
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepata malalamiko kutoka kwa watumiaji wa simu za mkononi kwamba kuna ujumbe unaosambazwa kwamba ukipokea simu utapata madhara. Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba taarifa zinazoenezwa