Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

HAPPY NEW YEAR...





Namshukuru Mwenyezi mungu kwa kunijalia kuuona mwaka mpya wa kiislam na pia mwaka 2010..pia napenda kuwashkuru wale wote walionisupport kwa njia moja au nyengine ktk kuufanya mwaka 2009 kuwa so special...especial my belove mama. i love you mama.ila nawashkuru all hater kwa kunichukia na pia kunikatisha tamaa kuwa sitaweza kufanya kitu..kupitia chuki zao zimenifanya kuwa jasiri na kuwa na moyo wa kuendeleaza yale niliyopanga.....nimewasamehe wote walionikosea ktk njia 1 au nyengine ila kwa kuwa am not perfect nawaomba msamaha wote nilowakosea.....let us open another page with alot of success...amin thanks all... happy new year..





i love mama.you a so special......

[ Read More ]

HAPPY ISLAMIC NEW YEAR.Muharaam


                                     Nawatakia wadau wote furaha ya mwaka mpya wa kiislam.
                                          MAY ALLAH BLESS YOU ALL...AMIN.
            
[ Read More ]

ZANZIBAR BILA YA UMEME KWA MARA NYENGINE TENA.




Tanzania bila Ufisadi tutafika?Je Zanzibar Bila Umeme inawezekana?Kuchaji simu 500,Saluni kichwa 2000,Soda 1000,Juice 500,Barafu 200,Maji ya kawaida hayapatikani,Wanaofaidika sasa ni Wazinifu na wizi,Sasa wewe ulioko nje ukijaribu kupiga simu kwa ndugu zako ZNZ usishtuke zikiwa zimefungwa ufahamu hakuna matatizo ila ni umeme tu.


Waziri wa maji ameshatangaza mapema mwakani (2010) umeme utapatikana,Je tatizo kama hili sasa linataka kupelekwa Pemba?Tayari Mh.Karume ashapokea kila nyenzo za kutandaza umeme kutoka Tanga,lakini Je hafahamu kwanza usipoziba ufa,Utajenga Ukuta?



mdau.

[ Read More ]

Miss Gibraltar is Miss World '09


Miss Gibraltar, Kaiane Aldorino has been crowned the Miss World 2009. The first runner up is Miss Mexico Perla Beltran and South Africa's Tatum Keshwar came up second runner up.
[ Read More ]

[ Read More ]

[ Read More ]

Mahakama yaamuru hoteli ya Bwawani ipigwe mnada


Mahakama Kuu Zanzibar, imeamuru kupigwa mnada Hoteli ya Kimataifa ya Bwawani inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) baada ya kushindwa kulipa deni la mchele la Sh. trilioni 1.6 kwa muda mwafaka.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kampuni ya Leamthore Rice Ltd kutoka nchini Thailand kushinda kesi ya madai namba 4 ya mwaka 1997, dhidi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katika kesi hiyo, kampuni hiyo ilifungua mashitaka dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar, baada ya Serikali kuchukua mchele kutoka kampuni hiyo na kushindwa kulipa kwa muda mwafaka.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilifunga mkataba wa kibiashara kuchukua mchele kutoka katika kampuni hiyo na kuuza katika soko la ndani la Zanzibar.

Amri ya kupigwa mnada hoteli hiyo ya Serikali ilitolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Yesaya Kayange kufuatia hukumu iliyotolewa Mei 16, mwaka 1997 na Jaji Walfong Dourado.

Kwa mujibu wa barua ya Novemba 12, mwaka huu, uongozi wa Ushirika wa Mnada wa Kumekucha, umetakiwa kupiga mnada hoteli ya Bwawani ambayo ipo mita chache kutoka katikati ya Mji mkongwe wa Zanzibar.

“Ili haki itendeke, uendelee na utekelezaji wa hukumu ya kuuza Hoteli ya Bwawani Zanzibar”, alisema Mrajis huyo katika barua yake hiyo.

Mrajis huyo alieleza kuwa awali Mahakama iliamuru kupigwa mnada Shamba la Serikali liliyopo katika kijiji cha Kijichi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, lakini ilishindikana kutokana kutoeleweka kwa mipaka yake ya ardhi.

Akizungumza na Nipashe, Kiongozi Mwanadamizi wa ushirika wa mnada wa Kumekucha, Salim Ahmed Salim, alithibitisha kupokea amri ya Mahakama inayowataka kuipiga mnada Hoteli ya Bwawani ili kulipa deni la mchele iliyokuwa ikidaiwa Serikali.

Kampuni hiyo ilifungua kesi ya madai Januari, mwaka 1997 baada ya Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar, kushindwa kulipa deni la dola za Marekani milioni 69.4 na kutaka walipwe riba ya asilimia 25 na gharama zote za kesi.

Kampuni hiyo ilikuwa ikitetewa na wakili wake, Masumbuko Lamwai na Mahakama Kuu iliamua kutoa hukumu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi wakati huo, Omar Sheha Mussa, kushindwa kuzingatia wito wa Mahakama na kuamriwa kutolewa uamuzi huo.

Hata hivyo, upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ulichukua juhudi za kutaka kukata rufaa lakini muda ulikuwa umepita na hivyo kuamuliwa kulipwa kiwango hicho cha fedha pamoja na asilimia 25 ya riba tangu kutolewa kwa hukumu hiyo.

Kutokana na deni hilo kutolipwa kwa muda mwafaka, riba ya deni hilo iliendelea kuongezeka kutoka deni ya dola za Marekani milioni 69.4 hadi dola za Marekani biloni 1.6 sawa na bajeti ya miaka mitatu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo wakati wa Utawala wa Serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wake marehemu Idrissa Abdul Wakil na aliyekuwa Waziri Kiongozi, Maalim Seif Sharif Hamad.

Iwapo amri hiyo ya Mahakama itatekelezwa, kampuni nyingi zitaathirika kwa vile hoteli hiyo hivi sasa imepangishwa baadhi ya makampuni yanayofanya biashara ya utalii na uwakala wa mizigo.

Tayari wafanyabiashara marufu Zanzibar na wengine kutoka nje ya nchi, wameanza kufanya matayarisho ya kuinunua hoteli hiyo ambayo ilijengwa kwa nguvu za wazalendo baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964.


source;nipashe.

[ Read More ]