Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Taarifa ya Mwenyekiti wa TASAM




Assalam aleikum.


Ndugu watanzania, ikiwa ni mara ya kwanza kutoa salam zangu na shukrani za dhati kwenu ikiwa ni wiki ya 3 sasa baada uchauguzi kufanyika na kutumia haki yenu kuchagua uongozi mpya ukiongozwa na mimi kuchukua hatamu hii ya kuongoza chama chetu cha wanafunzi wa kitanzania Mysore kwa mwaka wa masomo 2010-2011.

Ndugu watanzania, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kuweza kufika hapa tukiwa katika hali ya amani na utulivu ijapokuwa juzi tarehe 18-04-2010 kulitokea kuchafuka kwa hali ya amani miongoni mwetu ila namshukuru Mwenyezi Mungu tumeweza kurudusha amani hiyo.

Ndugu watanzania, ikumbukwe ya kwamba baada ya Mwenyekiti wa TASAM aliepita Bi. Mwinga kutangaza kujiuzulu na kuvunja baraza lote la uongozi, watanzania walikusanyika na kuchagua kamati ambayo ingeshughulikia uchaguzi wote hadi kukamilika kwake na kukabidhi madaraka kwa uongozi utakaochaguliwa. Kamati ilichaguliwa na wajumbe walikuwa kama ifuatavyo:-
1. Fred Kapara, Mwenyekiti wa kamati
2. Faris Lyimo, Mjumbe
3. Abdul haji, Mjumbe,
4. Josephina, Mjumbe.

Ndugu watanzania kamati yetu iliendeleza kazi iliyoachwa na Mwenyekiti mstaafu Bi. Mwinga kutangaza uchaguzi na kugawa fomu kwa watu wenye sifa ya uongozi kama katiba ya TASAM ilivyohusisha sifa hizo. Kamati ilitangaza siki ya uchaguzi kwa watanzania wote na kutaka watanzania kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali. Bahati mbaya au nzuri ni watu wachache waliojitokeza kuchukua fomu hizo nikiwemo mimi na makamu wangu katika nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti.

Ndugu watanzania, juu ya kwamba tarehe ya uchaguzi kutangazwa ila ni watanzania wachache walijitikeza kupiga hizo bila sababu ya msingi. Hata hivyo kutokana na sheria inayohusu uchaguzi (universal laws of election) kwamba uchaguzi hautahairishwa kwa kufika wati wachache katika vituo vya kupigia kura, kwani kutofika kwa yoyote kutumia haki yake basi atakua amaipoteza haki hiyo. Hivyo uchaguzi ulifanyika na uongozi mpya wa Tasam 2010-2011 uliingia madarakani.

Ndugu watanzania viongozi waliochaguliwa ni kama ifuatavyo

Hussein Milao, Mwenyekiti
Joanmery, Makamu Mwenyekiti,
Mohammed Ali, Katibu
Fayka Salum Naibu katibu
Shemsa Khalid, Mshika Fedha.

Ndugu watanzania, kutokana mambo yanawaohusu baadhi ya makundi ya watu hapa Mysore yasipelekee kupotosha watanzania na kuharibu amani iliyopo miongoni mwetu. Napenda kutoa wasiwasi kwa watanzania uongozi wenu tayari umeshawasiliana na ubalozi wetu New Delhi pamoja na Afisi ya Kamishna wa Polisi Mysore juu ya hali iliyotokea, hivyo tunawaomba watanzania tusijihusishe na hayo mambo yanayotaka kuletwa na baadha ya vikundi vya watu kutokana tu na uhasama uliopo kati yao na ninaomba zaidi tuzidishe nguvu yetu kwenye masomo yetu kwani hayo ndiyo mambo ya msingi yaliyotuleta hapa.

Mwisho napenda kukushukuruni zaidi kwa ushirikiano mnaonionyesha kila siku zinavyoenda mbele. Nawatakia watanzania wote mitihani mema, na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutafanya vyema na kupaisha jina la nchi yetu kimasomo hapa Mysore. Amin.

Mungu ibariki Tanzania. Amin.

Ahsanteni

HUSSEIN MILAO
MWENYEKITI, TASAM.
[ Read More ]