Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

AJALI....




Mtoto Mwanaidi Ibrahim (4) (kulia), ambaye wazazi wake wote wawili walifariki dunia katika ajali ya gari, Kibamba juzi, akiwa amebebwa na Mama yake mdogo, Sharifa Ally wakati wa maombolezo ya msiba wa wazazi wake hao, Kibamba, Dar es Salaam jana. Kushoto ni ndugu yake Salha Jaffar (3). Mtoto huyo kwa sasa amebaki yatima.

Ajali ya gari iliyochukua nafasi juzi alfajiri eneo la Kibamba, Dar ndani yake kuna zaidi ya tukio, baada ya kuibuka kwa taarifa mpya kwamba kulikuwa na wanandoa watarajiwa ambao roho zao zilizimika papo papo...

ndani ya daladala lililoangukiwa na lori la mafuta, kulikuwa na wanandoa watarajiwa ambao walikuwa safarini kwenda Morogoro kwa ajili ya kukusanya michango ya harusi.

Kwa mujibu wa mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Chaudama Emanuel, wanandoa watarajiwa waliopoteza maisha ni Justin na Helen.

Akifafanua kila kitu, Chaudama alisema kuwa Justin na Helen walipata ajali hiyo walipokuwa wanakwenda kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi yanayokwenda mikoni na nchi jirani, Ubungo ambako walikuwa wapande basi la Hood kwenda Moro.

“Kwanza kulikuwa na ubishi wa wao wenyewe, masikini mdogo wangu (Justin) alitaka wasubiri basi hapa hapa Kibamba, lakini wifi akataka wakapandie Ubungo, kwahiyo Justin akamsikiliza mchumba wake kumbe walikuwa wanafuata wito wa Mungu,” alisema Chaudama.

Aliongeza: “Walikuwa wanakwenda Morogoro kufuata michango ya harusi, walitakiwa kurudi leo leo (juzi) jioni au kesho (jana) asubuhi na ndoa yao ingefungwa Jumamosi (leo) kanisani kwa sababu sisi ni Wakatoliki.”

MKOSI
Wakati hali ikiwa hivyo kwa Justin na Helen ambao pumzi yao ilikatika siku mbili kabla ya kutimiza tukio muhimu katika historia ya binadamu, yaani ndoa, ‘ishu’ nyingine ya kusikitisha ni kuwa, mwanamke aliyekuwa amesotea mtoto kwa muda mrefu, akiwa njiani kwenda kujifungua kwenye hospitali ya Mwananyamala, Dar ni mmoja wa abiria waliopoteza maisha hali inayotafsiriwa na wakazi wa Kibamba kuwa ni mkosi wa mji huo.

Katika ushuhuda wa gazeti hili baada ya ajali hiyo, mtoto mchanga akiwa amepoteza maisha, alitokeza kwenye tumbo la mama huyo, tukio ambalo liliwaliza wengi walioshuhudia.

Shuhuda mmoja aliyezungumza na gazeti hili eneo la tukio na kueleza kwamba anamfahamu mwanamke huyo aliyekuwa mjamzito, alisema kwamba alikuwa na mumewe wakienda hospitali ya Mwananyamala baada ya kushikwa na uchungu.

“Walikuwa wanakwenda hospitali Mwananyamala, sasa Mungu ana yake ndiyo maana wamepata ajali kabla ya kufika hospitali. Inasikitisha sana,” alisema mtoa habari wetu huku akijifuta machozi.

Katika ajali hiyo, Lori la kubeba mafuta lenye namba za usajili T192 ABP, lililiangukia daladala aina Hiace na kuua abiria wote waliokuwemo.


Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, katika idadi hiyo, waliopoteza maisha ni wanaume wanane na wanawake watatu.

Kutokana na ajali hiyo, waandishi wetu walizunguka mitaa mbalimbali ya eneo la Kibamba ambako ndiko inasemekana watu wengi waliopoteza maisha wanaishi, na kushuhudia nyumba nyingi zikiwa katika hali ya utulivu.

Picha iliyoshuhudiwa na Risasi Jumamosi ni kuwa japo si kila nyumba iliyokutwa na msiba lakini uzito wa tukio hilo, ulivuta hisia za watu wengi ambao waliungana na wafiwa kuomboleza.

chanzo cha habari hii:GLOBAL PUBLISHER.





[ Read More ]

AJALI:LORI LA MAFUTA LAIANGUKIA HIACE.


mwili ukiwa umenasa kwenye gari hilo



Leo majira ya saa kumi na nusu alfajiri, lori lenye namba za usajili T 189 ABP na tela lake lenye namba za usajili T 192 ABP lililokuwa limebeba mafuta kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kibaha Pwani, limepata ajali mbaya na kuliangukia basi dogo la abiria (Hiace) lenye namba za usajili T 615 AJW katika eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na kusababisha basi hilo dogo kupondeka vibaya.

Ajali hiyo ya kutisha imesababisha vifo vya watu 7 waliokuwa ndani ya basi dogo, baada ya lori hilo kulilalia basi hilo lililokuwa likitokea Kibamba kwenda Ubungo. Akiongea na mwandishi wetu aliyefika eneo tukio, Kamanda Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga , alisema kuwa basi hilo dogo aina ya Hiace lilikuwa na abiria saba ambao wote wamefariki dunia, na kati ya maiti hizo, ni maiti mbili tu ndizo zilizoweza kutolewa hadi muda huu tena zikiwa vipandevipande.

Katika maiti hizo zilizotolewa, moja ni ya mwanamke ambae hakuweza kutambuliwa kwa wakati ule na na mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Shukuru Hussein, maarufu kama Kibwetere, mkazi wa Kibamba. Aidha Kamanda Mpinga aliongeza kuwa bado utaratibu unaendelea kwa kuwa lori lilikuwa limejaza mafuta hivyo imeleta ugumu katika utoaji hadi mzigo wote utakapoisha na kuweza kufanya utaratibu wa utoaji.

Kamanda Mpinga aliweza kumtaja dereva wa lori ambaye amekimbia mara baada ya tukio hilo kutokea kuwa ni Kudura Adam na mmiliki wa Lori hilo ametambuliwa kwa jina la Mahamudu Mohamed.

Hata hivyo baada ya ndugu wa mmiliki wa Hiace kupatikana na kudai mwenyewe yuko Mkoani Kilimanjaro, walisema kuwa mmiliki huyo anaitwa Selemani Khalfan na Hiace yake huwa inalala Ubungo Kibo maeneo ya Rombo na kumtaja Dereva wa Hiace hiyo kwa jina moja kuwa ni Seif na Kondakta wake Faraji Ismail Kalama ambao mpaka sasa bado maiti zao hazijatolewa eneo la ajali.

SOURCE:GLOBAL PUBLISHERS.

[ Read More ]