Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;Jambo ninalotaka kulizungumzia sasa sikutaka kulizungumza kwa sababu Waziri Mkuu alishalifafanua baada ya semina ya Wabunge wa CCM na hata Mheshimiwa John Chiligati, Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa alishalizungumzia. Sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa sababu viongozi wenzangu hao wameelezea kwa ufasaha uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa kikao cha pamoja cha Wabunge