Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

ITS OFFICAL KATE MIDDLETON MARRIES THE PRINCE







[ Read More ]

MAMBO YALIVYOKUWA HARUSINI LEO KULE UINGEREZA KATIKA HARUSI YA KIFAMLE


Heheheheheeh Mr.Bean nae alikuwepo ndani miongoni mwa waalikwa...nampenda huyu baba jamani



Ilivyokuwa harusi ya Mjukuu wa malkia wa Uingereza,Prince William asubuhi ya leo....
Washangaaaji barabarani....wote hawa walikuwa wakisubiri kuona wanaopita na maharusi kwa ujumla... 


Wakenya nao naona wanawakilisha heheheheeheheh namuona mama wa kikenya akiwa katinga vazi lake la kimasai na mbele kaweka bendera yake pale kuonyesha nae alikuwepo hata kama barabarani...hii nafikiri ni kwa vile wapenzi hawa walivalishana pete za uchumba nchini Kenya.


Bibi harusi nae akiwasili katika gari la vioo ambalo sio tinted huku akipunga...akiwa anawasili kanisani kwa ajili ya kufunga ndoa.


Queen Elizabeth akiwasili kanisani kwa ajili ya harusi ya mjukuu...


Baba wa bwana harusi prince charles akiingia kanisani na mkewe Camilla 


Frower girls


Bwana harusi Prince William akiwasili kanisani...


Mke wa waziri mkuu msaidizi wa uingereza bi Miriam Gonzalez akishuka kwenye gari wakati akiwasili kwenye harusi 


Zara Phillip...mjukuu wa malkia Elizabeth kwa mtoto wake wa kike anaeitwa Anne ambae pia ni mtoto wa kike pekee wa malkia

Mama wa bibi harusi Carole Middleton akiwasili nae

Zile kofia pale kati...mweeeeeeee!!!

Mdogo wa bibi harusi

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon...

Queen Sophia,PrinceFelipe na princess Leticia wa Spain walikuwepo

Hapa princess Beatrice wa York akiwasili eneo harusi ilipofungwa..



Tara Palmer...huyu ni model,pia mtangazaji wa tvThe Backam...David & Victoria...naona tumbo la victoria limevaliwa kiatu kirefu...



Sir Elton John na mumewe....lol


Zile kofia leo nilibaki nashangaa mwenyewe....


[ Read More ]

Death Can Be Round The Corner

I wake up every morning. Within the first 30 minutes of waking up, I’m checking my e-mail and browsing the net. It’s a routine.

Before leaving for a journey, I know that I won’t get net access for a while, so I check my e-mail thoroughly and spend some extra time checking some stuff online, since I won’t be able to do so for the next little while.

In the same way, I study throughout the semester (a routine), but when it’s exam-eve, I take the extra moment to solidify the data in my mind for the exam.

In both these instances, I’m pretty sure that I’ll either be going on a journey or will be faced with an exam the next day, thus I take the time to prepare.

Alhamdulillah, through the blessing of Allah (SW) and the efforts of my parents, I have become accustomed to offering my 5 daily salat. Yet, it also has become a routine of sorts. I’m used to praying so I pray.

Many of those prayers are spent thinking about what I have to do next, while others speed-by while lost in thought about some other matter or pursuit. Although they are not the ideal salat, Insha-Allah, it is hoped that Allah (SW) will accept my duty of daily salat as being discharged, even with these semi-conscious prayers (which aren't supposed to be that way).

However, in contrast with the two examples in the beginning, I can never be sure if a salat will be my last.

During ta`leem this afternoon, a hadith caught my attention.

The Prophet (SAW) is reported (by many narrators) to have said, “Offer each salat (with) such (devotion) as if it were the last salat of your life.”

My thoughts suddenly rushed over to Southeast Asia and the tsunami disaster. Many Muslims perished (may Allah grant them all a place in Jannah). While walking out of the masjid, how many would have thought that they had just offered their last salat and that they will soon be swept to sea?

We can try to sweep it under the rug as much as we want, but the fact remains that (as I’ve said before), our birth certificates don’t carry expiry dates. The `Asr I have just prayed or the Maghrib I’m about to offer (Insha-Allah) may very well be my final call to Allah (SW) before He calls me back.

Before leaving for a journey or prior to an exam, I know that I better take the extra minutes to prepare and do it well, for I won’t get another chance in the near future. But when offering my salat, I don’t even know if I’ll suddenly find myself in an unexpected journey - from which there is no turning back.

Isn’t it ironic that I tend to sacrifice that which will (hopefully) help me in the Hereafter - when it all really counts - in exchange for short-term concerns that won’t help one bit in the Hereafter, and may even turn out to be a disadvantage for me?

Man, I’m such a fool.

May Allah (SW) help me and all of us in streamlining our thoughts towards Allah during our salat, and help us make each of our prayers as if they’re our last. Ameen.
[ Read More ]

Death Can Be Round The Corner. Ponder Over Death




Desirous to drive large, shiny cars,
essence of death - Car
REMEMBER: You will be driven one day as a horizontal passenger.




Wild and crazy over expensive clothes,
clothes when you're dead
REMEMBER: You will end up in just a 'KAFN.'




Recklessly sacrificing everything to construct beautiful homes and palatial mansions,
grave pit house
REMEMBER: the graveyard 'PIT' - one's real home.




Greedily devouring tasty dishes and all types of extravagant delicacies,
food
REMEMBER: one day YOU will be the meal for ants, worms and other insects.




Aspiring for fame, fortune, and bright lights.
reality of life
REMEMBER: the awaiting darkness and loneliness in the grave.
[ Read More ]

Rubani aokoa abiria 109, ndege yatua kwenye majani



NI ajabu lakini kweli, unaweza kusema vyovyote unavyoweza, lakini mimi nasema, mwacheni Mungu aitwe Mungu.


Nasema hivyo kwa sababu naamini kwamba, ndiye aliyewapa ujasiri marubani wa ndege ya United Airlines, Airbus 319 wakaweza kuiongoza ndege hadi ikatua kwa dharura baada ya mfumo WOTE wa utendaji wa ndege hiyo kufa wakati ikiwa angani dakika 20 baada ya kuruka katika uwanja wa ndege wa Louis Armstrong huko New Orleans, Marekani jana asubuhi.


Baada ya mfumo huo kufa, moshi ulianza kujaa kwenye chumba cha marubani hivyo walitafuta uwezekano wa kurudi uwanjani lakini hawakuwa na uwezo wa kujua wapo wapi, umbali gani kutoka juu, mwendo kasi, hali ya hewa, hivyo walitegemea miujiza tu.


Walikuwa angani lakini hawakufahamu walikuwa wapi, na umbali gani kutoka uwanjani au umbali gani kutoka ardhini, kwa bahati, waliweza kupata mawasiliano ya simu na mwongozaji ndege uwanjani, akawa anawaeleza waende kushoto au kulia, chini, chini, chini chini na waangalie alama wanazoweza kuzitambua ili wajue wapo wapi.


Kwa kuwa mfumo wote wa ndege hiyo ulikuwa umekufa, ilimaanisha kuwa hata ingefika uwanjani isingeweza kusimama kwa kutumia mfumo wa kawaida wa breki hivyo marubani walilazimika kutumia mfumo wa dharura (backup system) ulio nyuma ya ndege hiyo, Mungu akawasaidia ikatua kwenye majani ikiwa na kiasi kikubwa cha mafuta kwa sababu ilikuwa na safari ndefu.
[ Read More ]

Buriani Bi Rahma Mshangama


Leo baada ya Salat ya  IJumaa, maiti ya Maremu Bi Rahma Mshangama ilisaliwa katika msikiti wa Ijumaa Mwembeshauri, mjini Unguja na baada ya hapo ilienda kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwereke nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Bi Rahma Mshangama alifariki jana katika hospitali ya MnaziMmoja mjini Zanzibar, Marehehemu Bi Ramha alizaliwa tarehe 21 Aprili 1961 Kikwajuni Mjini Zanzibar na kupata elimu yake ya msingi mwaka 1969 mpaka 1978 katika skuli ya msingi na Sekondari ya Kidutani na Lumumba Zanzibar.

Mnamo mwaka 1979 mpaka 1981 alipata elimu ya Juu katika Chuo Cha Lumumba ambapo katika mwaka huo wa 1981 aliajiriwa katika Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo.

Mwaka 1985 mpaka 1987 alipata elimu ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Mkoani Morogoro ambapo mwaka 1991 alihudhuria mafunzo ya Utafiti wa Masuala ya Elimu na Ufugaji katika Chuo Cha Mifugo Afrika nchini Ethiopia.

Mwaka 1989-1990 alihudhuria mafunzo ya (MSC) Uzalishaji wa wanyama katika Chuo cha Reding University nchini Uingereza na mwaka 1991 alihudhuria mafunzo ya Ukuzaji Kilimo pamoja na Mafunzo ya Maendeleo ya Wanawake katika Kilimo nchini Uingereza na mwaka 1996 alihudhuria mafunzo ya Ubinafsishaji nchini Ireland.

Katika uhai wake Marehemu Bi Rahma Mshangama aliwahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Posta kuanzia mwaka 1996, na pia alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Uzalishaji wa wanyama nchini Tanzania kuanzia mwaka 1989 mpaka alipofariki.

Kwa upande wa nafasi alizowahi kushika Marehemu Bi Rahma Mshangama aliwahi kuwa Mkuu wa Idara ya Mifugo katika kitengo cha Mifugo mnamo mwaka 1987-1989, mwaka 1991 hadi 1992 alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Kamisheni ya Mashamba ya Serikali katika Wizara ya Kilimo na Mifugo.

Mwaka 1992 hadi mwaka 1995 alikwua msaididi wa Meneja wa Mradi wa Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa hapa Zanzibar na mwaka 1995 hadi mwaka 2000 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Wanawake na Watoto na mwaka 2000 hadi 2008 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili na Ushirika na mwaka 2008 hadi 2010 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto.

Hadi anafariki Bi Rahma Mshangama alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto. Bi Rahma Mshangama ameacha mume na Mama Mzazi.

Mapema katika hotuba ya Sala ya Ijumaa, akieleza sifa za Marehemu Bi Rahma Mshangama, Sheikh Fadhil Soraga alisema kuwa Bi Ramha Mshangama atakumbukwa daima kutokana na alikuwa mchapa kazi hodari na aliishi na jamii kwa wema mkubwa na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi, Amin
[ Read More ]

MAZIKO YA KATIBU WA WIZARA YA USTAWI WA JAMII, VIJANA WANAWAKE NA WATOTO.



                  Marehemu Rahma Mshangama enzi za uhai wake. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Rahma Mshangama, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa jamii,maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, aliyezikwa jana katika makaburi ya mwanakwerekwe mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, (katikati) na Makamo wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali,(wapili kushoto) wakijumuika na waislamu wengine kumuombea dua Marehemu Rahma Mshangama,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, aliyezikwa jana katika makaburi ya mwanakwerekwe mjini Unguja.
Wananchi na waislamu wakiubeba mwili wa Marehemu Rahma Mshangama,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa jamii,maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto,na kuzikwa makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, (wa nne kushoto) na Makamo wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali, (watatu kushoto) wakijumuika na waislamu wengine kumsalia Marehemu Rahma Mshangama, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, katika msikiti wa Mwembe Shauri Mjini Zanzibar jana.

Picha na Ramadhan Othman, Ofisi ya Rais Zanzibar.
[ Read More ]

IS-HAK GRADUATES @ UNIVERSITY OF MYSORE.. MANY CONGRATS.

Is-hak akipata picha ya kumbukumbu mbele ya jengo la University of Mysore 





Is-hak na wadau Charles na Hassan 

Is-hak  na rafiki
ishak
ishak


Ishak akipokea cheti cha kuhitimu shahada yake ya BCOM






wanafunzi wa Bcom class 2011 wakipata picha ya kumbukumbu pamoja na wageni rasmin
bcom class 2011    

Mdau Faresi Liymo na Ishak katika picha ya pamoja


Class 2011

Wageni rasmini na baadhi ya wahitimu wakikata keki



















[ Read More ]

'BABU' MPYA AIBUKA ZENJ




MGANGA wa tiba mbadala aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Msigwa kutoka Kigoma Tanzania amedai kuvumbua dawa aina ya 4A 9 Medicine inayotibu magonjwa sugu ikiwemo ukimwi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliotayarishwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) Mtaa wa Welesi Kikwajuni Mjini Zanzibar Msigwa alisema kwamba dawa zake zimetoa mafanikio makubwa sana kwa wagonjwa kadhaa aliowatibu hadi sasa.

Alisema dawa yake imenza kutumika zaidi ya mikoa 11 ya Tanzania Bara ikiwemo Kigoma, Arusha Mwanza, Iringa na mikoa mengine lakini pia jijini Dar es Salaam pia ametoa huduma hiyo kwa watu kadhaa.

Mganga huyo alisema alipata nafasi ya kwenda Nchini Muscat Oman na kufanya kazi kubwa sana ya kutoa huduma ambapo mgonjwa mmoja alikuwa akimuona kwa real 20 sawa na dola 50 za marekani ambapo wagonjwa wengi waliotumia daa zake walipona.

Matumizi ya dawa yake vipimo vyake unatumia kichupa kimoja au viwili hadi kupona kabisa hata hivyo alikataa kutaja inatokana na aina gani ya miti lakini alisema hiyo ni siri yake kwa kuwa dawa nyingi hutokana na miti ya majani hasa hizo zinazotumiwa katika hospitali kubwa za kimataifa.

Mganga huyo alisikitishwa na kukosekana ushirikiano kwa taasisi za juu za Afya ikiwemo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na ambapo imeshindwa kutambua dawa hiyo aliyodungua na kutibu.

Alisema hadi sasa ameweza kutibu zaidi ya wagonjwa wapatao 800 hapa Zanzibar katika kipindi kifupia alichokaa amekuwa akipokea wagonjwa wengi sana na wa maradhi mbali mbali ikiwemo maradhi ya kisukari, ukimwi na magonjwa ya akina mama.

Akitaja matumizi ya dawa zake Mganga huyo alisema kazi ya dawa hiyo ni kusukuma damu mwilini, kuongeza madini ya chuma, kuongeza kinga katika mwili na kujikinga na maradhi mbali mbali.

Mganga huyo alisema ujuzi wa matumizi ya dawa ambayo imegunduliwa miaka mingi lakini kwa zaidi ya miaka 13 sasa inafanya kazi ya kuwatibu wagonjwa mbali mbali ndani na nje ya nchi hiyo amesema awali dawa hiyo iligunduliwa na mama yake mzazi ambaye ameshafariki muda mrefu lakini kwa zaidi ya miaka kumi na tatu dawa hiyo amekuwa akiitumia kuwatibia watu mbali mbali ndani na nje ya nchi ikiwemo nchini Muscat Oman.

Aidha aliilaumu serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya kwa kushindwa kuitambua dawa hiyo ambayo imeshatibu watu tofauti na imekuwa ikiwapa nafuu wagonjwa wengi wa maradhi mbali mbali kwa madai kwamba dawa yake wanaifanyia utafiti jambo ambalo alisema limekuwa likisuasua.

“Tatizo liliyopo ni kati ya wataalamu wakizungu na sisi waganga wa tiba asili waganga wa dawa hizi za mitishama na ndio maana wakaweka kikwazo hiki kwamba wanaifanyia utafiti jambo ambalo linachelewesha dhana nzima ya utoaji tiba kwa wagonjwa” alisema mganga huyo.

Katika mkutano huo ambayo uliwashirikisha watu wenye kuishi na virusi vya ukimwi na asasi zisizokuwa na kiserikali Mganga huyo alisema dawa yake imetambuliwa na Baraza la Tiba Asilia la Zanzibar pamoja na bodi ya chakula na vipodozi na kwa sasa amekuwa akitoa dawa zake kwa urahisi na wagonjwa wengi wamekuwa wakienda kuchukua dawa zake.

Alisema watu walioathirika na virusi vya ukimwi na wagonjwa wengine wamekuwa wakitegemea dawa zake lakini aliwataka wagonjwa kutovunjika moyo na matumizi ya dawa hizo ambazo amesema yupo tayari kutoa tiba kwa kuwasaidia wagonjwa wanne ambao atawapa dawa bure iwapo watakubali kwenda kuangaliwa afya zao kwanza kabla ya kutumia dawa hizo.

“Mimi sharti langu ni kwamba kabla hujatumia dawa zangu basi hutaka lazima ukachekiwe afya yako na upimwe kwanza ili ukija kutumia nijua ni virusi vingapi ulivyonavyo mwilini na baada ya kumaliza kutumia dozi yangu pia hutaka wende ukapime vile vile ili tujue waliobaki na kama wameshamalizika” alisisitiza mganga huyo.

Akifafanua kwamba baadhi ya watu wenye virusi vya ukimwi kwa watu wenye CD4 kiwango cha 427 na baada ya wiki mbili mgonjwa huyo huyo CD4 zake ziliongezeka na kufikia 613.

“Mimi dawa yangu inayo uwezo wa kuongeza CD4 kwa muda wa wiki moja tofauti na zile za kupunguza makali ya virusi za ARV na kabla ya kumpa mgonjwa dawa nataka kwanza akapime na aje na vipimo vyake ndipo aweze kutumia daa hizi” alisema Msigwa.



Akitoa ushuhuda wa magonjwa yaliokuwa yakimsumbua mmoja ya wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Jaffar Masale ambaye alidai awali kuwa na ukimwi lakini baada ya kutumia dawa hiyo amepona kabisa kwa mujibu wa vipimo alivyopewa huko katika hospitali mbali mbali alizokwenda kupimwa.



“Kwa kweli niseme kwamba nilikuwa katika hali mbaya sana baada ya vipimo kubaini kwamba nimeathirika na ukimwi na nilikuwa naharisha na ngozi yangu yote kuharibika lakini baada ya kutumia dawa hiyo sasa nipo salama na ninaweza kufanya kazi zangu vizuri sana na ninashukuru kwamba hivi sasa nimepata nguvu ya kufanya kazi” alisema Masale.



Shuhuda mwengine ni mhadhiri wa chuo kikuu, Abdulkadir Mohammed amesema yeye alikuwa akizumbuliwa na malaria sugu ambayo kwa miezi kadhaa amekuwa akitumia dawa bila ya mafanikio lakini baada ya kutumia dawa za Mganga huyo amepona na amekwenda kupima ameonekana amepona kabisa.

“Nilikuwa nimeshachoka kutumia madawa ya kila aina lakini nashukuru kwamba nilipotumia dawa za Dk Msigwa nimepona kabisa lakini nilipokwenda hospitali kupima nikaulizwa nimetumia dawa gani lakini sikutaka kusema dawa niliotumia lakini kwa ufupi dawa nilizotumia ni hizi hizi” alisema mhadhiri huyo katika mkutano huo.



Msigwa alitoa ombi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupatikana kwa mashine ya kujuwa kiwango cha virusi katika damu ya binaadamu inayojulikanana kwa jina la 'Viral load' ili wananchi wapate kwenda kupima afya zao kupitia kipimo hicho.

“Mashine hii ni muhimu sana ambayo ikipatikana itawasaidia wagonjwa kujuwa kiwango cha virusi katika damu yao ....kwa sasa wagonjwa hao wanakwenda Dar-es-Salaam kupima lakini ikipatikana hapa itakuwa rahisi kujulikana vipimo vyao badala ya kupoteza nauli kufuata huduma hiyo mbali”alisema Msigwa.

Msingwa alisema hakuna kipimo hata kimoja kinachoweza kukuonesha mgonjwa ambaye ana vizuri vya ukimwi na baadaa ya kutumia dawa vipimo vikaonesha kwamba hana ukimwi.


“Mimi nawashangaa watalaamu wa tiba unapokwenda kupima daktari anaokwambia kuwa wewe una virusi idadi kadhaa maana idadi ya virusi ni kubwa inafika millioni 50 na zaidi lakini ukishatumia dawa ukenda tenda wanakwambia virusi vyao vimemalizika mwilini sasa kama virusi vimemalizika madaktari wanasita nini kusema kwamba wewe umepona? Alihoji Mganga huyo na kuongeza kwamba “hakuna kipimo duniani kitakachokuonesha kwamba wewe ni positive na baadae upime tena kipimo hicho kiseme wewe ni negative kipimo hicho hakuna duniani kote” alisema.
[ Read More ]