Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

POLISI ZANZIBAR WAZIMA JARIBIO KUBWA LA UJAMBAZI





Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, limefanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi lilokuwa lifanyike mara baada ya kuchukuliwa kwa mishahara ya watumishi wa hoteli moja ya Kitalii.

Afisa Habari wa Jeshi hilo Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa jaribio hilo limezimwa na Polisi jana Alhamisi Desemba 29, 2011 majira ya saa 7.00 mchana baada ya makachero wa Jeshi la Polisi kupata taarifa mapema na kuweka mtego uliowanasa majambazi watatu kati ya sita.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa majambazi wapatao sita wakiwa na silaha aina ya SMG walijipanga kumteka mhasibu wa Hoteli ya Kitalii ya Blue Bay iliopo Kiwengwa huko Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kamanda Aziz amesema majambazi huo walipanga kufanyika uporaji huo mara baada ya kuchukuliwa kwa mishahara hiyo ya watumishi wa Hoteli ya Blue Bay na tukio hilo lingefanyika njiani wakati mhasibu huyo akitokea katika Tawi la Benki ya Barclays lililopo eneo la Kinazini Mjini Zanzibar na Hoteli ya Blue Bay ya Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema majambazi hayo yalifika eneo la tukio wengine wakiwa kwenye gari dogo na wengine wakiwa kwenye pikipiki za kukodi mbili za kukodi vyombo ambavyo viliegeshwa pembeni mwa barabara inayoelekea Bububu wakimsubiri Muhasibu wa Hoteli ya Blue Bay atoke Benki ili wampore fedha hizo ambazo zilikuwa za kigeni.

Hata hivyo Kamanda Aziz amesema kuwa katika tukio hilo ulifanyika ukamataji salama ambao haukuhusisha matumizi ya silaha na hivyo kunusuru maisha ya majambazi kwa upande mmoja lakini pia na kwa Polisi.

Kamanda Aziz amesema Polisi wamefanikiwa kuzima tukio hilo baada ya kuwa na taarifa za kutosha kutoka kwa wasiri wake ambao ni wananchi.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi, kwa kupitia falsafa ya Polisi Jamii, walipatie taarifa sahihi zitakazowezesha kukamatwa watuhumiwa waliotoroka nakuwataka watu wote wanaokwenda Benki kwa dhamira ya kuweka au kuchukuwa fedha nyingi wawe wasiri na kutoa taarifa Polisi ili wapatiwe usindikizaji salama wa fedha zao.
[ Read More ]


[ Read More ]

DK SHEIN MGENI RASMI MAHAFALI YA SABA SUZA




DHAMIRA ya kuwa na walimu waliofuzu katika kiwango cha Shahada imeanza kufikiwa na katika kipindi kifupo kijacho walimu wote wa skuli za sekondari hapa Zanzibar watakuwa na Shahada ya Chuo Kikuu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), aliyasema hayo katika Mahafali ya saba ya Chuo Kikuu hicho yaliofanyika katika viwanja vya chuo hicho katika Kampasi ya Vuga.

Katika mahafali hayo ambapo pia, aliwatunukia Shahada za Heshima za Uzamivu za Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dk. Salmin Amour Juma na Dk. Amani Abeid Karume kutokana na juhudi zao katika uanzishwaji wa chuo hicho pamoja na juhudi zao katika kuiletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa Zanzibar.


Dk.Shein katika hotuba yake alieleza kuwa katika kuizingatia tathmini ya miaka kumi ya chuo hicho kuna kila sababu ya kuzingatia kukua kwa idadi ya taaluma zinazotolewa chuoni hapo ambapo leo hii wahitimu 139 walipata Shahada zao za Sanaa na Elimu na 63 walipata Shahada ya Sayansi na Elimu.

Dk. Shein aliwahakikishia wanachuo kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano wake katika kuhakikisha chuo hicho kinatoa fani nyenginezo kama vile Utalii, Kilimo na Udaktari na kueleza furaha yake kwa chuo kuanza kutoa wataalamu wa Fani ya Teknohoma (IT).

Katika maelezo yake Dk. Shein pia, alishauri kwamba Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni katika chuo kikuu hicho ikuzwe ili iwez mashuhuri kwa lugha hiyo duniani kama ilivyo kwa chuo kikuu cha Oxford, Uingereza kilivyo mashukuri kwa lugha ya Kiingereza.

Alisema kuwa hilo linawezekana huku akieleza kutofurahishwa na tabia ya semina nyingi hapa nchini kuendelshwa kwa lugha ya kiengereza hali ambayo inaonesha kikiviza kiswahili.

Dk. Shein pia, alitilia mkazo suala zima la utafiti kwani kufanikiwa kupitia utafiti kutaongeza kiwango cha mandeleo katika chuo hicho pamoja na kupata sifa nzuri, wataalamu sanjari na kupata jawabu juu ya matatizo mbali mbali.

Akinukuu maelezo ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika Bwana Obiageli Ezekwesi, alisema kuwa ni muhimu kwa vyuo vikuu kutilia mkazo ubora wa elimu unaokidhi mahitaji ya kisasa ya uchumi uliojaa ushindani.

Kutokana na hali hiyo Dk. Shein alieleza kuwa ni wajibu kujipanga vyema na kuhakikisha kwamba matunda ya vyuo vikuu ni kuchangia maendeleo ya nchi.

Aidha, Dk. Shein akieleza maandiko ya Profesa Manuel Castells kuwa Mfumo wa Elimu ya juu uwe ni injini ya maendeleo katika uchumi wa ulimwengu mpya, alisisitiza kuwa mtazamo huo ukitekelezwa ipasavyo vyuo vikuu vitaweza kutoa mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto za maendeleo ya nchi na wananachi wake.

Alieleza kuwa matarajio ya baadae katika chuo hicho ni kuwa na Vitivo vya Uhandisi, Biashara, Taasisi ya Utafiti na Taasisi ya Sayansi za Bahari na kusisitiza kuwa Vitivo hivyo na viliopo vitasaidia kupeleka mbele maendeleo.

Dk. Shein alieleza kuwa ataendelea kufanya kila jitihada katika kushajiisha na kutilia nguvu ushirikiano utakaoleta tija kwa chuo hicho kwa njia ya mahusiano na vyuo vikuu vya nchi za nje.

Pia, Dk. Shein alieleza kuwa jitihada zitaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha wanafunzi wanasaidiwa ili wawe na mazingira bora ya kujifunzia ikiwemo suala la kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu na kuahidi kuyaangalia maslahi ya Wahadhiri.

“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar itatengewa fedha zaidi katika bajeti zijazo za Serikali kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu”,alisema Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alitoa wito kwa wazazi wanaojimudu pamoja na sekta binafsi kwa jumla waunge mkono juhudi za Serikali katika kuwawezesha watoto kupata elimu kwa lengo la kuleta kasi ya maendeleo nchini.

Mapema Makamu Mkuu wa Chuo cha SUZA, Profesa Idrisa Ahmada Rai alieleza kuwa dhamira kuu ya chuo wakati kinaanzishwa ilikuwa ni kutayarisha walimu wenye sifa ili kukuza elimu ya msingi na sekondari Zanzibar, na baadae kukitanua na kusomesha masomo negine tofauti chuoni hapo.

Alisema kuwa ndani ya miaka 10 ya SUZA hilo limefanikiwa asilimia 100 ambapo kati ya wahitimi 327 wa leo 284 wamesomea ualimu sawa na asilimia 87 ya wahitimu wote na kueleza kuwa hiyo ni ishara ya SUZA kusonga mbele.

Nae Rais mstaafu Dk. Amani Abeid Karume akitoa shukurani baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu kutoka chuo hicho, alieleza kuwa ni mafanikio makubwa kwa chuo hicho tangu kuanzishwa kutoa wahitimu 1427 ambapo ingekuwa vigumu kuwapata wahitimu hao wote iwapo chuo hicho kisingelikuwepo na kueleza kuwa hayo yote ni matunda ya Mapinduzi matukufu ya Januari 1964.

Dk. Shein pia katika Mahafali hayo alitoa zawadi mbali mbali kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao, waanzilishi wa chuo kikuu hicho, Makamu wakuu wastaafu wa chuo hicho, Washirika wa Maendeleo waliokisaidia chuo, wafanyakazi bora na wengineo.

Viongozi mbali mbali walihudhuria akiwemo Makamu wa pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Mawaziri, Mabalozi wadogo wanaofanya kazi zao hapa Zanzibar, wawakilishi wa Jumuiya na Mashirika ya Kimataifa na wengineo.
[ Read More ]

VODACOM YAWAFARIJI WAATHIRIKA.


Sehemu ya shehena ya magodoro 430 yaliyotolewa msaada na Vodacom kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam yakiwa tayari kukabdhiwa kwa kamati ya maafa ya mkoa wa Dar es salaam. Mbali na magodoro Vodacom ilikabidhi pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadiq Meck Sadick ksuhoto akiwa na Mbunge wa Kinondoni Bw. Iddi Azan akipokea magodoro kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule .Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Vodacom Bi. Najengwa Mbagga. Vodacom imekabidhi magodoro 430, mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 30 milioni kusaidia kambi za waathirika wa maafa ya Dar es salaam.

Sehemu ya watoto wanaoishi katika kambi ya waathirika ya maafa ya Dar es salaam katika kambi ya shule ya msingi Mchikichini wakiwa na magodoro yaliyogawiwa na Vodacom kwa waathirika wanaoishi katika kambi hiyo. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation.




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
VODACOM YAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAAFA YA DAR.
*       Yatoa magodoro, mablanketi na vyakula kwenye kambi
Dar es salaam Disemba 23, 2011. Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom leo imekabidhi msaada wenye thamani ya shilingi 30 Milioni kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam wanaoishi katika makambi maalum yaliyofunguliwa kuwawezesha kujihifadhi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya.
Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule amekabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadik Meck Sadiq ukijumuisha magodoro 430 mablanket 800,na vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni kumi.
"Tumeshtushwa sana na hali halisi ya maafa yaliyotukumba jijini Dra es salaam,  tumefika hapa kuendeleza utamaduni wa Vodacom kwa kuonesha upendo na kuwa karibu na wananchi katika nyakati za raha na shida."Alisema Mwakifulefule.
Vodacom imekabidhi msaada huo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ambao umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za maendeleo katika jamii na pia kufariji waathirika nyakati za maafa.
"Mafuriko haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi kuwahi kutokea Dar es salaam katika muda wa miaka mingi iliyopita na hivyo ni wazi athari zake ni kubwa, tunatoa pole kwa wote waliopoteza watoto, ndugu na jamaa na wale walionusurika tunawatakia afya njema na faraja katika wakati huu mgumu wa maisha wanaoupitia"Aliongeza Mwakifulefule Adha kampuni hiyo imetangaza pia fursa kwa wateja wake na wa wananchi kwa ujumla kuungana na Menejimenti na wafanyakazi wake kuchangia walichonacho kupitia nambari maalum ya maafa ya Vodacom Red Alert na kwa njia ya m-pesa.
Kupitia nambari ya Red Alert  wananchi wanaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi  - SMS wenye neno "MAAFA" kwenda nambari15599 na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.
"Mahitaji kwa wenzetu waliothirika ni makubwa. Tuna imani kuwa wote kwa pamoja tutaonesha umoja, upendo na mshikamano wetu wa kitaifa unaojenga tunu ya Utanzania wetu kusaidia wenzetu ambao kwa wakati huu wapo katika mashaka makubwa wakihitaji faraja ya kila aina". Amesema Mwakifulefule.
Michango yote itakayokusanywa kupitia nambari hizi itawasilishwa kwa kamati ya Maafa ya mkoa kuongeza nguvu katika juhudi za kuwasaidia waathirika na kwamba utaratibu wa kuwapatia taarifa wachangiaji utakuwepo.
Aidha kampuni ya Vodacom Tanzania imevipongeza kipekee vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa juhudi kubwa za uokozi kwa kushirikiana na wananchi hatua ambayo imesaidia kunusuru maisha ya maelfu ya watu.
Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa
*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 - Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni - weka namba 155990 Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu - weka namba yako ya simu Hatua ya 5: Weka kiasi - ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri Hatua ya 7:Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia.

Mwisho.

[ Read More ]

HALI INAZIDI KUWA MBAYA DAR-ES-SALAAM. POLE KWA WALIOPOTELEWA NA NDUGU ZAO PAMOJA NA MALI



Maji yakiwa yamelizingira jengo la Mayfair Plaza.

Jengo la hospitali ya TMJ likiwa limezingilwa na maji.
Mtoto kikwea ukuta kujisalimisha.

Baadhi ya wafanya biashara wa vocha katika eneo la Mayfair Plaza wakiwa juu ya vibanda…
Maji yakiwa yamelizingira jengo la Mayfair Plaza.

Jengo la hospitali ya TMJ likiwa limezingilwa na maji.
Mtoto kikwea ukuta kujisalimisha.
Baadhi ya wafanya biashara wa vocha katika eneo la Mayfair Plaza wakiwa juu ya vibanda vyao.
Wasamaria wema wakitoa msaada  kusukuma gari baada ya kuzimikia
kwenye maji.
Lango kuu la kuingia ofisi za Tanesco Mikocheni likiwa limezingirwa maji.
Ukuta wa jengo la Tanesco ukiwa umezingirwa maji.
Nyumba ikiwa imejaa maji.
Vijana wakisuribi maji yapunguwe waweze kupita.
Barabara kuelekea kwenye nyumba ya Mwalimu Julius Nyerere kiwa
imejaa maji.

 


Hapa ni mahali ambapo pamewekwa uzio ili kuzuia watu kuvuka ng'ambo yaani uapnde wa pili.
 Hali ni mbaya katika barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ambapo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiishi hapo, japokuwa serikali imekuwa ikiwaambia hawatakiwa mkujenga katika eneo hilo kutokana na madhara yanayoweza kutokea endapo mvua zitanyesha,Lakini hali ndivyo ilivyo kwa sasa.
Akinamama hawa wakilia baada ya kuokolewa kwenye maji hapa walikuwa wakielekea kupanda gari tayari kwa kuwapeleka hospitali ya muhimbili kwa uangalizi zaidi wa afya zao.Ni  watu wakiokooa vitu vyao na kuviweka kando ya barabara ya Morogoro.
Baadhi ya nyumba zikiwa zimezingirwa kabisa na maji katika eneo la Jangwani.








[ Read More ]

KWA NINI MWANAMKE HULIA?




Kijana mdogo alimuuliza mama yake, "Kwa nini unalia?" mama yake alimjibu "Kwa sababu mimi ni mwanamke,". kijana kwa mshangao akamwambia mama yake "Sielewi,". Mama yake akamkumbatia akamwambia, "Na kamwe, hautaweza kuelewa."
"Wanawake wote wanapenda kulia bila sababu za msingi," ndicho baba yake alichoweza kusema.
Kijana huyo mdogo alikua akawa mtu mzima, na bado akawa anashangaa kwa nini wanawake huwa wanalia. Mwisho, Akaamua kumuuliza Mungu. "Mungu, kwa nini wanawake huangua kilio kwa urahisi?" 


Mungu akasema:
"Wakati namuumba mwanamke nilitaka awe ni wakipekee, maalum.
Nilitengeneza mabega yake kuwa na nguvu ya kutosha kubeba uzito wa dunia, lakini mpole kutosha kutoa faraja.Nilimpa nguvu ambayo inamuwezesha kuendelea wakati kila mtu mwingine anapokata tamaa, na uwezo wa kuitunza familia yake hata kama akikutana na kikwazo cha ugonjwa na uchovu bila kulalamika. 

Nikampa nguvu ya kuvumilia kuzaa na uvumilivu wa kuudhiwa mara kwa mara na watoto wake. 
Nikampa usikivu na upendo kwa watoto wake chini ya yoyote na hali zote, hata wakati mtoto wake ana maudhi kwake vibaya sana. 

Nikampa nguvu na uvumilivu wa kubeba karaha ya mume wake na roho ya kusamehe makosa yake na kuwa kinga ya ubavu wake wa kulinda moyo wake.
Nikampa hekima ya kujua kwamba mume mzuri kamwe hawezi kutambua machungu ya mke wake, lakini wakati mwingine ni vipimo vya nguvu yake na imani yake vitamwezeshe kutatua na kuendelea kusimama karibu naye. 


Na hatimaye, nikampa uwezo wa kumwaga machozi. Hii ni ya kipekee kutumika wakati inahitajika. "
"Nahizo ndizo zababu zenyewe mwanangu," alisema Mungu, "uzuri wa mwanamke si katika nguo alizovaa, ama haiba aliyoibeba, au jinsi anavyo tengeneza nywele zake.
Uzuri wa mwanamke ni upo katika macho yake, kwa sababu ni mlango wa moyo wake -. Mahali ambapo upendo anaishi "


Iende kwa wanawake wote ambao hawachoki kupambana na hali zote zinazojitokeza katika maisha yao.Usiogope kulia pale inapobidi liaaaaaa dada baada ya hapo endelea kusimama!


source Dina marios

[ Read More ]

World’s Tiniest Teenager Wins Guinness World Record


Jyoti Amge of India has been recognized by Guinness Book of World Records as the world’s shortest woman. Jyoti was known as the world’s shortest teenager until she turned 18 this year. Guinness said in a statement Jyoti has grown less than one centimetre (0.4 inch) in the last two years and will not grow any taller due to a form of dwarfism called achondroplasia.

The teenager stands at 24.7 inches tall – 2.76 inches shorter than the 22-year-old American who had held the title since September. She weighs about 10 lbs.
[ Read More ]

Kampuni tano zaomba kujenga daraja Kigamboni


KAMPUNI tano zimejitokeza kuomba zabuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambazo moja kati ya hizo ndiyo itakayopewa dhamana ya ujenzi huo mara mchakato huo utakapokuwa umekamilika.

Akizungumza wakati wa kufungua zabuni hiyo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ludovick Mrosso, alisema awali kampuni saba zilijitokeza kuomba, lakini mbili kati ya hizo, zilishindwa kuwasilisha mchanganuo wake.

“Tunashukuru kuwa mwitikio umekuwa mzuri, hivyo kinachohitajika kwa sasa ni kumpata mshindi mmoja kutoka katika kampuni hizi tano ili tuweze kumkabidhi jukumu la ujenzi wa daraja hilo linalotarajiwa kuwa chachu ya uchumi katika sekta ya usafirishaji,” alisema Mrosso.

Alizitaja kuwa ni Long Jian Road and Bridge, Sichuan Road and Bridge Group, China Communication Construction, China Railway Contract Eng Group ikishirikiana na China Major Bridge Eng, zote za China.

Mrosso alisema hatua iliyofikiwa ni ya kwanza kuelekea nyingine na kwamba kinachosubiriwa kwa sasa ni mchujo kwa makandarasi hao ili kumpata mmoja atakayekabidhiwa jukumu la ujenzi huo.

Alisema wanatarajia kuwa mkandarasi atakayepatikana, atajenga daraja hilo kwa ufanisi na hivyo kumaliza kiu ya muda mrefu ya kuwepo kwa daraja hilo linalotarajiwa kuwa kiunganishi kizuri kwa wakazi wa Kigamboni.

Aidha, alisema ujenzi wa Daraja la Kigamboni ni mradi mkubwa kwa NSSF kusimamia katika kutoa huduma bora kwa jamii.
[ Read More ]

SIKU YA UKIMWI DUNIANI:MASHINE ZA KUNYOLEA NYWELE HATARI


      Wakati watanzania wakiungana na watu mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani Aids Week in Review linaandika:Wizara ya Afya naUstawi wa Jamii, imesema spiriti inayotumiwa katika mashine za kunyolea na vifaa vya kutengenezea kucha katika saluni za kike na kiume nchini Tanzania, haziui virusi vya Ukimwi.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hadji Mponda pamoja na kutoa kauli hiyo alisema njia pekee ya kuwa salama wakati wa kutumia vifaa vya saluni ni kuvitakasa(sterilization).

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema), aliyetaka kufahamu kauli ya Serikali juu ya matumizi ya vifaa vya saluni na uhusiano katika maambukizi ya Ukimwi na kamaspiriti zinasaidia kuua wadudu vikiwemo virusi vya Ukimwi. 

Alisema ili kuepuka uwezekano wa kutokea kwa maambukizi,wenye saluni na wanaokwenda katika saluni hizo waepuke kuchangia matumizi ya vifaa vyenye ncha kali.

Pia vifaa vyenye ncha kali vinapotumika kwa zaidi ya mtu mmoja ni vema vikatakaswa au kuua vijidudu kwa dawa.
[ Read More ]

WORLD AIDS DAY.Never give up.





Started in 1988, World AIDS Day is not just about raising money, but also about increasing awareness, fighting prejudice and improving education.  World AIDS Day is important in reminding people that HIV has not gone away, and that there are many things still to be done.



[ Read More ]