Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Oman Oktoba mwaka 2012 baada ya kualikwa na Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said ambapo aliambatana na ujumbe wa mawaziri na viongozi waandamizi wa biashara.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete alibadilishana uzoefu wa uhusiano na kuangalia namna ya kudumisha
ushirikiano wa nchi hizo mbili kuhusiana na biashara, elimu, utamaduni na mambo mengine.
Hiyo ilikuwa ni ziara ya pili muhimu ya kiongozi wa Tanzania kutembelea nchi hiyo tangu mwaka 1985 wakati Rais wa kwanza, hayati Julius Nyerere akiwa madarakani.
Ziara hiyo ya Rais Kikwete inaonyesha umuhimu wa namna nchi hizo mbili zinavyojenga mahusiano makubwa na undugu baina yao.
Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Oman lililofanyika Oktoba 16 katika Hoteli ya Al Bustan Palace wakati Rais Kikwete akitoa hotuba yake.
Kongamano hilo liliangalia fursa za kibiashara katika rasilimali zilizopo katika nchi hiyo iliyopo Ukanda wa
Afrika Mashariki zikiwemo kilimo, viwanda, utalii, usafirishaji, mafuta na gesi.
Kituo cha Uwekezaji (TIC)Tanzania kiliwasilisha namna uwekezaji katika kiuchumi na nafasi za uwekezaji nchini Tanzania.
Mwishoni mwa tukio hili muhimu, malaka za nchi hizi mbili zilisaini na kukubaliana kuanzisha Baraza la Biashara kati ya Oman na Tanzania ambalo litakuwa ni hatua muhimu katika kuanzisha uhusiano wa mataifa hayo mawili katika ngazi ya juu.
Madhumuni mengine muhimu ya ziara hiyo yalikuwa ni pande hizo mbili kusaini makubaliano ya kukuza na kuulinda uwekezaji jambo ambalo ni kichochezi katika Baraza hilo la Biashara la Oman na Tanzania, itarahisisha kutoa fursa za kibiashara na uwekezaji kati yao.
Pia makubaliano ya kupeana ushauri katika masuala ya siasa yamesainiwa hivyo itakuwa ni njia nzuri ya uzileta nchi hizo mbili zenye undugu karibu katika jambo hilo
muhimu.
Walisaini makubaliano kuhusu Utunzaji kumbukumbu na Nyaraka ambazo zinatunza kumbukumbu za historia muhimu kwa vile nchi hizo mbili zina historia inazofanana kiasi fulani.
Kubadilishana huko kwa nyaraka na kumbukumbu za historia kunaweza kusaidia kuchimbua matukio
ya kihistoria yaliyotokea zama hizo. Walisaini makubaliano ya kushirikiana katika elimu ya juu.
Oman na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu hivyo ziara hiyo ya Rais Kikwete inalenga
kufungua fursa nyingi na hatimaye kufikia ngazi wanazostahili wananchi.
Nchi hizo zinafaidika na upendo baina ya watu wake kwa sababu Oman ni nchi pekee nje ya Afrika ambako wananchi wengi wanazungumza Kiswahili na Wa-Oman wamezaliana na Watanzania pamoja
na kuwa na utamaduni wa aina moja.
Kuna uwezekano mkubwa wa kufungua fursa za usafiri wa ndege ndani na nje ya Afrika katika uwekezaji na biashara katika juhudi za kibinadamu.
Tanzania ina fursa kubwa za uwekezaji katika sekta za
mifugo, uvuvi na kilimo.
Ikiwa imebarikiwa kuwa na eka za ardhi yenye rutuba, maji na hali nzuri ya hewa, Tanzania ni mahali
pazuri kwa Oman kuwekeza na kukuza shughuli za kilimo ili kufanikisha mahitaji yake.
Hii ni namna Oman inavyoweza kujibadilisha yenyewe kutoka kuwa muingizaji wa bidhaa nchini na kuwa muuzaji wa bidhaa za matunda na mboga mboga nje ya
nchi hivyo kujihakikishia kutokuwa tegemezi wa chakula.
Kwa vile Tanzania imegundua visima kadhaa vya Mafuta na gesi, na nchi hizo mbili zinaweza kuanzisha
ushirikiano katika suala hili ambalo litawanufaisha wote kwa pamoja.
Oman inaweza kuwekeza katika miundombinu iliyokua nchini Tanzania kama barabara, madaraja, hoteli,
resort na pia katika usafirishaji, na sekta ya usafiri wa njia ya meli.
Pia sekta ya viwanda itatoa fursa za uwekezaji kwa Serikali ya Oman na jamii ya biashara.
Cha muhimu ni kwamba nchi ya Tanzania yenye ananchi 44,929,002 inahudumia soko la watu milioni 150 katika nchi zake za jirani kupitia Bandari ya Dar es
Salaam.
Tanzania ni nyumbani kwa baadhi ya maeneo muhimu duniani kwa shughuli za utalii na miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wageni kutoka Oman wakienda nchini Tanzania jambo ambalo limefanya safari za ndege za Ndege ya Oman ziwe nyingi.
Tanzania ni nchi kubwa zaidi Afrika Mashariki ikiwa na jiografia inayoruhusu uwekezaji katika sekta ya utalii ambapo pia inasifika kuwa na hali nzuri ya hewa, ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha na rasilimali
ambayo inavutia uwekezaji.
Baada ya ziara Rais Mheshimiwa Dk.Jakaya Kikwete, Umoja wa wadau wa biashara nchini Oman umeamua kuwekeza fedha kiasi cha sh.bilioni 160 ili kuendeleza Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Hatua hiyo ilikuja baada ya mkutano kati ya Kikwete na ujumbe wa wafanyabiashara hao.
Akizungumza wiki hii, Mwenyekiti wa Al Hayat Development na kampuni yake ya uwekezaji, Sheikh
Salim Al Harthy alisema wanashukuru kwa msaada huo uliotolewa na Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said Sultan wa Oman.
Alisema wanashukuru kwa vile msaada huo utasaidia na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili hasa baada ya makubaliano kufikiwa kati ya viongozi wa nchi hizo.
Na kama sehemu ya kujitolea kwao huko wanadhamiria kusaini makubaliano na Air Tanzania na kuwekeza
dola milioni 100 na kuongoza wawekezaji ambao tumekuwa na uhusiano nao wa karibu.
Alisema uekezaji huo utatumika katika kukodisha na kununua ndege ambazo zitatumika katika safari za
ndani na nje ya Afrika kukuza biashara ndani ya Tanzania na nchi
nyingine.
Sheikh Salim Al Harthy aliongeza kuwa fursa hiyo ilikuja kwa ukarimu na matarajio mazuri ya Rais Kikwete na Serikali ya Tanzania kwa kutuamini kuja kuwekeza
katika kushughuli za kiuchumi nchini Tanzania.
“Tunamshukuru Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said wa Oman na Rais Kikwete wa Tanzania kutupa nafasi
hiyo hasa ukizingatia kipindi hiki tuna mpango wa kujenga kituo cha mafunzo ya masuala ya ndege, ofisi
nzuri kwa ajili ya ATCL, kununua ndege na kufanya shughuli nyingine za maendeleo tunazotarajia kuanza
ndani ya miezi sita hadi kumi” alisema.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akiwa na Mtukufu Sultan Qaboos Bin Said wakati wa
ziara yake nchini Oman.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Al Hayat, Shaikh Salim Al Harthy, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro. Wa kwanza kushoto ni Al Sayyid Fahar Bin Taimur Al Said na kulia ni Bwana Saeed S. Bawazir kama wa wakilishi wa Al Hayat inchini Tanzania.