Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (katikati), akiwa amekaa na Mbunge Mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (kushoto), akimpa moyo, baada ya hukumu kutolewa.
Mmoja wa wafuasi wa Chadema, Naomi Solomon (56), akiwa amepoteza fahamu, mara baada ya mahakama kutangaza kumtengua Ubunge Godbless Lema.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katikati akihutubia umati wa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika mahakamani kusikiliza shauri la kupinga ubunge wake, ambapo mahakama imeutengua ikidai Lema alikiuka sheria za uchaguzi na kuamuru uchaguzi urudiwe.
Umati wa wafuasi wa Chadema ukisikitishwa na uamuzi wa mahakama ya mjini Arusha, ulitolewa na Jaji, Gabriel Rwakibarila wa mahakama kuu kanda ya Sumbawanga.
habari na global.p