HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE TOKA ZENJI ZIKISEMA KWAMBA MSANII MAARUFU WA HUKO VISIWANI YUSUF AHMED ALLEY MAARUFU KAMA BWAN'CHUCHU HATUNAYE TENA. HABARI HIZO ZINASEMA BWAN'CHUCHU AMEFIA JIJINI NAIROBI, KENYA, ALIKOKUWA AMEKWENDA KIKAZI. CHANZO CHA MAUTI YAKE HATUJAAMBIWA ILA IMETHIBITISHWA KWAMBA MWILI WAKE UMESHAREJESHWA ZENJI NA MSIBA UKO KWAO SEHEMU ZA KISIMA MAJONGOO NA MAZIKO YATAFANYIKA LEO SAA 10 KWENYE MAKABURI YA MWANAKWEREKWE.
BWAN'CHUCHU ATAKUMBUKWA KWA UHODARI WAKE KATIKA MUZIKI HASA ALIPOUNDA BENDI YA CHUCHU SOUND ILIYOTAMBA SANA KWA VIBAO VYAKE VIKALI NA CHAPUO ZA MAONGEZI KATI YAKE NA OMARI MKALI YALIYOKUWA YAKIHITIMISHWA NA NENO LA 'EE! KWAHERI'.
MAREHEMU CHUCHU PIA ALIKUWA MMOJA WA WAJUMBE WA BODI YA TAMASHA LA KILA MWAKA LA SAUTI ZA BUSARA NA PIA ALIKUWA ANAMILIKI STUDIO YA KUREKODIA MUZIKI PAMOJA NA STESHENI YA REDIO.
MOLA AIWEKE MAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU
-AMIN