Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mjadala wa Wazi Matokeo ya Mtihani




Inshaallah Kesho Jumamosi asubuhi saa 2.30 katika ukumbi wa Beit Al Yamin Malindi kutakuwa na mjadala wa wazi wa wadau wote wa elimu kuhusu matokeo ya mtihani wa taifa kidato cha nne.

Mjadala huo utawashirikisha walimu wa skuli za serikali na binafsi, wazazi, wanafunzi na wadau wengine wa elimu karibuni katika mjadala huo ili kutoa maoni yenu katika mjadala huo.
Kwa wale watakaopenda kufuatilia tutakuwa tukirushwa moja kwa moja kupitia facebook ya Salma Said au mtandao wa www.zanzibaryetu.wordpress.com. Msikose kufuatilia kujua kinachozungumzwa katika mjadala huo muhimu.

Aidha Kesho hiyo hiyo jioni inshallah saa 4:30 eneo la Mapembeani Mwembe Tanga kutakuwa pia na mkutano wa kutoa elimu ya uraia kuhusu katiba, mkutano ambao umeandaliwa na baraza la Katiba Zanzibar

Mnaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo, vitabu vya KATIBA TUITAKAYO vitatolewa bure katika mkutano huo. watakaoongoza utoaji wa elimu ni pamoja na Professa Abdul Shareef, Awadh Said na Ally Saleh. Mnakaribishwa kuhudhuria kwa wingi na mnaombwa kwa kila atakayesikia tangazo hili amuarifu na mwenzake
[ Read More ]