Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Rolls Royce la Thamani Kubwa...Lakini Kamwe Hutatamani Kulipanda





Stylish final journey: The Rolls-Royce hearse is converted from a Phantom for those who want the ultimate send-off

Pricey: The one-off funeral chariot is thought to be worth over £400,000, according to its makers

High-spec: The Rolls-Royce hearse has a 6.75-litre V12 engine developing 453bhp and a suspension designed to be the smoothest and most comfortable on the road

Gari hili la kifahari lina thamani ya zaidi ya pauni laki nne za Kiingereza (zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania) lakini cha kuogopesha sio hiyo thamani pekee bali ukweli kwamba NI GARI LA KUBEBEA MAITI...!!!
na Evarist Chahali.
[ Read More ]

Have a nice day

[ Read More ]

Serikali Kutafuta Mwekezaji Eneo la Mangapwani



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inatafuta mwekezaji mwengine katika eneo la Mangapwani wilaya ya kasikazini “B” Unguja baada ya Shirika la Agakhan Foundation kushindwa kuliendeleza eneo hilo ambalo walikodishwa na Serikali kwa lengo la kuliendeleza.

Hayo yamesemwa leo huko Baraza La Wakilishi Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwiji Haji Makame wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma (CCM) aliyetaka kujua hatma ya mwekezaji huyo ambaye kashindwa kuliendeleza eneo hilo kwa muda mrefu.


Dk.Mwinyi Haji akijibu swali hilo amesema kwamba mkataba wa mradi huo umefutwa tokea mwaka 2008 baada ya kusimamishwa mkataba wa kukodishwa ardhi kutokana na muekezaji huyo kushindwa kutekeleza yale aliyoagiza.

Aidha alisema kuwa kutokana na mradi huo kufutwa kabisa na muwekezaji kushindwa kuomba kurejeshewa kwa mradi huo serikali inatafuta mwekezaji mwengine ambae ataweza kuliendeleza eneo hilo kwa kuweka miradi mbalimbali .

Dk.Mwinyi Haji alisema kwamba, kwa sasa Serikali imepokea maombi mengi kwa waekezaji wengine kwaajili ya kuliendeleza eneo hilo ili kutimiza azma ya kuwawezesha wananchi wa Mangapwani kupata ajira.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Thuwaiba Edington Kisasi amesema kuna viashiria vinavyoonesha kuongezeka kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi Pemba kutokana na ujazo wa fedha uliojitokeza kwa sababu ya mavuno ya Karafuu.

Thuwaiba aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayuob aliyetaka kujua iwapo bei mpya ya Karafuu imesaidia kuinua kipato cha wakulima.

Thuwaiba amevitaja viashiria hivyo vya kiuchumi kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa ujenzi wa nyumba za kudumu na za kisasa,kuongezeka kwa ununuzi wa vipando kama vile magari na pikipiki na ongezeko la uanzishwaji wa miradi midogo midogo ya maendeleo.

Kikao hicho kidogo cha Baraza la Wawakilishi kimenza leo katika Ofisi zake zilizoko Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar ambapo inatarajiwa kuchukua muda wa wiki mbili.
[ Read More ]

Tujihadhari na utapeli huu


Nilikua njiani naelekea ofisini kwangu, nikiwa mitaa ya Darajani Zanzibar simu yangu iliita aliyenipigia alijitambulisha na nilikua simjui, alisema yupo Mkoani Kigoma anafanya kazi shirika moja la kimataifa, alinieleza anahitaji mtu wa kushirikiana naye katika mambo ya kibiashara anayetoka Zanzibar, alidai alipatiwa namba yangu na moja kati ya rafiki zangu wanao ishi Uk, na hakutaka nimuulize niliendelea kumsikiliza.
Akaanza kunielekeza anafanya Biashara ya kununua Product ambayo inahifadhi vyakula visiharibike na akanipatia namba ya mtu anayehusika katika utengenezaji wa production na jina lake akadai anaitwa Ibrahim na anapatikana Mahonda Zanzibar, akaniambianimpigie Ibra kumuuliza kama hiyo Production ipo na inapatikana kwa bei gani, nilimpata Ibrahim na akanieleza wanazo bidhaa kutoka ncho tofauti lakini best zinatoka Sweeden na bei yake kwa chupa 2 ni T shs 1,200,000/= nikamjibu yule jamaa aliyenitambulisha kwa Ibra kwamba bei yake ndio hiyo, baada ya hapo akaniambia kwamba pia wapo mabosi wake wa kizungu wamefikia Zamani Kenpisky Hotel Pwani Mchangani wananunua hiyo bidhaa kwa bei ya juu sana mara 2 ya bei ya kununulia, wakati nawasiliana na hawa jamaa tokea dakika ya kwanza niligundua kwamba hawa ni matapeli na nilichukua hatua za kuripoti tukio hili kituo cha Polisi na walifika kwa wakati nikawa nawashirikisha katika mawasiliano na hawa matapeli.
Polisi niliwapatia namba za simu za hawa jamaa wakaweza kuzifanyia utafiti na wakagungua wenye kuzimiliki, na sasa baada ya muda mfupi nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwamba anaitwa Fred yupo Kenpsky na ameelekezwa kwangu kuja kununua Product mimi sikujivunga nikamwambia zitapatikana ndio hapo akaniambia kabla sijapeleka mzigo nimpelekee sample 1 pair ili akiridhika nao ndio tunaondoka pamoja na kwenda kuchukua mzigo wote.
Nikamweleza yule jamaa aliyenipigia simu mwanzoni kwamba wanunuzi wanahitaji sample wakiridhika ndio wanunue mzigo wote, hivyo akaniambia niwasiliane na Ibra kuhusu sample nikampigia akaniambia beio yake ndio hiyo aliyoniambia hapo juu Milioni moja na laki mbili, nikamjulisha jamaa akaniambia nifanye maarifa nipeleke hizo pesa.
Nikawaeleza Polisi tukaweka mtego baada ya muda kidogo nikawaambia kwamba fedha tayari waniletee mzigo, wakanielekeza walipo wakaniambia wapo Kibweni tukaenda mimi nilitangulia na polisi wakiwa nyumba yangu kwa umbali kidogo, nikapiga simu akaja kijana mmoja akaniuliza ni wewe niliyeagizwa kuhusu mzigo nikamwambia ni mimi na mzigo uko wapi nikupatioe hizo fedha? akaniambia nimsubiri kidogo akaufuate niliendelea kusubiri pale na kupiga simu hakutokea baadae alizima simu kabisa.
Nikawaarifu polisi kwamba jamaa wameshtuka nikarudi ofisini kwangu. nilichoamua kufanya baada ya hapo niliwapigia simu wale jamaa wote tuliokuwa tunawasiliana kwamba nawashukuru sana mzigo nimeupata na tumeshafanya biashara nimemkabidhi jamaa Milioni moja na Laki mbili ispokuwa jamaa aliyepokea pesa alitaka wale jamaa wote wasijue kama tayari ameshapokea fedha.
na nikawashukuru sana sikujua kilichoendelea baada ya hapo, hii ni tahadhari natoa kwa wenzangu wa JF na watanzania tuwe makini na tujiepushe na tamaa za kijinga tutaingizwa mjini.
nawasilisha.
[ Read More ]