MCHEZAJI El Rayan Abdallah wa timu ya Taifa ya Sudan (kushoto) akipambana na Sabri Ramadhani China, Mkongwe wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, wakati wa mechi
Mfungaji wa mabao mawili ya Zanzibar Heroes, Salum Shiboli akishangili bao la pili la timu yake.
Ali Shiboli aishangilia baada ya kuwatungua Wasudan
Beki wa Timu ya Taifa ya Zanzibar - Zanzibar Heroes akichuana vikali na mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Sudan Ramadhan Shareef Ferein
Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakitoka uwanjani kwa kuwasalimia washabiki wachache waliokuwepo uwanjani
Picha kwa hisani ya Michuzi na Bashir Nkoromo
Timu ya Taifa ya Zanzibar imeanza vyema mashindano ya Cecafa yanayofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kuichabanga timu ya Taifa ya Sudan kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa kundi B uliofanyika jana.
Magoli ya Zanzibar Heroes yalifungwa na mchezaji Ali Shiboli ambaye karibuni tu alimwaga wino kuichezea Simba Sports Club ya Dar.
Zanzibar inaongoza katika kundi lake linalojumuisha timu ngumu za Rwanda na Ivory coast. Rwanda pia iliweza kushinda mchezo wake wa kwanza kwa kuifunga Ivory Coast 2-1.
Zanzibar itajitupa tena uwanjani siku ya Jumatano tarehe 01/12/2010 kwa kupambana na Timu alikwa ya Ivory Coast na kumalizia na Timu ya Taifa ya Rwanda hapo tarehe 03/12/2010.
Tuzidi kuipa moyo timu yetu kupata matokeo mazuri kwani ndio njia nzuri ya kutuma ujumbe FIFA kwamba nasi pia tu wakali katika kulisakata kabumbu.