Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

MATOKEO YA WANAFUNZI KIDATU CHA PILI YAKO JUU ZANZIBAR



Wanafunzi wa skuli ya Kengeja Pemba
Idadi ya wanafunzi waliofaulu kuingia kidatu cha tatu kwa mwaka 2010 imeongezeka kwa asilimia 58.2 kutoka asilimia 54.2 ya mwaka 2009, huku skuli ya Kajengwa wilaya ya kusini ikishika nafasi ya kwanza.
Taarifa ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kidato cha pili ya mwaka 2010 iliyotolewa na wizara ya elimu imesema jumla ya wanafunzi elfu 19, 855 waliofanya mtihani kati yao elfu 11, 562 wamefaulu kuingia kidatu cha tatu.
Taarifa hiyo imesema jumla ya wanafunzi elfu moja 610, wakiwemo wanawake elfu moja na 49 hawakufanya mitihani kwa sababu mbali mbali, huku kukiwa na kesi 58 za udanganyifu.
Skuli tatu bora zilizofanya vizuri ya kwanza ni skuli ya sekondari ya Kajengwa wilaya ya Kusini, skuli ya Kiuyu wilaya ya Micheweni na skuli ya Maungani wilaya ya magharibi.
Skuli zilizofanya vibaya ni Mwambe Shamiani ambayo haikupasisha mwanafunzi hata mmoja, skuli ya Mgogoni wanafunzi wanane, skuli ya Umbuji wanafunzi sita, skuli ya Michamvi wanafunzi saba na skuli ya Shengejuu mwanafunzi mmoja ambapo kwa sasa skuli hizo hazitakuwa na madarasa ya kidatu cha tatu.
Kwa upande wa darasa la Saba jumla ya wanfunzi elfu 18, 908 wamechaguliwa kuingia kidatu cha kwanza sawa na asilimia 81.2 kati yao wanafunzi mia moja na 77 wataingia madarasa ya vipawa maalum na 952 wamechaguliwa kuingia mchipuo.
Skuli bora kwa upande wa darasa la Saba ya kwanza ni Kizimbani Pemba, Mtiulaya na Jongowe Unguja na skuli zilizofanya vibaya Kandwi, Mkokotoni na Kikobweni zote za Unguja. Majina ya wanafunzi hao yanatarajiwa kutangazwa leo.
[ Read More ]

Binti wa Will Smith's Hot


Willow Smith(10) akiwa katika harakati za kurekodi video ya wimbo wake










Kikazi zaidi

Mtoto wa wasanii nyota wa Hollywood, Will Smith na Jaden Pinkett akiwa kikazi zaidi wakati akimrekodi dada yake, Willow.
Willy Smith na mkewe, Jada Pinkett Smith wakionesha hisia wakati wakimshuhudia binti yao akirekodi video ya wimbo wake (wa Willow).
Gwiji wa sinema, Jack Chen nae alikuwepo kumshuhudia Willow
Jaden Smitth akiwa kazini wakati dada yake anafanya mavituz ya kupata shots za video ya wimbo.
Willow hakuwa peke yake, alikuwa na dancers kunogesha 'shughuli'

[ Read More ]

TAARIFA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA KUHUSU TOLEO LA NOTI MPYA

Gavana Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Benno Ndulu akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Kuhusu noti mpya zinazotumika nchini kuwa zina ubora na viwango vya kimataifa na kuwataka wananchi kuwa makini katika kufwatilia na kuzitambua alama muhimu za noti halali ikiwemo ile ya kutoa rangi pindi inaposugulia kwenye karatasi nyeupe.Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki (BOT) Bw Emmanuel Boaz
Toleo jipya la Noti za Tanzania,Marekani  na Rwanda ambazo zina ubora na kiwango cha kimataifa zikionyeshwa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jana.Picha na Aron Msigwa-MAELEZO
---

BENKI KUU YA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 

KUHUSU TOLEO LA NOTI MPYA
 


1. Mwezi Januari 2011 Benki Kuu ya Tanzania ilitoa toleo jipya la notiza Shilingi 500, 1000, 2000, 5,000 na 10,000. Baada ya kipindi chatakriban mwezi mmoja sasa, pamejitokeza dukuduku na maswali mbalimbali
kutoka kwa wananchi. Kwa kuwa ni maswali ambayo yakijibiwa yatasaidiakuelimisha jamii katika ufahamu wa noti hizi tumeona ni vyematukayajibu kupitia kwenu.

2. Maswali yaliyopokelewa au kuandikwa katika vyombo vya habariyameonekana kutaka kutoa uelewa zaidi katika maeneo yafuatayo:

2.1 Noti mpya zikisuguliwa kwenye karatasi nyeupe zinaacha rangi nakwamba zikilowa zinatoa rangi. Je hali hii haitokani na uduni wa notihizi mpya?

Hali ya kuacha rangi noti zinaposuguliwa kwenye karatasi nyeupe ni yakawaida kwa noti zote zilizochapishwa kwa teknolojia maaluminayojulikana kwa kitaalamu kama “Intaglio Printing”. Aina hii yauchapishaji (Intaglio Printing) inazifanya noti kuwa na hali yamparuzo zinapopapaswa. Teknolojia hiyo imetumika ili kuimarisha kingoza noti kwa lengo la kupunguza uwezekano wa kuchanika na kuchakaaharaka. Miparuzo hii huacha rangi noti inaposuguliwa kwa nguvu kwenyekaratasi nyeupe kitendo ambacho kinathibitisha kuwa noti hiyo nihalali. Hali hii pia ni moja alama ya usalama (security feature)inayothibitisha kuwa noti siyo ya bandia.

Aidha, noti halali hazichuji zikilowekwa kwenye maji kama inavyodaiwakwa kuwa wino uliotumika hauyeyuki katika maji. Vilevile noti hizizimetengenezwa kwa teknolojia ya kuwekewa kinga dhidi ya uchafu
inayojulikana kitaalamu kama “Anti Soiling Treatment” ili kupunguzauwezekano wa kunasa uchafu inapokuwa katika mzunguko.Teknolojia hizi mbili zinalenga kuongeza uhai wa noti katika mzunguko.

2.2 Je noti za zamani bado ni halali na zinaendelea kutumika?

Noti za zamani bado ni noti halali na zitaendelea kuwa katika mzungukopamoja na zile mpya mpaka zitakapotoweka kwenye mzunguko kwa sababu zauchakavu wake. Kwa hiyo wananchi wanashauriwa kuendelea kutumia notiza toleo la zamani bila wasiwasi wowote.

2.3 Kwa kuwa noti mpya ni ndogo kuliko za zamani kwa umbo je thamani ya noti hizo siyo pungufu kulizo zile za toleo lililotangulia?

Thamani ya noti ni ile iliyoonyeshwa kwa tarakimu zilizoandikwa kwenye noti yenyewe bila kujali ukubwa wake. Kwa hiyo thamani ya noti za zamani na za sasa haitofautiani.

2.4 Kwa kuwa kumekuwa na matatizo ya upatikanaji wa noti mpya, je Benki Kuu ina mipango gani kuhakikisha noti mpya zinapatikana nchi nzima?

Benki Kuu huingiza noti mpya katika mzunguko kwa kupitia benki za biashara. Benki Kuu inaendelea kutoa noti hizo mpya kupitia benki hizo lakini kwa kuwa mtandao wa baadhi ya matawi ya benki hizo ni mpana
imechukua muda mrefu kwa baadhi ya maeneo kufikiwa na noti hizo. Hata hivyo kwa kuwa biashara nchini haina mipaka, noti hizo zitaendelea kusambaa nchini kote kupitia mzunguko wa kibiashara na kuongezeka siku
baada ya siku.

2.5 Je noti halali zinatofauti gani na noti bandia?

Ili kuhakiki uhalali wa noti tunawashauri wananchi kuzichunguza kwa makini noti kwa kutumia alama za usalama kama zilivyoainishwa kwenye matangazo na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu ama kuwasiliana na ofisi zetu kwa ufafanuzi zaidi pale mtu anapokuwa na mashaka na noti hizi.

2.6 Je Benki kuu ina mikakati gani ya kuelimisha jamii na hasa
vijijini kuhusu toleo jipya la noti?

Mtakumbuka baada ya uzinduzi wa noti mpya tarehe 17 Desemba 2010nilisema noti hizi zitaanza kuingizwa katika mzunguko Mwezi Januari 2011. Hii ililenga kutoa kipindi cha kutoa elimu kwa jamii kupitia
vyombo vya habari kuhusu toleo jipya kabla ya kuliingiza katika mzunguko. Aidha Benki Kuu ina mikakati endelevu ya kufikisha elimu ya “tambua noti zako” kwa wananchi wote kupitia matangazo, semina,
ushiriki katika mikusanyiko mikubwa kama Sabasaba na nanenane na kwenye masoko pamoja na minada mikubwa ya mifugo. Tovuti ya benki kuu Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania vilevile imetoa maelezo mazuri kuhusu kutambua alama muhimu katika noti.

2.7 Kwa kuwa Benki Kuu inabadilibadili fedha kila baada ya miaka mitano hadi saba. Je ni kwa nini isiwe na toleo la kudumu kama ilivyo kwa fedha ya Uingereza au ya Marekani?

Kubadili noti husababishwa na maendeleo ya teknolojia ya uchapaji wa noti katika kuongeza uhai wa noti katika mzunguko na kuweka alama bora zaidi za usalama ambazo ni ngumu kuzighushi. Aidha sio kweli kwamba Uingereza na Marekani hazijabadili noti zake. Kuna mabadiliko makubwa
na mengi tu yaliyopita na yanayotarajiwa kwa noti za nchi hizi.

2.8 Kwa nini Benki Kuu haikutoa noti kubwa zaidi ya 10,000 ilikurahisha malipo katika biashara?

Benki Kuu haikuona haja ya kutoa noti yenye thamani kubwa zaidi kwa sasa kwani malipo makubwa yanahimizwa kufanywa kupitia njia nyingine za kibenki. Noti ya Shilingi 10,000 bado inakidhi mahitaji ya malipo ya kawaida katika biashara kwa sasa.

Ni matumaini yetu kwamba ufafanuzi huu utaondoa wasiwasi uliokuwepo na kujenga imani kuhusu noti zetu mpya. Na Benki Kuu na matawi yake iko tayari kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu noti zetu mpya pindiunapohitajika.

Asanteni sana

Prof Benno Ndulu
Gavana
Benki kuu ya Tanzania

3 Februari 2011
[ Read More ]

SHIRIKA LA UMEME LASHINDWA KUTUMIA JENERATA MPYA KUTOKANA NA GHARAMA KUBWA


Majenereta ya Shirika la Umeme Zanzibar
Shirika la umeme Zanzibar ZECO limesema linashindwa kuzitumia Genereta zake 32 za akiba kwa kuzalisha nishati ya umeme kila unapokatika umeme kutoka gridi ya taifa kutoakana na gharama kubwa za mafuta ya kuendesha genereta hizo.
Akizungumza na zenji fm radio afisa uhusiano wa ZECO Salum Abdalla Hassan amesema Shirika hilo  limekuwa likiwasha Genereta hizo kila siku kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne za usiku ambapo huzalisha Megawati 10 ili kusaidia Megawati 40 kutoka Gredi ya taifa kutokana na ongezeko la mahitaji kwa wateja hasa katika nyakati hizo.
Amesema kwa sasa shirika hilo linatumia  wastani wa shilling Milioni 400 kila mwezi kuzalisha Megawati 10 kwa masaa matano kila siku…
Hata hivyo amesema kukosekana kwa huduma ya umeme leo hii kunatokana na Shirika la umeme Tanzania TANESCO Kufanya kazi zake za kawaida za usafishaji mitambo yake katika kituo cha Ras Kiromoni kabla ya umeme huo kupokelewa katika kituo cha Fumba.
[ Read More ]

TANZANIA YAWEKA HISTORIA UMOJA WA MATAIFA


DKT. SERVACIUS LIKWELILE, NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI AKIWASILISHA MPANGO WA PAMOJA WA MAENDELEA KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGAO WA TANZANIA NA MASHIRIKA MANNE YA UMOJA WA MATAIFA KATIKA MOJA YA VIKAO VYA BODI TENDAJI ZA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA. VIKAO VYA BODI TENDAJI ZA UNDP, UNICEF, WFP NA UNFPA VINAFANYIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA, JIJINI NEW YORK, MAREKANI.
---
NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka historia ya kuwa nchi ya kwanza duniani kuandaa Mpango wa Pamoja wa Maendeleo kwa kushirikiana na Mashirika Manne yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa (UM).
Mashirika hayo ni Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la kuhudumia watoto (UNICEF), Mpango wa Chakula Duniani(WFP) na Shirika linalohusika na Idadi ya watu (UNFPA). 
Kufuatia kukamilishwa kwa mchakato huo wa aina yake, Jumuia ya Kimataifa imeipongeza na kuisifu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuonyesha njia na kuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine.
Mpango huo ambao unajulikana kama Common Country Programme Document (CCPD), Umewasilishwa mbele ya Bodi tendaji za UNDP na UNFPA na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelile. Ukiwa ni sehemu ya Mpango Mkubwa wa Umoja wa Mataifa ( UNDAP).
Bodi Tendaji za Mashirika hayo manne zinafanya mikutano yao ya kikazi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.Ambapo Tanzania ilipatiwa fursa ya kuwasilisha Mpango huo.
Utekelezaji wa CCPD utafanyika kwa miaka minne kuanzia Julai 2011 hadi June 2015. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mpango huo itapata Dola za Kimarekani 773 milioni zitakazotolewa na Umoja wa Mataifa.

Akiuwasilisha CCPD Naibu Katibu Mkuu anasema, maandalizi na utekelezaji wake umezingatia vipaumbele na mipango ya maendeleo ambayo Serikali zimeainisha kupitia MKUKUTA kwa Tanzania Bara na MKUZA kwa Tanzania Visiwani.

“ Ingawa tumeshirikiana na mashirika hayo tangu hatua zote za maandalizi hadi utekelezaji wake, huu ni mpango wetu, tunaumiliki wenyewe na tumehakikisha unakidhi vipaumbele ambavyo Serikali zimejiwekea katika kuharakisha maendeleo ya wananchi wake” anasema Dkt. Likwelile.
Anaongeza kuwa maandalizi hayo pia yamewashirikisha wadau wengine zikiwamo asasi zisizo za kiserikali.
Dkt. Likwelile anasema kwa Tanzania kuwasilisha mpango huo katika Bodi tendaji za Mashirika hayo, kumeipa fursa nchi ya kutoa uzoefu wake kwa nchi nyingine wa namna ya mchakato mzima ulivyofanyika. 
“ Lakini hii pia ni changamoto kwa UM, kwa sababu kwanza, hawakutegemea kwamba tungefikia hatua hii, tumewaonyesha njia, na tunawapa changamoto ya kuwa sasa wana mahali pa kuanzia katika kuboresha mfumo wa utendaji katika ngazi ya nchi”, anasisitiza Naibu Katibu Mkuu. 
Akasema kuwa Mpango unaweza kutumika kama mwongozo kwa UM kama ulivyo au kwa kuuboresha kwa kuzingatia mahitaji na malengo ya nchi husika.
Akielezea manufaa ya kuwa na CCPD,Dkt Likwelike anayataja manufaa yake kuwa ni pamoja na kuboresha utendaji kazi, utekelezaji, ufuatiliaji, ufanisi katika matumizi ya raslimali fedha.
Manufaa mengine ni kujenga uwezo wa raslimali watu ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ili kwa pamoja waweze kukabiliana na changamoto za kuleta maendeleo.

Kupitia CCPD, sasa inakuwa rahisi kujua nani anafanya nini na katika eneo gani, na itasaidia kupunguza muingiliano wa shughuli kati ya Shirika moja na jingine na kwa upande mwingine Serikali itaondokana na urasimu na ukiritimba wa kufanya kazi na shirika moja moja.
Maeneo yatakayonufaika na mpango huo ni Mazingira, HIV/AIDS,Elimu, Afya, Ukuaji wa Uchumi, Utawala Bora na Masuala ya Wakimbizi.

Bi Anne Webster kutoka Ubalozi wa Ireland, akizungumza kwa niaba ya mataifa 17 anasema.
“ Kama marafiki wa maboresho ya mfumo wa UM, na baada ya kufuatilia kwa makini mchakato wote huu. Tumeridhishwa sana na kazi iliyofanywa.Tunapenda kutambua na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hatua hii ya kihistoria” 

Nchi hizo ni Japan, Sweden, Uingereza, Ujerumani, Jumuia ya Ulaya, India, Canada, Finland, Belgium, Denmark,Netherelands, Norway, Ireland, Ufaransa, Spain, Switzerland na Marekani.
Akasema nchi hizo zinaunga mkono kwa dhati Mpango huo kwa sababu unaifanya Tanzania kuwa mshirika mkubwa wa UM katika maeneo muhimu ya Maendeleo.

Watendaji Wakuu wa Mashirika ya UNDP Bi Helen Clark na UNFPA Dkt. Babatunde Osotimehin, nao kwa nafasi zao walitumia fursa hiyo kuutambua, kuupokea na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuukamilisha, lakini pia kwa hatua mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
[ Read More ]