Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

HAPPY BIRTHDAY NELSON MANDELA

 Nelson Rolihlahla Mandela.
 
LEO ni siku ya kuzaliwa kwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela. Mzee Mandela ametimiza miaka 95 ya kuzaliwa mbali na afya yake kuwa mbaya baada ya kuwa mahututi kwa muda mrefu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini. Tunamtakia kila la kheri Mzee Mandela katika siku yake ya kuzaliwa leo.

[ Read More ]

MAMA AMCHOMWA MWANAE NA MKASI MARA 90 KWA MADAI YAKUMG'ATA ZIWA AKIWA ANANYONYA.

Maskini unyama mwingine hauna hata maana maybe alikuwa amechanganyikiwa
Kweli ukistaajabu ya Musa....
Ni kama miujiza kwa mtoto wa kichina kuwa hai mpaka sasa licha ya kuchomwa chomwa mara 90 na mama yake mzazi huko China kwa madai kuwa alimng’ata ziwa mama yake wakati akinyonyeshwa.
Kwa mujibu wa Daily Mail mtoto huyo Xiao Bao mwenye miezi 8 tu ameshonwa zaidi ya nyuzi 100 ili kuurudisha uso wake katika hali nzuri baada ya shambulizi hilo lililotokea katika jiji la Xuzhou mashariki mwa China.
Bao anaishi na mama yake pamoja na wajomba zake wawili ambao wanajishughulisha na ukusanyaji wa taka kwaajili ya kipato. Mmoja wa wajomba hao ndiye aliyegundua kuwa Bao ameumizwa baada ya kumkuta akiwa amelala kwenye damu iliyotapakaa nyumbani hapo kabla hajamkimbiza hospitali
Mama wa mtoto huyo baadaye alikiri kumchoma choma mwanae na mkasi mara 90 hususan eneo la usoni baada ya mtoto huyo kumng’ata ziwa wakati akimnyonyesha.
Baada ya tukio hilo majirani wa familia hiyo wameiomba serikali imnyang’anye mama huyo wa kichina mtoto kwa sababu za kiusalama, lakini ombi hilo limekataliwa kwa madai kuwa hakuna uthibitisho wowote mpaka sasa kama mwanamke huyo anamatatizo ya akili, lakini wameongeza kuwa hata hivyo mtoto huyo bado ana walezi wengine wawili anaoishi nao (wajomba zake)
Mtoto huyo anaendelea kupata nafuu akiwa hospitali.

Source: Vijimamb
[ Read More ]