Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Just In: Rais Jakaya Kikwete Ateua Wabunge Wapya Watatu Zakhia Meghji Na Shamsi Vuai Nahodha Waula


Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
Zakia Hamdan Meghji
-------------
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete,amefanya uteuzi wa Wabunge watatu(3)kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(e)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha,Prof.Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Anne Semamba Makinda(Mb)kwa ajili ya hatua zipasazo.

MWISHO

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010
[ Read More ]