Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

VODACOM FOUNDATION...YAFUNGUA NAMBA YA MAAFA ILI KUSAIDIA GONGOLAMBOTO


   Vodacom Foundation kusaidia wahanga wa Gongolamboto

Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba ameviambia vyombo vya habari kwamba
Kampuni yake kupitia  mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umeguswa na janga la milipuko ya mabomu yaliyotokea  katika kambi ya Jeshi Gongolamboto Jijini Dares Salaam:Na hivyo kumfanya kuamua maamuzi ya haraka kama  yafuatayo.

1.  Kufungua tena namba yao ya maafa ili kuruhusu watanzania ambao wangependa kuchangia wenzao kufanya hivyo kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15599 kupitia mitandao yote.
Ujumbe huu utatozwa shilingi 1000 na pesa zote zitaenda kwenye tume ya maafa ya serikali ili kuweza kununua vitu vya dharura vya wahanga. Red alert itawasha rasmi kesho ijumaa tarehe 18.
2. Vodacom Foundation itatoa chakula na vinywaji  kwa  siku nzima ya ijumaa kwa wahanga zaidi ya 1000 waliopo Uwanja wa taifa ambao wengi wao ni watoto
3. Pia Vodacom foundation imetoa namba za simu kwa timu ya clouds ilioanzisha kituo cha habari na matukio huko shule ya mzambarauni ukonga. Namba hizi zinatumika kupiga bure na kutoa taarifa ya kupotelewa Ndugu au jamaa na pia kutoa taarifa ya maafa zaidi ambayo hayajulikani ili taarifa ziende kwa wahusika. Namba hizi ni 0767 111401 , 0767111402 na 0767111403
4. Pamoja na kuwawezesha watanzania kutuma mchango wao kupitia ujumbe mfupi, Vodacom Foundation pia unakusanya misaada ya chakula na maji na vifaa mbalimbali katika Ofisi zao zilizopo Mlimani city kwa watu ambao hawajui waipeleke wapi. Misaada hiyo itakabidhiwa kwa red Cross ambao wanahudumia wahanga waliopo Uwanja wa taifa na sehemu  mbalimbali
[ Read More ]