Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

PUMU HAIPATANI NA VYAKULA VYA MAFUTA

Kama tunavyosema kila siku, 

hakuna kitu kibaya kama mgonjwa kutokujua aina

 ya vyakula anavyopaswa kula na kuviepuka.

 kwa sababu bila kuwa na uelewa huo

uwezekano wa mgonjwa huyo kupata 

ahueni katika ugonjwa 

unaomsumbua, utakuwa mdogo sana.



Pumu ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua watu wengi duniani,

Tanzania ikiwemo. Ni ugonjwa ambao hauna tiba ya kuponya kabisa bali huwa 


na dawa ya kutuliza pale mgonjwa anapozidiwa.

Ili mgonjwa asisumbuliwe sana na ugonjwa huu unaoziba pumzi, tiba pekee ni kujua na kuepuka aina ya vyakula vinavyochochea, halikadhalika kujua aina ya vyakula vinavyotoa ahueni kwa mgonjwa.


Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, vyakula vyenye mafuta mengi (high fat meal), huchangia matatizo katika njia ya hewa na hivyo kumfanya mgonjwa kupumua kwa tabu, tena hali hiyo huweza kutokea muda mfupi baada ya kula vyakula hivyo.

Kwa maana nyingine, mtu mwenye ugonjwa wa pumu anapokula vyakula vyenye mafuta mengi, kama vile nyama za kukaanga, chips, n.k, hufanya tatizo lake kuwa kubwa na gumu na kujikuta akibanwa na pumu mara kwa mara.

Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na watafiti nchini Australia, vyakula vyenye mafuta mengi husababisha hata dawa ya kutuliza pumu anayotumia mgonjwa (Ventolin ) ishindwe kufanya kazi yake sawasawa.

Aidha, utafiti huo umeonesha kuwa idadi ya wagonjwa wa pumu imeongezeka sana katika nchi za ulaya kutokana na kuongozeka kwa matumizi ya vyakula vyenye mafuta na kupungua ulaji wa vyakula vya asili.



LISHE YA MGONJWA WA PUMU (ASTHMA)
Baadhi ya vyakula vinavyoaminika kutoa ahueni na kuwa kama tiba kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na asali, juisi ya limau, mchanganyiko wa vitunguu swaumu na maziwa na mchangayiko wa abdalasini pamoja na asali. Vyakula hivyo vikiwa sehemu ya mlo wa mgonjwa kila siku, atapata ahueni ya ajabu.

Pamoja na kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mgonjwa wa pumu anatakiwa pia kula kwa kiasi kidogo mlo wenye matunda, mboga za majani na vyakula vingine vitokanavyo na nafaka ambavyo hutoa ‘alikalaini’.


Aidha, wagonjwa wa pumu wanatakiwa kujiepusha na ulaji wa kiasi kikubwa cha wali, sukari, mtindi (yoghurt), unywaji mwingi wa chai, kahawa, pombe na vyakula vote vya kusindika au kwenye makopo.


Mgonjwa anashauriwa pia kufanya mazoezi ya kuvuta hewa safi na kuishi katika hali ya hewa isiyo na baridi, kunywa maji mengi mara kwa mara, kufunga kula (fasting) japo mara moja kwa wiki. Kwa kufuata masharti hayo, mgonjwa anaweza kuishi na pumu bila kusumbuliwa wala kutumia dawa kali kwa maisha yake yote.
habari hii kwa hisani ya abdalah mrisho blog.
[ Read More ]

Mtandao Wa Mobile Monday Wazinduliwa Rasmi Jijini Dar


Muanzilishi wa mtandao Mobile Monday (MoMo) unaojihusisha na maswala ya kukutanisha wataalam wa mambo ya habari na teknolojia ya mawasiliano (ICT) Duniani,Jari Tammisto akizungumza katika uzinduzi wa mtandao huo kwa hapa nchini uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia,Kijitonyama jijini Dar.
Mmoja wa waanzilishi wasimamizi wa mtandao wa Mobile Monday (MoMo) kwa hapa nchini,Kaye Billy akiweka sawa taratibu za shughuli nzima ya uzinduzi wa mtandao huo hapa nchini iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia,Kijitonyama jijini Dar.Da' Amina Lukanza wa Mobile Monday (MoMo) akionyesha utaratibu mzima wa mtandao kwa mwaka mzima kwa baadhi ya wataalam waliofika katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wataalam na wadau wa mambo ya habari na teknolojia ya mawasiliano (ICT) waliofika watika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakiendelea katika uzinduzi huo.
Wadau woote wa habari na teknolojia ya mawasiliano (ICT) waliofika katika uzinduzi wa mtandao wa Mobile Monday walipata nafasi ya kupata picha ya pamoja kabla ya kuondoka ukumbini hapo.

[ Read More ]

Dk. Bilal Aingia Mzigoni Leo


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika Ofisi yake Ikulu Dar es salaam leo ikiwa ni siku ya kwanza tangu kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakati alipotembelea katika Ofisi hiyo iliyopo katika mtaa wa Luthuli jijini Dar es salaam leo ambapo ni siku ya kwanza tangu kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
[ Read More ]