baada ya kuandika makala ya kwanza kuhusu keratoconus nimegundua kuwa kuna idadi kubwa ya watu wanaohitaji kujua zaidi juu ya hili tatizo na vilele juu ya tiba yake. na wapo wengine
ambao hawana ufahamu wowote juu hili na wapo wale ambao amegundulika na hili tatizi ila kwa njia moja ama nyengine wamekosa ufumbuzi wake.na leo nitaongea zaidi juu ya dalili na tiba yake.
kama nilivyokwisha eleza maana ya keratoconus ni hali ya kuendelea ambayo inafanya muundo wa kawaida
wa cornea ambao ni curve kwenda kwenye muundo wa cone.na vilevile nikatoa mambo yanayopelekea tatizo hili kuwa
ni urithi na mazingira..na sababu nyengine pia ni ukunaji wa macho kupindukia.
ukunaji wa macho kupindukia, kwa mtu mwenye matatizo ya macho ni kawaida kwake kujikuta na uwasho katika macho ambapo inapelekea yeye kutumia muda mwingi sana kujikuna.kitu ambacho ningependa kuwashauri ni kwamba kupunguza kufanya kujikuna na kujitahidi kuacha kabisa kwani ni sababu moja apo inayosemekana kupelekea keratoconus.
na miongoni mwa dalili za keratosconus ni;
*maumivu ya kicha na macho kwa ujumla
*kuwashwa kwa macho na kujikuna kupindukia.
*kushindwa kuendesha chombo wakati wa usiku
*kuona vitu viwiliviwili
*kuumizwa na muangaza
*kushindwa kusoma alama za barabarani
* blurring vision ambayo haitaweza kurekebishika kwa mawani isipokua kwa 20/20 with rigid,contact lenses.
*mabadiliko ya namba za miwani mara kwa mara.
kwa upande wa matibabu ya keratoconus yapo mengi na kwa hatua mbali mbali.kwanza kabisa mgonjwa pindi anapogundulika na keratoconus changa hutakiwa kuvaa miwani au contact lens,ambazo mara nyingi huwa si suluhisho ya tatizo hili,pia kuna treatment nyengine ambayo inaitwa Intacs,c3-r,na cornea transplant.
intacs ring
contact lens
classes
C3-R. Corneal Collagen Crosslinking with Riboflavin.
in 2008 FDA clinic ya nchini marekani ulikuja na tiba ya kuzuia tatizo hili ambalo kwa kitaalam inaitwa corneal collagen cross-linking (C3-R).
C3-R huzuia kuendelea kwa ukuaji wa kertocunus,naomba ifahamike kwamba c3-r haitabadisha shape ya cornea iliyoharibika na wala haitoondoa athari iliyotokezea bali inazua kabisa maradhi haya kuendelea kukua tena,na pia huondoa ulazima wa cornea transplant.vilevile c3-r inasaidia kupunguza namba ya miwani yako.ingawa wataalamu wanasema keratoconus inaendelea na baada ya muda inasita but hawezi jua hadi kipindi itakoposita yaweza kuwa imeshakuathiri kiasi gani.
\
watu wengi wamekua na uelewa wa tiba corneal transplant lakini ningependa kuwaambia kuwa tiba hii ni ya mwisho kabisa kwa tatizo hili pindi tiba zote zitakaposhindikana ingawa ma daktari wengi nchini tanzania wanawashauri wangonjwa kufanya cornea transplant.
Cornea Transplant.
ni surgery inayofanywa ku replace cornea kwa kutumia tissue ya mchangiaji mwengine mnaoendana.kusema ukweli cornea transplant sio suluhisho kamili ya keratoconus ila ndio hivyo lisilobudi kwani mgonjwa anaetakiwa kufanyiwa tiba hii ni yule ambae amekosa kabisa uwezo wa kuona na ameshatumia njia zote,
napenda kusema ukweli kuwa cornea transplant ni tiba yenye hasara nyingi pia,naomba ifahamike kwamba baada ya kufanyiwa cornea transplant bado utakua unahitaji miwani ili kuona vizuri.na pia huwa inachukua muda mkubwa ili ku recover na pia hata kama cornea transplant itafanikiwa kufanyika bila ya tatizo lolote hutarudi kwenye hali
yako ya kawaida kabisa..nakumbusha tena corneal transplant ni tiba ya mwisho kwa mgonjwa wa keratoconus.
kama una mtu mwenye tatizo hili nyumbani kwako au mtu yeyote unaemfahamu basi mshauri aende hospital na aulizie hii C3-R treatment na doctor atamueleza kama ni candidate mzuri
wa kufanyiwa hii treatment au la.
Inspire Me Daily.One Person Can Make a Difference.