Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa mkazi mmoja wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina moja la Thabiti ndiye aliyeligundua kaburi hilo alipokuwa akitafuta sehemu ya kuchimba jalala, jirani na Hospitali ya Mwananyamala.

“Mzee Thabiti aliamua kuwataarifu polisi ambao walifika eneo la tukio, jirani na makaburi ya Mwananyamala. Baada ya kuona hali ilivyokuwa, polisi waliwapigia simu madaktari waliowasili muda mfupi baadaye,” kilieleza chanzo chetu.
POLISI KUFIKA ENEO LA TUKIO
Habari zinaeleza kuwa mara baada ya polisi kupewa taarifa hizo na kuwasili eneo la tukio wakiwa kwenye gari aina ya Landrover ‘defender’ walianza uchunguzi wao mara moja.

Dakika chache baadaye shimo likiwa na urefu wa futi nne, lilionekana shuka jeupe likiwa limeviringishwa kitu. Lilipotolewa, kwa mshangao mkubwa maiti ya kitoto kichanga ikadondoka.
Polisi aliyekuwa akifanya kazi hiyo alipolichunguza vizuri shuka lile, aligundua kuwa kuna kitu kingine kimebaki. Alipoingiza mkono, alichomoa maiti nyingine ya kitoto kichanga.
KANGA KIBAO ZILITUMIKA
Askari huyo aliendelea na zoezi hilo na baadaye akalifunua kabisa shuka hilo, ndipo alipokuta maiti nyingine za watoto wachanga zikiwa zimevingirishwa kwenye kanga tofauti.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa moja ya kanga iliyokutwa kwenye kaburi hilo ilikuwa imebandikwa plasta yenye maneno yaliyosomeka: ‘Ruth Mtanga, Male Pre-mature (yakimaanisha kuwa mwanamke mwenye jina hilo alikuwa amejifungua ‘njiti’ wa kiume).
Haikufahamika maandishi yale kwenye plasta hiyo yameandikwa na nani katika hospitali gani, hivyo polisi wakaanzia uchunguzi wao hapo.

DAKTARI AKACHA WANAHABARI
Daktari mmoja wa Hospitali ya Mwananyamala aliyefahamika kwa jina moja la Karamahia, alipohojiwa kuhusiana na shuka hilo pamoja na maiti za watoto hao wachanga, alikataa kusema chochote kwa madai kuwa tayari sakata hilo lipo mikononi mwa polisi.
Polisi waliondoka na miili hiyo kuelekea Hospitali ya Mwananyamala, ilikoenda kuhifadhiwa wakati uchunguzi wa kina ukiendelea.

WANANCHI WALIVYOSIKITISHWA
Hata hivyo, baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo waliliambia Uwazi kwa masikitiko kuwa kitendo hicho siyo cha kibinadamu na ni tukio la kwanza la kutisha kugundulika hapa nchini.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa watoto hao hawakuzikwa siku nyingi zilizopita kwa sababu walikuwa bado hawajaharibika sana.

source-global publisher
Pichani kati Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania (BTA), Juliana Urio,akizumgumza na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusina kuanza kambi wa warembo wa shindano la Kisura wa Tanzania 20110.kushoto ni Meneja masoko wa SBC,Bwa.George Michael,Afisa Mipango Ujana wa FHI Bwa.Aziz Itaka,Mwisho kabisa ni Meneja Masoko wa ATCL,Bwa. Musyangi Kajeri
WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini mapmea jana katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.
Mchakato wa kuwapata wasichanahao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.
Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.
Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),
Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).
Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.
Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records

Mchakato wa kuwapata wasichana
hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.
Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.
Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),
Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).
Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.
Mkurugenzi msaidizi wa hospitali ya CCBRT Haika Mawala akimkaribisha Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba wa pili toka kushoto akiambatana na Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo walipotembelea hospitali ya CCBRT kwa lengo la kujionea jinsi gani huduma ya Vodafone M pesa inavyosaidia wagonjwa wa fistula na mdomo wa sungura kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.

Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba