Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

MAANDAMANO YA KUADHIMISHA MWAKA MPYA WA KIISLAM


KATIBU wa Ofisi ya Mufti Zanzibar Shekh Fadhil Soraga akitowa
 hadithi ya Mwaka wa Kiislam kwa Waumuni wa
 Dini ya Kiislamu waliohudhuria sherehe za
kuukaribisha mwaka wa Kiislam zilizofanyika
 kiwanja cha Kisonge, Michezani.

BAADHI ya Waislamu waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya
 Mwaka wa Kiislam wakisikiliza mawaidha. 
WANAFUNZI wa Madrasat mbalimbali waliohudhuria
 sherehe za kuadhimisha mwaka wa Kiislam leo  duniani
 katika viwanja vya Kisonge Michezani  
[ Read More ]

UJENZI UKUTA WA UWANJA WA NDEGE WAANZA.


SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeanza ujenzi wa ukuta utaozunguka Uwanja wa Kimataifa Abeid Amani Karume wenye urefu wa kilomita 12.

Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa Idara ya Anga, Malik Mohamed Hanif, alisema ujenzi huo unafanyika chini ya Kampuni ya Sagea Satom ya Ufaransa, ambayo ndio iliyohusika katika upanuzi wa Njia ya kurukia ndege na kutulia hivi karibuni, ambapo tayari kazi hiyo imekamilika na kuruhusu ndege kubwa kutua nchini.

Alisema ujenzi wa ukuta utahusisha kilomita 10 utakuwa kwa kiwango cha zega na kilomita mbili utawekwa waya (senyenge) ili kuruhusu kuonekana vizuri kwa kiwanja hicho.

Alifahamisha kuwa, ujenzi huo unafadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni tano na kazi ya ujenzi wa zege imeshaanza na kufikia kilomita tatu katika maeneo ya Mombasa na Kisauni.

Aidha alisema maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa ya upanuzi wa njia ya kurukia ndege na kutulia, Zanzibar imepata sifa kubwa kutoka kwa kampuni mbali mbali zinazotoa usafiri ndani na nje ya nchi.

Malik alieleza upanuzi wa njia ya kurukia ndege na kutilia imefikia kwa urefu kilomita 3022 kutoka kilomita 2462 za zamani na kufikia upana wa mita 45 kwa sasa, jambo ambalo limeongeza uwanja huo kuwa na hadhi ya kimataifa.

Hata hivyo, alisema sambamba na upanuzi huo lakini barabara yake (njia ya kurukia ndege na kutulia), iko imara zaidi katika viwango vya kimataifa hadi kufikia PCN 61, ambayo inauwezo wa kuhimili vishindo vya ndege za aina mbali mbali.

Mkurugenzi huyo, alisema hivi sasa kuna maombi ya kampuni tatu za mashirika ya ndege, ambazo zimepeleka maombi ya kuja kuangalia uwanja huo ili kuweza kuleta ndege zao Zanzibar, ambapo miongoni mwa kampuni hizo ni Shirika la Oman Air na Kampuni ya Emirates.
[ Read More ]

UJENZI WA JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE KUANZA JANUARI.


JENGO la kisasa la abiria katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, utaanza Januari mwakani ambao utagharimu dola za Marekani milioni 70.4 hadi kukamilika kwake.

Mkurugenzi wa Anga, Malik Mohamed Hanif, alisema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti hili, mjini hapa amesema ujenzi huo utaanza mapema mwezi ujao na utachukuwa miaka mitatu hadi kukamilika kwake, ambao utagharimu Dola za Marekani milioni 70.4.

Alisema jengo hilo litajengwa na kampuni ya Beijing Enginering Construction Group (BECG) ya China ambayo imeshinda zabuni ya ujenzi huo.

Alieleza hatua za awali za matayarisho zimeshafanyika za kupima udongo na hivi sasa kazi inayoendelea ni kuingiza vifaa vya ujenzi nchini ili kazi hiyo iweze kuanza mwezi ujao.

Aidha alifahamisha kuwa, ujenzi huo pia utahusisha barabara katika eneo la jengo hilo sambamba na kuweka maeneo maalum ya maegesho ya vyombo vya moto, ili kuweka haiba nzuri ya muonekano wake.

Ujenzi wa jengo jipya la kisasa la abiria linajengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kupata fedha za mkopo nafuu kutoka China.

Hata hivyo kujengwa kwa jengo hilo litasaidia kuondoshea kero abiria wanaosafiri na wananchi mbali mbali wanakwenda kuwapokea wageni wao au kuwasindikiza katika uwanja huo.
[ Read More ]