WATU sita wamekufa papo hapo wakati gari walilokuwa wakisafiria lilipopata ajali likikwepa mbwa katika eneo la katikati ya Kijiji cha Paje na Jambiani katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Augustino Olomy alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa dereva wa gari hilo, Said Hemed Salim pia alikufa.
Wengine waliokufa ni Abdalla Maliki Jaffari (20), Haji Hassan Pandu (20), Ayoub Andrea (20),
Abdalla Haji Hemed (20) na Ramadhan Hanaa (19).
Kwa mujibu wa Kamanda Olomy, ajali hiyo ilitokea wakati wakienda Kijiji cha Paje usiku saa
sita ambapo walikutana na mbwa na wakati wakijaribu kumkwepa, gari hilo iliserereka na kugonga ukingo wa barabara.
Pia watu wengine sita walijeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini
hapa ambapo ni Hassan Kichupa aliyekuwa amepata afueni na kuweza kuzungumza.
Olomy alisema gari hilo aina ya Toyota Noah liliharibika vibaya huku injini yake ikitoka nje pamoja na bodi ya gari hiyo kuvurugika.
“Ni ajali mbaya katika mwanzo wa mwaka wa 2012 katika Mkoa wa Kusini Unguja ambayo imesababisha vijana sita; nguvu kazi ya taifa kupoteza maisha,”alisema Olomy.
[ Read More ]