Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Eti wanawake wenye kipato kisichopungua Milioni 3 kwa mwezi hawaoleki




Inadaiwa kwamba mwanaume anapooa mwanamke ambaye ana mafanikio na ambaye ni msomi au mwenye taaluma, ajue kwamba, ndoa yake imeegeshwa kwenye mawe.

Tafiti za hivi karibuni kabisa zinaonyesha kwamba wanawake wenye mafanikio ya kimasomo pamoja na kipato wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupambana na talaka ukilinganisha na wanawake wa kawaida. Siyo hivyo tu, pia wanaonekana kuwa wako kwenye nafasi ya kutoka nje ya ndoa kirahisi na kutojali sana kuhusu watoto.
Utafiti ulioripotiwa kwenye jarida la Social Forbes kwa mfano, unaonesha kwamba, wanawake wenye mafanikio ya kitaaluma pamoja na kipato hata wanapopata watoto, furaha yao haiwi kubwa kama ya wanawake wengine.
Wanawake hawa hupenda kuona waume zao wanakuwa chini yao kimapato. Hapa kuna utata mkubwa kwa kuzingatia kwamba, wanaume wenye mafanikio hupendelea wanawake wa kaliba yao. Hivyo wanapooana nao ndoa ni lazima iyumbe sana kwa sababu hawa wanawake nao wanataka kutokeza pembe zao.
Kwa kadiri mwanamke anavyostawi kimapato na kupanda juu kitaaluma au hata kicheo, ndivyo ambavyo hamu yake kwa mumewe ambaye naye ana mafanikio inavyopotea.

Kuna mambo mengi yanachangia kufanya ndoa kuwa imara au kuyumba na pengine kuvunjika. Kwa mfano mtu ambaye ametoka familia iliyovunjika kwa talaka, anaweza kuingia kwenye talaka kirahisi, umri wa kuolewa, imani na sababu nyingine zinachangia. Lakini mafanikio ya kipato ni jambo lingine kubwa.
Nikisema mafanikio, nina maana wanawake ambao wamemaliza elimu ya chuo kikuu na ambao pato lao kwa mwenzi haliwezi kuwa chini ya shilingi milioni 3. Je mmeelewa sasa wanawake ninaowazungumzia…?

Kama inabidi tuamini tafiti zote ambazo zimefanywa kuhusu wanawake hawa, ina maana kwamba, kuoa wanawake wa aina hii ni hatari sana. Nasema ni hivyo kwa sababu tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wanawake wenye mafanikio kitaaluma pamoja na kipato, huteleza sana kwenye ndoa


source-jamii forum.
[ Read More ]