Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

HAPPY-BIRTHDAY TO ME







Alhamis kama ya leo tarehe 25 kama ya leo mwezi wa 8 kama wa leo nilizaliwa..Namshuru Allah

subhanahu wataallah kwa kuwezesha mm kufika duniani kwa kunijaalia pumzi afya njema,amani

na utulivu ndani ya nafsi yangu,kwa kunijaalia mama bora zadi.Nakupenda mama na

                                            HAPPY-BIRTHDAY TO ME
[ Read More ]

TAFADHALI SOMA YAWEZA KUKUSAIDIA.



Sharing this story may save some life,may touch someone's life in a similar related problem,may bring hope to hopeless situation.yawezakua si wewe na unaweza kuchukulia just simple.ila yaweza kumgusa mwenzio na kupelekea ku save maisha yake..
tumekua tukiamka kila leo na kutembea , unaweza kujiona una nguvu na afya tele bila ya kujijua kuwa kuna ugongwa unakula ndani kwa ndani,
au unaweza kutokewa na hali isiyoya kawaida ya hafla ila ukapuuzia na kuipa kisogo,waweza kugundua tatizo kwa mtoto wako ndugu yako,jirani yako au mtu yeyote 
yule wa karibu bali ukajenga woga au  ukazarau na kutokutilia manane hali yake,bila ya kujua kuwa ukimya wako unazidi kuhatarisha maisha ya mwenzako huyo.

kila kiungo kina u.muhimu katika mwili wa binaadamu ila siku ya leo napenda kugusia zaidi kwenye  Macho.
CONE SHAPE YA CORNEA

KERATOSCONUS 
 ni jina kutoka Greek na ni  miongoni mwa magojwa ya macho.na naweza kuitafsiri kama hali ya kuendelea ambayo inafanya muundo wa kawaida
wa cornea ambao ni curve kwenda kwenye muundo wa cone.
 ukijiuliza chanzo au sababu ya maradhi haya jibu ni kuwa hakijulikani ingawa wana sayansi wamejaribu kuleta vyanzo tofauti.
wapo wanaosema ni urithi na mazingira yanachangia.keratoconus huathiri mtu mmoja kwenye watu zaidi ya 2000.ingawa kwa hivi sasa maradhi haya yanakua zaidi.
back to my story nilipokua na umri wa miaka 4 nilianza kupata tatizo la macho na baada ya kupelekwa hospital nilishauriwa kuanza kutumia miwani
jambo hili halikuungwa mkono na mama angu na ikambidi ajaribu kutafuta njia na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali..na ndipo aliposhauri badala ya kuvaa miwani nijaribu kutumia tiba mbalimbali na vyakula vitakavyonisaidi hadi umri wangu utakaposogea mbele
nilipofika std 5 hakukuwa na jinsi tena bali ni kurudi hospital na kuanza kuvaa miwani kwani tayari macho yangu yalishaanza kupoteza uwezo wa kuona bila ya masaada huo.
sikuwa napenda kuvaa miwani kwani yalikua yakinikosesha raha na kunizuia kushiriki katika michezo mbalimbali shuleni na badala ya takecare of myself inanibidi ni takecare of my glasses,haikua rahisi.

niliendelea kubadilisha miwani muda baada ya muda na kila siku ninapo kwenda kupima namba zangu zikawa zinabadilika.
sikutilia manani kwasababu sikuwa na elimu yeyote juu ya maradhi haya ya macho.inapotokea siku sioni tena basi ninachofanya ni kupima mawani mengine.

hali iliendelea kuwa hivyo na ikafikia wakati hata nikipima nakosa kipimo sahihi cha namba yangu. maisha niliyaona magumu sana kila unapofika muda wa shule maana hata ninapoingia darasani inanibidi kuchungulia daftari la jirani pindi mwalimu anapo andika notes na pale anapofahamisha inanibidi nimsikilize tu bila ya kuona anachoandika.
na ikawa inanibidi kutumia nguvu za ziada kuyalazimisha macho kuona kilichoandikwa ubaoni na hapo ndipo inapopelekea maumivu makali ya kichwa.kuishi na Keratoconus haikua rahisi kwangu kipindi chote cha elimu ya secondary kwanza nimekua nikiishi na ugonjwa
MUONO WA MTU MWENYE KERATOCONUS

nisioufahamu na pili wanafunzi wengi darasani wamekua wakinicheka pale ninaposhindwa kuandika na kukosa kuona kilichoandikwa ubaoni labda ni akili zao za kitoto au ni kutokuelewa kwao ila uwepo wa tabia yao hii mbaya ulikua ukinikosesha raha sana na ukiathiri maendeleo yangu,nikawa nachukia sana kufika shule.

2007 nilibahatika kwenda hospital kubwa ya macho kwa lengo la kutaka kupatiwa miwani.lakini sikuamini na nilihizunika sana nilipoambiwa huwezi kupata namba yako sahihi bali ni kutumia contact lens na ni ngumu sio  soft one.
                                              CONTACT LENS
kwa bahati mbaya  hospitali hapo licha ya kuhoji na kuwa na shauku ya kutaka kujua tatazi langu  sikuelezwa nini hasa kisayansi zaidi bali ni kuambiwa kuwa cornea yangu imebadilika shape,laiti kama ningeelezwa kiundani zaidi tangu kipindi kile ingesaidia sana na kuniokoa, tatizo limekua likikua siku hadi siku.. nilibahatika kununua contact lens na kuanza kutumia..
                                         CONTACT LENS
iliniwia vigumu mno kuzoea hali ile ya kila ufikapo asubuhi badala ya kuwahi darasani wewe uhangaike kuvaa lens.na kutokana na hali ya hewa ya vumbi
inanilazimu kuzivua kila mara ninapoingia mchanga machoni.baada ya miezi kadhaa ya uvaaji wa contact lens ikanilazimu kuacha na kurudia tena kwenye miwani yangu ingawa sikuwa naona vizuri

2008.nchini india nilifanikiwa kupata namba sahihi ya miwani na nikaanza kutumia. ila namba hiyo imekua ikibadilika siku hadi siku.nimekua nikipata namba tofauti kila ninapo tembelea hospital kwa vipimo.
2010, mwanzoni doctor akanishauri nifanye lasik eye surgery au kwa jina jengine tunaita laser treatment.tiba hii husaidia kurudisha vision yako na kupelekea ww kutokuvaa miwani tena.nilifarijika baada ya kusikia kuwa nitaweza ishi bila ya kuvaa miwani nikaendelea kujipa tamaa na kuendelea kuchanga pesa kwa ajili ya tiba hii..kipindi hichi chote sikugundua mabadiliko makubwa ila hadi pale ninapopima miwani mapya.mabadiliko hutoke kwenye namba.



 JUNE 2011  zanzibar ndipo niligundua  kuwa vision imebadilika kwasababu sikuwa na uwezo tena wa kuona vizuri bila ya miwani,kila nilipojaribu kuvua miwani nilichokua naona ni blurred.baada ya kuona mabadiliko haya nilikua siamini na nilikua nikilia every second ninapovua miwani na ikawa inanilazimu 
kushinda na miwani siku nzima kila sehemu.niliogopa sana na ku hofia naweza kukosa uwezo wa kuona..


                          MUONO WA MTU MWENYE KERATOCONUS

July 2011,Namshukuru Mwenyezi mungu kwa kunipa akili ya kufikiria kwenda  hospital kwa ajili ya kufanya lasik treatment,Pia namshukuru sana my dearest friend kwa kunipa moyo na kunishawishi kufanya hivi.Sushrutha eye hosptal chini ya Dk Pallavi ni hospital nzuri ya macho na inayoaminika..nikaamini kuwa pale nitapata tiba ya tatizo langu.
na baada ya Dk  kuniona akanieleza nije siku ya pili mapema kwa ajili ya vipimo.

July 15 2011.mapema asubuhi nilifika hospital na baada ya muda nikaona na Dk na kuanza vipimo kama alivyoniahidi..nilitumia nusu siku kwa ajili ya vipimo.na alichoniomba niwe msatahamilivu kwani macho ni kitu hatari sana na huwezi kukurupuka tu kwa kuchukua vipimo juu juu bali wanachotakiwa ni kurudia vipimo
na hadi kuhakikisha majibu waliopata ni sawa.nilimaliza vipimo vidogo na kwenda kumalizia na kipimo kinachoitwa orbscan .na ndicho kilichoonesha kuwa nina Keratoconius..
nilishindwa kujizuia nilianza kulia sana nilifikiria mambo mengi sana itakuaje baadae?je vipi kama hii hali ya kuchongeka kwa cornea haijasita what will happen after?
baada ya muda Pallavi Dk akanipatia njia pekee ambayo natakiwa kufanya na sio nyengineyo bali ni  C3-R (corneal collagen cross-linking riboflavin) hii ni aina ya tiba ambayo anatakiwa kufanyiwa mgonjwa wa  keratoconus ambae ameshatumia both classes and contact lens na kushindikana.
na sasa nipo kwenye process ya kutaka kufanya hii treatment miezi michache ijayo kabla hali haijawa mbaya zaidi..



MPENDWA MSOMAJI
                   Nimetoa mfano wa keratoconus sina maana ya kuwazungumzia wenye hili tatizo tu bali nina maana ya kuwafumbua na kuwaambia muwe makini na afya zenu na mmpendelee kuangalia afya zenu na msisubiri hadi tatizo liwe kubwa
na haliwezi kutibika tena.Tujaribu kujipenda na kujijali sisi wenyewe na pia tuelewe kuwa hakuna mtu atakae kuja kukushika mkono na kukuambia twende checkup ya tumbo or cancer na kadhalika.Ni wengi sana miongoni mwetu wameweza kuokoa afya zao baada ya kuona mabadiliko wamekimbilia hospital na baada y
a vipimo anaambiwa ni cancer inaanza ila tunaweza iwahi na ukapoa..Bado hujachelea,Bado una muda wa kuwahi afya yako,bado una muda wa kuchunguza afya yako,fanya hivyo leo na usingoje kesho,na tumia muda wako kumuelesha mwenzio na usijali jinsi gani
 atapokea ushauri wako.


 Remember Inspire Me
 Daily.One Person Can Make a Difference.You can change someone life.
Happy birthday to me.

[ Read More ]