Wakati watanzania wakiungana na watu mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani Aids Week in Review linaandika:Wizara ya Afya naUstawi wa Jamii, imesema spiriti inayotumiwa katika mashine za kunyolea na vifaa vya kutengenezea kucha katika saluni za kike na kiume nchini Tanzania, haziui virusi vya Ukimwi.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hadji Mponda pamoja na kutoa kauli hiyo alisema njia pekee ya kuwa salama wakati wa kutumia vifaa vya saluni ni kuvitakasa(sterilization).
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema), aliyetaka kufahamu kauli ya Serikali juu ya matumizi ya vifaa vya saluni na uhusiano katika maambukizi ya Ukimwi na kamaspiriti zinasaidia kuua wadudu vikiwemo virusi vya Ukimwi.
Alisema ili kuepuka uwezekano wa kutokea kwa maambukizi,wenye saluni na wanaokwenda katika saluni hizo waepuke kuchangia matumizi ya vifaa vyenye ncha kali.
Pia vifaa vyenye ncha kali vinapotumika kwa zaidi ya mtu mmoja ni vema vikatakaswa au kuua vijidudu kwa dawa.