za kigeni wa G8, kuhamasisha dunia kuhusu dhulma za kingono katika maeneo ya vita.
[ Read More ]

Ujumbe wa Oman Wawasili Zanzibar kwa matayarisho ya Mkutano wa Kimataifa wa Historia ya Oman na Zanzibar, Historia ya Kiislam na Utamaduni wake.



Kaimu Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Saleh Suleiman, akisalimiana na Kiongozi wa Msafara wa Wajumbe wa Oman waliowasili Zanzibar leo kwa ajili ya matayarisho wa Mkutano wa Historia na Utamaduni wa Kiislam. unaotarajiwa kufanyika mwezi wa september 2013 Zanzibar. 
 BALOZI wa Oman  nchini Tanzania Yussuf Al Bakar ( katikati) akiongozana na Ujumbe kutoka Nchini Oman ukiwasili Zanzibar kwa ajili ya matayarisho ya Mkutano wa Kimataifa wa utakaozungumzia Historia na Utamaduni wa Kiislam Zanzibar kulia Kiongozi wa Ujumbe huo Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyaniy, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mamlaka ya Makumbusho ya Taifa ya Oman. Na kushoto Kaimu Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Saleh Suleiman

 Ujumbe wa Oman ukiwa katika ukumbi wa Wageni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakibadilishana mawazo baada ya kuwasili Zanzibar leo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Dkt. Haji Mwevura Haji,akizungumza katika mkutano na Ujumbe wa Oman, uliowasili Zanzibar kwa matayarisho ya mkutano wa Historia na Utamaduni wa Kiislam, kushoto Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyaniy, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mamlaka ya Makumbusho ya Taifa ya Oman,na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Historia ya Uislam Oman Dkt.Halit Eren.
 Mkuu wa Msafara wa Ujumbe wa Oman uliowasili Zanzibar kwa matayarisho wa Mkutano wa Kimataifa utakaozungumzia Historia na Utamatudi wa Kiislam, Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyaniy, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mamlaka ya Makumbusho ya Taifa ya Oman,Zanzibar ina mahusiano ya Kihistoria na Mataifa ya Kiarabu katika historia na Utamaduni wa Kiislam.kulia  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Dkt. Haji Mwevura Haji na  Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Historia ya Uislam Oman Dkt.Halit Eren,
 Mkuu wa Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Issa Haji Zidi, akitafsiri katika mkutano huo kutoka katika lugha ya Kiarabu, wakati wa mkutano huo wa matayarisho ya Mkutano wa Kimataifa wa Historia na Utamaduni wa Kiislam unaotarajiwa kufanyika Zanzibar mwezi wa September 2013.  
 Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Historia ya Uislam Oman Dkt.Halit Eren, akizungumza katika mkutano huo uliowashirikisha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA,  
 Ujumbe wa Oman wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Dkt. Haji Mwevura Haji, akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa SUZA Majestiki Zanzibar. 
Ujumbe wa SUZA wakiwa katika Mkutano na Ujumbe kutoka Oman uliofika Zanzibar kwa maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Historia ya Uislam na Utamaduni wake baina ya Nchi hizi mbili.mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mkutano Chuo Kikuu cha Taifa Kampasi ya Majestic Zanzibar. 
[ Read More ]