
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, limefanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi lilokuwa lifanyike mara baada ya kuchukuliwa kwa mishahara ya watumishi wa hoteli moja ya Kitalii. Afisa Habari wa Jeshi hilo Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa jaribio hilo limezimwa na Polisi jana Alhamisi Desemba 29, 2011 majira ya saa 7.00 mchana baada ya makachero wa Jeshi la Polisi