Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote waishio Reading UK walioweza Kuja Leo mchana Vincent kuchangia wahangwa wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa mda wa saa moja tumekusanya Jumla ya pesa taslim Pounds £200 Pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali. Tafadhali Kumbuka bado hujachelewa kwa wakazi wa Reading ambao hawakuweza kufika leo mnaweza kupeleka michango yenu Vincent siku ya mwisho ya kukusanya ni jumanne ijayo tarehe 1.3.11.
Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, MRS NASIBU, MRS NTULLY SCHULZ NA Utawala wa Vincent Restaurant Reading kwa kusaidia zoezi la leo.
Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni
"SAIDIA GONGO LA MBOTO"
wadau wa UK wakifuatilia mpango mzima wa Harambee
Mdau akichangia
Mkurugenzi Mtendaji wa LOCUS IMPEX SHIPPING MR B CHISUMO akifungua Harambee
Mtoto Chanele akimpa Mchango wake Miss Jestina
Toa Ndugu Imeanza
Toa Ndugu ikiendela
Jestina Akiwa kazini
Frank Kutoka Urban Pulse akiwa na tina kutoka Miss Jestina Blog wakila pozi baada ya harambee
Baada ya kazi, kutoka kushoto JJ, Chisumo, Miss Jestina,Gardol na Frank