Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, ‘Vodacom Group’ , Pieter Uys, (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare (kushoto) na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba, wakati wa ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Dar es Salaam juzi kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini.
Rais Jakaya Kikwete, akimkaribisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, ‘Vodacom Group’ , Pieter Uys, wakati wa ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Dar es Salaam juzi kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini, (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba, wakati alipoongozana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, ‘Vodacom Group’ ,Pieter Uys (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare (wapili kushoto) kwa ajili ya mazungumzo na rais kuhusu Masuala ya kuongeza uwekezaji nchini, Ikulu Dar es Salaam jana