Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Tamasha la 12 la kimataifa la filamu laanza Zanzibar

TAMASHA la 12 la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF), 2009 limezinduliwa rasmi jana mjini hapa katika eneo la Mji Mkongwe, viwanja vya Ngome Kongwe kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

Burudani kutoka kwa mshairi Mrisho Mpoto 'Mjomba', Beni na Siti zilipamba uzinduzi wa tamasha hilo ambalo litaendelea hadi Julai 12.

Baada ya uzinduzi huo, filamu ya Izulu Lami (My Secret Sky) ya dakika 93 ilionyeshwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzu wa ZIFF, Profesa Muhando, Watanzania wameingiza filamu 13 katika tamasha hilo na mgeni wake rasmi anatazamiwa kuwa muigizaji maarufu wa Hollywood, Danny Glover.

Danny Glover anatarajiwa kwasili nchini Jumatatu tayari kwa ratiba ndefu ikiwa ni pamoja na mwaliko wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) na kuwatembelea watoto walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

[ Read More ]

Sheikh Suleiman Gorogosi afariki dunia katika ajali ya gari



KAIMU Mufti wa Tanzania, Sheikh Suleiman Gorogosi amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea kwenye Kijiji cha Mnolela Wilaya ya Lindi Vijijini baada ya tairi ya mbele ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Mtwara kupasuka na kupinduka.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Sifuel Shirima zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 8:09 katika barabara ya Mtwara-Lindi wakati akitokea Uwanja wa Ndege Mtwara baada ya kushuka kwenye ndege akitoa jijini Dar es Salaam.

Kamanda Shirima alisema katika gari hilo kulikuwa na watu watatu, akiwamo Bakari Maguo, mfanyabiashara wa Lindi ambaye ni mmiliki wa gari hilo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Lindi mjini, Bakari Fundi ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Ligula mkoani Mtwara.

Gorogosi alikuwa amekwenda Lindi kufungisha ndoa ya mtoto wa Maguo ambaye ni mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambayo ilikuwa ifungwe leo.

Ndugu wa marehemu Abilahi Mohammed aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa mazishi wa Gorogosi ambaye alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Lindi yatafanyika saa 10:00 jioni leo jioni mjini humo.

Pia Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata), lilitoa taarifa jana jioni likieleza kuwa Gorogosi lilithibitisha kifo cha Gologosi na kueleza kuwa atazikwa leo.

Marehemu ameacha wake wawili. Kabla ya kifo chake alikuwa pia mjumbe wa baraza la Ulamaa la Bakwata.

Siku za hivi karibuni, Sheikh Gorogosi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambao ulimfanya kulazwa katika hospitali binafsi ya Fire jijini Dar es Salaam kwa wiki mbili, na juzi aliruhusiwa kurudi nyumbani kabla ya kwenda Lindi.

Mufti Sheikh Issa Bin Shaaban Simba alivunja baraza la maulamaa na kamati ya hija ya baraza hilo na kuviunda tena vyombo hivyo, huku akimkabidhi kukaimu nafasi yake Sheikh Gorogosi.

Mufti Simba, ambaye awali alikuwa Sheikh wa Bakwata Mkoa wa Shinyanga, alichaguliwa na Mkutano Mkuu wa Bakwata kushika wadhifa wa Umufti Oktoba 13, mwaka 2002, mkoani Dodoma katika uchaguzi ambao, masheikh tisa walijitokeza kuwania wadhifa huo. 



Masheikh hao, ni pamoja na marehemu Sheikh Gorogosi, Sheikh Suleiman Kilemile, Mbunge wa zamani wa Kibiti, Profesa Juma Mikidadi, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Ma`amur, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ahmed Twalib, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Manyema, Kariakoo, Hamid Jongo.

Wengine, ni aliyekuwa Naibu Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Bakwata, Sheikh Ahmed Zubeir, Sheikh wa Bakwata Mkoa wa Kigoma, Tawfiq Malilo na aliyekuwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Idara ya Dini (Kitengo cha Usuluhishi) ya Bakwata, Sheikh Twaha Majaliwa.

[ Read More ]

Michael Jackson 'hakufanyiwa hila'


Madaktari waliochunguza kifo cha mwanamuziki maarufu wa mtindo wa Pop, Michael Jackson, aliyefariki dunia Alhamisi, wamesema matokeo ya awali hayajaonyesha hila yoyote.

Lakini vipimo vingine vikiwemo vya sumu vimechukuliwa ambapo uchunguzi wake unaweza kuchukua majuma kadhaa, ofisi ya mchunguzi wa vifo vya Los Angeles ilieleza.

Maafisa wamesharuhusu ndugu kuuchukua mwili wa Jackson, lakini bado hakujawa na taarifa zozote kuhusu mazishi yake.

Waombolezaji wakiwemo wasanii wenzake, viongozi wa mataifa mbali mbali na mashabiki wamekuwa wakitoa rambi rambi zao kwa mwanamuziki huyo.

Jackson aliyekufa akiwa na umri wa miaka 50, siku ya kifo chake alikimbizwa hospitalini huko Los Angeles, Marekani, baada ya kupata matatizo yanayodhaniwa kuwa ya moyo.

Taarifa za awali zilieleza kuwa mwanamuziki huyo alikuwa hapumui wakati madaktari wa huduma ya kwanza walipofika kumsaidia nyumbani kwake maeneo ya Bel Air yapata saa sita na nusu majira ya huko. Lakini mwishowe maafisa wakathibitisha kifo chake.

Utata mkubwa uligubika hali ya afya ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na albamu mbali mbali kama Thriller.

Wavuti ya TMZ ambayo huandika taarifa za watu mashuhuri katika maswala ya burudani ilikuwa ya kwanza kuandika kuwa Michael Jackson mwenye umri wa miaka 50 alikuwa ameaga dunia.

Vile vile, gazeti maarufu la Los Angeles Times liliandika katika wavuti yake kuwa Michael Jackson amefariki. Lakini vyombo vingine vya habari vilikuwa vikisema alikuwa bado yu hai, ingawa alikuwa mahututi.

Madaktari wa huduma ya kwanza walijaribu kuuzindua moyo wa Jackson wakati gari ya wagonjwa ilipokuwa ikimkimbiza katika hospitali ya UCLA, maafisa wameeleza.

Jackson alikuwa akitarajiwa kuanza matamasha mbali mbali ya kufufua kipaji chake kwenye ukumbi wa O2 jijini London ifikapo tarehe 13 Julai.

Imeelezwa alikuwa na historia ya matatizo ya kiafya na hajawahi kukamilisha ziara ya matamasha kwa kipindi cha miaka 12 iliyopita.




[ Read More ]