Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Shahidi akitoa ushuhuda kuhusiana na kutupwa kwa vichanga 11

[ Read More ]

UKATILI: MAITI ZA VITOTO 11 ZAFUKULIWA SHIMO MOJA.

KATIKA hali isiyo ya kawaida, wakazi wa Mwananyamala Kwakopa, jijini Dar es Salaam wamepatwa na mshituko mkubwa baada ya kaburi moja kugundulika jana (Jumatatu) likiwa na watoto 11 waliozikwa ndani yake, tukio lililoelezwa kuwa ni ukatili wa kutisha, Uwazi lina habari kamili.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa mkazi mmoja wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina moja la Thabiti  ndiye aliyeligundua kaburi hilo alipokuwa  akitafuta sehemu ya kuchimba jalala, jirani na Hospitali ya Mwananyamala.
Ilielezwa kuwa mzee huyo alipofika eneo hilo alishtuka baada ya kuona nzi wengi wamezingira huku kukiwa na harufu kali, machale yakamcheza na kuhisi kuwa huenda kuna kitu kibaya kimefukiwa.

“Mzee Thabiti aliamua kuwataarifu polisi ambao walifika eneo la tukio, jirani na makaburi ya Mwananyamala. Baada ya kuona hali ilivyokuwa, polisi waliwapigia simu madaktari waliowasili muda mfupi baadaye,” kilieleza chanzo chetu.

POLISI KUFIKA ENEO LA TUKIO
Habari zinaeleza kuwa mara baada ya polisi kupewa taarifa hizo na kuwasili eneo la tukio wakiwa kwenye gari aina ya Landrover ‘defender’ walianza uchunguzi wao mara moja.
Mwandishi wetu aliyekuwepo eneo la tukio, alishuhudia kazi ya kufukua kaburi hilo ikifanywa kwa uangalifu mkubwa.

Dakika chache baadaye  shimo likiwa na urefu wa futi nne, lilionekana shuka jeupe likiwa limeviringishwa kitu. Lilipotolewa, kwa mshangao mkubwa maiti ya kitoto kichanga ikadondoka.

Polisi aliyekuwa akifanya kazi hiyo alipolichunguza vizuri shuka lile, aligundua kuwa kuna kitu kingine kimebaki. Alipoingiza mkono, alichomoa maiti nyingine ya kitoto kichanga.

KANGA KIBAO ZILITUMIKA
Askari huyo aliendelea na zoezi hilo na baadaye akalifunua kabisa shuka hilo, ndipo alipokuta maiti nyingine za watoto wachanga zikiwa zimevingirishwa kwenye kanga tofauti. 
Zilipohesabiwa ilibainika kuwa jumla ya maiti 11 zilikuwa zimefukiwa kwenye kaburi hilo.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa moja ya kanga iliyokutwa kwenye kaburi hilo ilikuwa imebandikwa plasta yenye maneno yaliyosomeka: ‘Ruth Mtanga, Male Pre-mature (yakimaanisha kuwa mwanamke mwenye jina hilo alikuwa amejifungua ‘njiti’ wa kiume).

Haikufahamika maandishi yale kwenye plasta hiyo yameandikwa na nani katika hospitali gani, hivyo polisi wakaanzia uchunguzi wao hapo.
Uchunguzi wa gazeti hili eneo la tukio ulibaini kuwa shuka lililotumika kuviringishia maiti za watoto hao lilikuwa imeandikwa Mwananyamala.

DAKTARI AKACHA WANAHABARI
Daktari mmoja wa Hospitali ya Mwananyamala aliyefahamika kwa jina moja la Karamahia, alipohojiwa kuhusiana na shuka hilo pamoja na maiti za watoto hao wachanga, alikataa kusema chochote kwa madai kuwa tayari sakata hilo lipo mikononi mwa polisi.

Polisi waliondoka na miili hiyo kuelekea Hospitali ya Mwananyamala, ilikoenda kuhifadhiwa wakati uchunguzi wa kina ukiendelea. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela alipohojiwa na gazeti hili jana, alisema taarifa hizo amezipata na anazifanyia kazi hivyo apewe muda.

WANANCHI WALIVYOSIKITISHWA
Hata hivyo, baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo waliliambia Uwazi kwa masikitiko kuwa kitendo hicho siyo cha kibinadamu na ni tukio la kwanza la kutisha kugundulika hapa nchini.
“Haya mambo ya binadamu kuzikwa kaburi moja tulikuwa tukiyasikia kwa wenzetu lakini sasa tumeyashuhudia hapa leo. Haya ni mambo ya kutisha,” alisema shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Zuwena.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa watoto hao  hawakuzikwa siku nyingi zilizopita kwa sababu walikuwa bado hawajaharibika sana.



source-global publisher
[ Read More ]

WASHIRIKI WA SHINDANO LA KISURA WA TANZANIA 2011 WAANZA KAMBI.



Pichani kati Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania (BTA), Juliana Urio,akizumgumza na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusina kuanza kambi wa warembo wa shindano la Kisura wa Tanzania 20110.kushoto ni Meneja masoko wa SBC,Bwa.George Michael,Afisa Mipango Ujana wa FHI Bwa.Aziz Itaka,Mwisho kabisa ni Meneja Masoko wa ATCL,Bwa. Musyangi Kajeri
WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini mapmea jana katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.

Mchakato wa kuwapata wasichana
hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.

Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),

Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).

Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records

[ Read More ]

ZAIDI YA WAGONJWA 263 WA FESTULA NA MDOMO WA SUNGURA WAMENUFAIKA NA HUDUMA YA M PESA


Mkurugenzi msaidizi wa hospitali ya CCBRT Haika Mawala akimkaribisha Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba wa pili toka kushoto akiambatana na Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo walipotembelea hospitali ya CCBRT kwa lengo la kujionea jinsi gani huduma ya Vodafone M pesa inavyosaidia wagonjwa wa fistula na mdomo wa sungura kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.
Mkurugenzi msaidizi wa hospitali ya CCBRT Haika Mawala akimkaribisha
Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba
Mkurugenzi wa Vodafone Foundation wa Egypt Noha Saad kushoto akisaini kitabu cha wageni katika hospitali ya CCBRT mara baada ya kutembelea hospitalini hapo na wakurugenzi wenzake Mwamvita Makamba,Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo wakiwa na lengo la kujionea jinsi gani huduma ya Vodafone M pesa inavyosaidia wagonjwa wa mdomo wa sungura na fistula kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya CCBRT walipotembelea hospitalini hapo kwa lengo la kujionea ni jinsi gani huduma ya M pesa inavyosaidia wagonjwa wa fetula na wa mdomo wa sungura kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo,katikati Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Uingereza Andrew Dunnet,Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Tanzania Mwamvita Makamba.
Mkurugenzi wa hospitali ya CCBRT Tom Vanneste akifafanua jambo kuhusu ugonjwa wa mdomo kisungura na fistula kwa maafisa wa Vodafone M pesa Afrika walipotembelea hospitalini hapo hawapo pichani kujionea jinsi gani huduma ya M pesa inavyosaidia wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.

[ Read More ]

NIZAR KHALFANI AENDELEA KUNG'ARA NYUMBANI NA CANADA


Mchezaji nyota wa Vancouver Whitecaps ya jijini Vancouver huko British Columbia, Canada, akiwa anafundisha watoto kuliskata kabumbu maeneo ya Tabata jijini Dar alipokuja kuchezea Taifa Stars. Nizar amekuwa lulu kwa timu hiyo ya kulipwa na Taifa Stars, yote hii ikitokana na kujituma, nidhamu na kupenda kazi yake. Ni mfano wa kuigwa
Nizar ana mashabiki wengi watoto kwa wakubwa 
na anapeperusha vilivyo bendera yetu
Nizar akinyanyasa ngome ya adui
Nizar akiwakilisha wakati Taifa Stars ilipocheza na Brazil Dar
Nizar huwa haachwi peke yake. akiachwa tu nyavu hizi...
Nizar na kikosi cha kwanza cha Vancouver Whitecaps. 
Kwa habari kamili ya timu hiyo
BOFYA HAPA
[ Read More ]

Nelson Mandela discharged from hospital in South Africa

Nelson Mandela (file image) 

South African former President Nelson Mandela has been discharged from a hospital where he spent two nights.
Surgeon General Vejaynand Ramlakan said Mr Mandela, 92, was suffering from ailments that are common in people his age but was in good spirits.
Deputy President Kgalema Motlanthe - using Mr Mandela's clan name - said: "Madiba is well."
South Africa's liberation hero flew from Cape Town to Johannesburg on Wednesday for a check-up.
Friends and family visited him amid tight security at Milpark hospital on Thursday.
On Friday Mr Ramlakan said Mr Mandela had suffered a respiratory infection, but was responding well to treatment and would be receiving home-based care.
"To us he is stable, but will be subject to intense monitoring," he told reporters.
A convoy is now believed to be taking Mr Mandela to his home in the Johannesburg suburb of Houghton.
Correspondents say he has seemed increasingly frail since retiring from public life in 2004.
His last public appearance was at the football World Cup closing ceremony last July.
[ Read More ]

Mandela 'very sick,' But Not in Danger


South Africa's revered former president Nelson Mandela was Thursday described as "very sick" but his condition was "not life-threatening."
The news that Madiba -- the clan name by which the 92-year-old Nobel Peace Prize winner and country's first elected black leader is affectionately known -- was to spend a second night in hospital has gripped the nation.
The public has grown increasingly concerned for Mandela's health but he could be released as early as today, a source close to Mandela said on condition of anonymity.
"The old man is very sick but his condition is not life threatening," the source said.
"He came in for a checkup but the doctor decided to keep him in for observation.
"He is still not well but we expect him to be released tomorrow."
President Jacob Zuma
described the hospital visit as a checkup and called for calm, but a report said Mandela had been treated for a lung problem.
Mandela spent 27 years in prison for his role in the fight against apartheid in South Africa, emerging in 1990 to lead the transition to democracy.
[ Read More ]

MTANZANIA AFUNGWA MAISHA MAREKANI!!!!


Mfungwa wa kwanza katika jela ya Guantanamo kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia, Ahmed Ghailani kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya jimbo la Manhattan.

Ghailani alipatikana bila hatia mwaka jana, katika kesi ambayo alishtakiwa kwa mauaji pamoja na mashtaka mengine kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 katika balozi za Marekani mjini Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania


Mchoro ukionyesha Mtanzania Ahmed Ghailani

Jopo la majaji hata hivyo limempata na hatia ya kufanya njama ya kuharibu majengo ya serikali.

Upande wa mashtaka ulijaribu kumshawishi jaji kwamba Ghailani alipaswa kuonewa huruma kwa sababu hakujua kuhusu njama hiyo.

Vile vile walisema kuwa Ghailani aliteswa na CIA baada ya kukamatwa.

Hata hivyo waendesha mashtaka walitaka apewe kifungo cha maisha gerezani huku wakisisitiza kuwa alijua kuhusu njama hiyo.

Akijiandaa kutoa hukumu yake, Lewis A. Kaplan alisema ilikuwa siku ya haki kwa jamii za watu 224 waliofariki kwenye mashambulizi ya bomu ya mwaka wa 1998 pamoja na wale wote waliojeruhiwa.

Kaplan alisema aliridhishwa na ushahidi aliopata kwamba Ghailani alijua kwamba watu wangekufa kutokana na vitendo vyake.

Ghailani alikamatwa nchini Pakistan mwaka 2004.

Alipelekwa kwenye kambi ya siri inayosimamiwa na shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo Bay, Cuba, mwaka 2006.

Baadaye alihamishwa hadi New York alikoshtakiwa.
Credit to BBC.
[ Read More ]

KESI YA JERRY MURO ILIVYOUNGURAMA LEO

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imepokea pingu, miwani na hati ya upekuzi katika kesi ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 inayomkabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Jerry Muro kama kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo.
Vielelezo hivyo viliwasilishwa jana mahakamani hapo na Ofisa wa Polisi dwani Nyanda ambaye ni shahidi wa sita katika kesi hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Gabriel Mirumbe.
Shahidi huyo aliieleza Mahakama kuwa Januari 29, mwaka 2010 akiwa ofisini kwake alipokea maagizo kutoka kwa mkuu wake wa kazi Kamishina wa Upelelezi Charles Mkumbo akimtaka kufanya upekuzi katika gari yenye namba za usajili T 545 BEH mali ya Jerry Muro.
Alidai alishuka kwenda kulifuata gari hilo lililokuwa limepaki kwenye maegesho ya magari ya kituo kikuu cha polisi kati akiwa na mlalamikaji Michael Wage pamoja na mashahidi wengine ili kushuhudia zoezi la upekuzi huo.
“Wage aliyekuwa analalamika kutishiwa kuuawa na Muro alikuwepo makusudi ili kuitambua miwani yake aliyodai kuisahau katika gari ya Muro siku aliyokamatwa na pingu aliyodai kutishiwa kufungwa nayo.
“Baada ya upekuzi huo vitu vyote vilirekodiwa na kusainiwa na mimi na Muro mwenyewe kama uthibitisho kwamba kweli vitu hivyo vilikutwa garini kwake,” alidai shahidi huyo.
Katika kesi hiyo Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratius Mgasa wanadaiwa kuomba rushwa ya Sh milioni 10, kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage, Januari 29 mwaka jana.
Mwendesha mashitaka wakili Mkuu wa Serikali Boniface Stanslaus alidai kwa jana upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja ambapo wengine watatu waliobaki watatoa ushahidi wao pindi kesi hiyo itakapopangiwa tarehe nyingine. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 7 na 8, mwaka huu itakaposikilizwa tena.
[ Read More ]