
Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi na wakaazi wa mikoa ya kusini kwa ujumla, wanatarajia kunufaika na ugunduzi wa gesi katika visiwa vya Zafaran na Lavan vilivyopo wilayani huo. Kampuni ya Statoil kutoka nchini Norway ikishirikiana na Exxon Mobil imegundua gesi katika Visiwa vya Zafaran na Lavan vilivyopo Kitalu namba 2, Ukanda wa Pwani ya Tanzania, hususan Pwani ya Kilwa