Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

MTANZANIA AFUNGWA MAISHA MAREKANI!!!!


Mfungwa wa kwanza katika jela ya Guantanamo kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia, Ahmed Ghailani kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya jimbo la Manhattan.

Ghailani alipatikana bila hatia mwaka jana, katika kesi ambayo alishtakiwa kwa mauaji pamoja na mashtaka mengine kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 katika balozi za Marekani mjini Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania


Mchoro ukionyesha Mtanzania Ahmed Ghailani

Jopo la majaji hata hivyo limempata na hatia ya kufanya njama ya kuharibu majengo ya serikali.

Upande wa mashtaka ulijaribu kumshawishi jaji kwamba Ghailani alipaswa kuonewa huruma kwa sababu hakujua kuhusu njama hiyo.

Vile vile walisema kuwa Ghailani aliteswa na CIA baada ya kukamatwa.

Hata hivyo waendesha mashtaka walitaka apewe kifungo cha maisha gerezani huku wakisisitiza kuwa alijua kuhusu njama hiyo.

Akijiandaa kutoa hukumu yake, Lewis A. Kaplan alisema ilikuwa siku ya haki kwa jamii za watu 224 waliofariki kwenye mashambulizi ya bomu ya mwaka wa 1998 pamoja na wale wote waliojeruhiwa.

Kaplan alisema aliridhishwa na ushahidi aliopata kwamba Ghailani alijua kwamba watu wangekufa kutokana na vitendo vyake.

Ghailani alikamatwa nchini Pakistan mwaka 2004.

Alipelekwa kwenye kambi ya siri inayosimamiwa na shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo Bay, Cuba, mwaka 2006.

Baadaye alihamishwa hadi New York alikoshtakiwa.
Credit to BBC.
[ Read More ]

KESI YA JERRY MURO ILIVYOUNGURAMA LEO

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imepokea pingu, miwani na hati ya upekuzi katika kesi ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 inayomkabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Jerry Muro kama kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo.
Vielelezo hivyo viliwasilishwa jana mahakamani hapo na Ofisa wa Polisi dwani Nyanda ambaye ni shahidi wa sita katika kesi hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Gabriel Mirumbe.
Shahidi huyo aliieleza Mahakama kuwa Januari 29, mwaka 2010 akiwa ofisini kwake alipokea maagizo kutoka kwa mkuu wake wa kazi Kamishina wa Upelelezi Charles Mkumbo akimtaka kufanya upekuzi katika gari yenye namba za usajili T 545 BEH mali ya Jerry Muro.
Alidai alishuka kwenda kulifuata gari hilo lililokuwa limepaki kwenye maegesho ya magari ya kituo kikuu cha polisi kati akiwa na mlalamikaji Michael Wage pamoja na mashahidi wengine ili kushuhudia zoezi la upekuzi huo.
“Wage aliyekuwa analalamika kutishiwa kuuawa na Muro alikuwepo makusudi ili kuitambua miwani yake aliyodai kuisahau katika gari ya Muro siku aliyokamatwa na pingu aliyodai kutishiwa kufungwa nayo.
“Baada ya upekuzi huo vitu vyote vilirekodiwa na kusainiwa na mimi na Muro mwenyewe kama uthibitisho kwamba kweli vitu hivyo vilikutwa garini kwake,” alidai shahidi huyo.
Katika kesi hiyo Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratius Mgasa wanadaiwa kuomba rushwa ya Sh milioni 10, kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage, Januari 29 mwaka jana.
Mwendesha mashitaka wakili Mkuu wa Serikali Boniface Stanslaus alidai kwa jana upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja ambapo wengine watatu waliobaki watatoa ushahidi wao pindi kesi hiyo itakapopangiwa tarehe nyingine. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 7 na 8, mwaka huu itakaposikilizwa tena.
[ Read More ]