Mtoto unamuona katika picha ni mwanafunzi wa shule ya msingi Buguruni anasoma darasa la tatu siku yanamkuta haya alikuwa na kosa la kutokuwa na daftari mwalimu anaeitwa Ms.Haule ni mdada tu akampiga na kumfinya kwa kumvuta ngozi ya macho na hicho ndio kilichotokea.Mtoto nyama ya macho ikamtoka nje,macho yakawa mekundu yanatoa tu machozi mtoto akawa kama kapoteza fahamu hata kusikia akawa hasikii.Jamani nimesikitika sana kila nikiangalia picha hii machozi yananitoka siwezi kuitazama.Mtoto anaendelea na matibabu katika hospital ya CCBRT ambako baba yake amempeleka.Baba wa mtoto anasikitika sana hana hakika kama mtoto wake atakuwa sawa!!
Hivi ninavyoandika mwalimu kakimbia haijulikani alipo na polisi wanamtafuta.Kwa nini lakini mwalimu umefanya hivyo haukuwa na kitu kingine cha kumuadhibu huyo mtoto mpaka macho yake uyavute??Poor kid nahisi anasikia maumivu makali sana na huyu mtoto lazima hata kisaikolojia hayupo sawa.Wewe mwalimu huko uliko hata kama umejificha ila hutajificha milele hata kama si mkono wa sheria kukuangukia ila mwenyewezi Mungu atakuonyesha nguvu yake!!!
habari na dina marios