Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA LULU


Lulu (katikati) akiingia mahakamani na askari magereza wa kike.
Kamera zikimfuata kwa shauku.
Hapa ni karibu na mlango wa kuingia katika chumba cha mahakama.
Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitu iwa na mshitakiwa huyo.
[ Read More ]

MKAPA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU


Mkapa akiingia Mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi.
Akisindikizwa kuelekea kizimbani.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, leo amepanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kuhojiwa na mawakili wa serikali na wanaomtetea aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italy, Costa Mahalu, kwenye kesi ya ufujaji fedha katika ununuzi wa jengo la ubalozi inayomkabili balozi huyo.
Jengo hilo lilinunuliwa kwa shilingi, bilioni 2.9.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL
[ Read More ]