Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

WAZAZI WA MTOTO ALIYEZALIWA MZUNGU UINGEREZA KUPIMWA DNA



WAZAZI wa mtoto aliyezaliwa mzungu nchini Uingereza wamekubali uamuzi wa wataalamu wa vina saba kumfanyia uchunguzi mtoto huyo.

Habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa wazazi hao Benjamin na Angela wamekubali mtoto huyo wa kike afanyiwe uchunuzizaidi ili kuibaini sababu za kuzaliwa akiwa katika hali kama hiyo.

Mtaalamu wa vina saba kutoka Chuo Kikuu cha London Dkt.Mark Thomas amesema kuwa ana wasiwasi huwenda kuna mchanganyiko wa chembechembe nyeupe na zile na zile zinasobabbisha mtu kuwa na ulemavu wa ngozi albino.

Baba mzazi wa binti huyo Benjamni kwa upande wake amesema kuwa lichabya kukubali matokeo ya jinsi mtoto huyo alivyo,bado wataendelea kutafuta sababu za mtoto huyo kuzaliwa hivyo.

Mtoto huyo alizaliwa na wazazi weusi ambao ni raia wa Uingereza wenye asili ya Nigeria na inaelezwa kuwa katika familia yao hawana historia ya kuzaliwa mtu wa aina kama hiyo.Benjamin ambaye ni mshauri wa huduma kwa wateja alisema kuwa alipomuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza alishtuka lakini baadaye akasema kuwa ni mwanaye na anamuamini sana mkewe.

Alisema mkewe ni mwaminifu kwake sana na walihamia nchini humo wakitokea Nigeria miaka mitano iliyopita. 

[ Read More ]