Watu waklikinga vikombe kupata dawa kutoka kwa Mchungaji mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambikile Mwasapile nyumbani kwake Kijiji cha Samunge,Ngorongoro.Hutibu magonjwa ya Ukimwi na merngine sugu kwa sh 500 tu.
Gari inayoonyesha namba za usajili SM, ni mali ya Manispaa ya Arusha. Gari hili ni moja ya magari ya Serikali yakiwa nayo yanasonga mbele kwenye foleni ya kunywa dawa inayogawiwa na mchungaji Mwasapile kwa kikombe abiria wakiwa humohumo ndani ya gari.
misururu ya magari mbali mbali iliyoleta wagonjwa na wasio wagonjwa kwenda kunywa dawa dawa ya Mugariga katika kijiji cha Samunge wilayani Loliondo, aliyooteshwa na Mzee Mwasapile mwaka 1991.
Watu wakiwamo waasia mbalimbali kutoka Mkoa wa Arusha, Manyara na sehemu kadhaa za Tanzania na nje ya Nchi wakisubiri dawa ya Mugariga kwa ajili ya kujitibu.
----
MAELFU ya watu, wakiwemo vigogo wa serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa nchini, wamefurika katika Kijiji cha Samunge Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro kupata 'dawa ya maajabu ya Mungu' inayodaiwa kutibu magonjwa mengi sugu ikiwamo Ukimwi.
Helkopta za wafanyabiashara na magari zaidi ya 1,000 yakiwamo magari ya serikali, binafsi na mashirika ya kimataifa ikiwamo Umoja wa Mataifa (UN) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, yamefurika katika kijiji hicho kilichopo umbali ya takriban kilometa 400 kutoka Jiji la Arusha.